Bunge la Ulaya laitaka Tume kufuta Ufadhili wa Mwaka 2026 kwa Tanzania

Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio la kuitaka Tume ya Ulaya kufuta rasimu ya mpango wa ufadhili wa kiasi cha Euro milioni 156 uliotengwa kwa ajili ya Tanzania kwa mwaka 2026. Uamuzi huu umefikiwa kufuatia kile bunge hilo linachokieleza kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia baada ya uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 2025, ambapo serikali ilitumia nguvu kuzima maandamano na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kukamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Sababu za Bunge la Ulaya: Wabunge hao wameishutumu Tume ya Ulaya kwa kupuuza wasiwasi wao na kuandaa rasimu inayoenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya. Vilevile, wameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukwamisha ziara ya ujumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya bunge hilo iliyolenga kufuatilia utawala wa sheria. Kutokana na dosari hizo, wameagiza kuandaliwa kwa rasimu mpya itakayohakikisha kuwa fedha za msaada zinaelekezwa moja kwa moja kwenye kutoa huduma za msingi kwa wananchi, kulinda demokrasia, na kusaidia asasi za kiraia pekee.

Matukio Yaliyochochea Mvutano: Chimbuko la msimamo huu mkali ni mwendelezo wa matukio ya ukandamizaji wa kisiasa nchini humo. Hii inajumuisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyokiri kuwa zaidi ya watu 518 waliuawa kwenye vurugu za uchaguzi bila wahusika kuwajibishwa, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa haki. Zaidi ya hayo, bunge hilo limekumbushia kulaani kwake kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa yanayoweza kusababisha adhabu ya kifo, likisisitiza ulazima wa kumuachia huru na kumlinda.

Soma, Pia

View attachment 3610467View attachment 3610466
Ngoja sasa hao matunge wanyimwe misaada tuone watatunishia nini vitambi huko serikalini.
 
Haya mambo ya kumsikiliza Kabudi na Kombo yataleta shida...

Hivi Serikali haijui kwamba haya makelele huko Ulaya yanapunguza kuaminika kwa Serikali...

Inapunguza investment za watu wa Ulaya kuja Tanzania

Tunaonekana hatuna ustaarabu kama binadamu..

Kuna Doctor mmoja yupo Ocean Road..kaniambia alienda ubalozi wa EU akiwa na hofu ili wasisitishe misaada ya dawa za cancer..bahati nzuri akajibiwa hizo dawa zitaletwa kama kawaida maana zinahusisha jamii

Dawa za cancer ni bei mbaya..EU wanatoa dawa na vifaa tiba kwa mwaka inazidi billion 50... Na sisi tunajidai kukimbilia Urusi...

Hawa EU wanataka tuheshimu haki za binadamu....sisi tunajibu eti ni utamaduni wetu ..mara wasituingilie...
Sasa kwanini tunawaomba Hela kama hatutaki wasituingilie?
Na hii ya kuteka watu, kuwauwa,kuwaonea, kuwafunga bure sidhani kama nao ni utanaduni wetu toka lini na iwapo umeandikwa katika katiba yetu ya 1977
 
Nawaza tu,ingawa chadema watafurahi kiasi cha hata kunywa bia baridi, lakini nimetafakari sana,je?
*Tukipandisha bei ya unity ya umeme wa majumbani,
*Tukapandisha bundle za internet
*Tukapunguza safari za nje kwa watumishi
*Tukapunguza vikao na posho mbalimbali,
*Magari mengi /yote ya umma yakawa ya nishati ya umeme
*Tukaweka kodi ya kichwa,ya 10000 kwa mwaka,
*Ruzuku zikaondolewa kwa vyama vya siasa
HAPO VIPI?
Wananchi watakuondoa hatimaye
 
Samia akitoka ataishi kwa hofu kubwa kwanza akifariki familia yake itakuja kuteseka sana maana Ulaya hawaingii tena na pesa zao zitataifishwa kama zilizotaifishwa pesa za Mtoto wa Mobutu na Viongozi wengine wa aina yao.
Ni kweli kabisa. Je kwa Samia kuishi kwa hofu italeta nafuu ya maisha kule kijijini despite the sanctions?
 
Na hii ya kuteka watu, kuwauwa,kuwaonea, kuwafunga bure sidhani kama nao ni utanaduni wetu toka lini na iwapo umeandikwa katika katiba yetu ya 1977
Umewahi kumsikia Kizimkazi akizungumza ?

Hatutaki kuingiliwa, tutamaliza matatizo kulingana na Mila, desturi na tamaduni zetu..

Angalia tume zinaundwa kupoteza muda, kukwepa uwajibikaji...nk

Sasa hii ndio Mila na tamaduni zetu kitabia
 
Wanapiga picha za kwenye makorido afu wanatunga eti tumeshajadili 😂 kiko wapi? Hayo mamilion ya pesa mnazotumia kuzurura huko. Ulaya pelekeni shuleni watoto wapate zana za kujifunzia nguchiro nyie
 
So Samia ndo atakayeteseka na CHADEMA sasa itapeta
Sasa wewe, cdm inapoteza nini kwa mfano! Wanaoumia sana ni ccm ambao watapoteza serikali wanayoiongoza kimagumashi.
Kwa taarifa yako na machawa wenzako jiandaeni kwa mapigo mfuatano kwani zanzibar anakwenda kujitoa kwenye muungano wenu feki kwani hawezi kuwa sehemu ya shida zenu.
 
Wananchi wakiteseka sana, wanaungana na ndio wataandamana kuwatoa viongozi
umeweza kama mimi: kingine hiyo hela wanayopewa na CCP itabidi kuigawanya kidogo inaenda kwa machawa na kidogo inanunua kofia na t-shirt apo bado hawajanunua wapinzani baadae tunaelewana tu. Alafu wakumbushe SGR ya Mwanza to Isaka haijakamilika na wakati mkataba unasainiwa ilikuwa ndani ya miezi 36 iwe imekamilika
 
Hizi sasa ndo akili?
Mpk sasa hujui kuwa mishahara na posho za Samia na genge lake kupitia kodi yako itaendelea kama kawaida lkn kijijini kwenu watateseka?
Kwani ni lini matatizo ya wanakijiji yaliwahi kuisha? Maji, matibabu, miundombinu na elimu ni shida toka dunia iumbwe, itakuwa leo?
Mtaji wa ccm ni maskini na ndio maana wanapigana kufa na kupona ili kuzalisha maskini wengi zaidi.
 
umeweza kama mimi: kingine hiyo hela wanayopewa na CCP itabidi kuigawanya kidogo inaenda kwa machawa na kidogo inanunua kofia na t-shirt apo bado hawajanunua wapinzani baadae tunaelewana tu. Alafu wakumbushe SGR ya Mwanza to Isaka haijakamilika na wakati mkataba unasainiwa ilikuwa ndani ya miezi 36 iwe imekamilika
 
Wabunge wa Bunge la Ulaya (MEPs) wamepitisha azimio la kuitaka Tume ya Ulaya kufuta rasimu ya mpango wa ufadhili wa kiasi cha Euro milioni 156 uliotengwa kwa ajili ya Tanzania kwa mwaka 2026. Uamuzi huu umefikiwa kufuatia kile bunge hilo linachokieleza kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na misingi ya kidemokrasia baada ya uchaguzi mkuu wenye utata wa Oktoba 2025, ambapo serikali ilitumia nguvu kuzima maandamano na kusababisha vifo vya mamia ya watu na wengine wengi kukamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Sababu za Bunge la Ulaya: Wabunge hao wameishutumu Tume ya Ulaya kwa kupuuza wasiwasi wao na kuandaa rasimu inayoenda kinyume na sheria za Umoja wa Ulaya. Vilevile, wameikosoa Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kukwamisha ziara ya ujumbe wa Kamati ya Haki za Binadamu ya bunge hilo iliyolenga kufuatilia utawala wa sheria. Kutokana na dosari hizo, wameagiza kuandaliwa kwa rasimu mpya itakayohakikisha kuwa fedha za msaada zinaelekezwa moja kwa moja kwenye kutoa huduma za msingi kwa wananchi, kulinda demokrasia, na kusaidia asasi za kiraia pekee.

Matukio Yaliyochochea Mvutano: Chimbuko la msimamo huu mkali ni mwendelezo wa matukio ya ukandamizaji wa kisiasa nchini humo. Hii inajumuisha ripoti ya tume ya uchunguzi iliyokiri kuwa zaidi ya watu 518 waliuawa kwenye vurugu za uchaguzi bila wahusika kuwajibishwa, na hivyo kukwamisha upatikanaji wa haki. Zaidi ya hayo, bunge hilo limekumbushia kulaani kwake kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, kwa mashtaka yanayochochewa kisiasa yanayoweza kusababisha adhabu ya kifo, likisisitiza ulazima wa kumuachia huru na kumlinda.

Soma, Pia

View attachment 3610467View attachment 3610466
Safiii
 
IMG_1943.png
 
Nawaza tu,ingawa chadema watafurahi kiasi cha hata kunywa bia baridi, lakini nimetafakari sana,je?
*Tukipandisha bei ya unity ya umeme wa majumbani,
*Tukapandisha bundle za internet
*Tukapunguza safari za nje kwa watumishi
*Tukapunguza vikao na posho mbalimbali,
*Magari mengi /yote ya umma yakawa ya nishati ya umeme
*Tukaweka kodi ya kichwa,ya 10000 kwa mwaka,
*Ruzuku zikaondolewa kwa vyama vya siasa
HAPO VIPI?
Akili za kuikomboa nchi zimeishia hapo? Unapandisha kutoka kwa wananchi wenye vyanzo vipi vya mapato? Hiyo ni kuzidisha ukali wa maisha ambapo itafikia hatua watu watasema INATOSHA NA WATAFANYA MAAMUZI. NA UTAKUWA USHINDI WA WALIO WEKA VIKWAZO.

umejaribu kufikiria kwa mtazamo huo baada ya miaka mi 3 hali itakuwaje?
 
Back
Top Bottom