Pre GE2025 CCM wamchangia Lissu Milioni 5 atengeneze gari lake. Lissu azipokea
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Alikataa ile hongo ya Abdul sasa Msigwa kamtumia Nchimbi.

Kuna issue Ccm wana itega kwa Lissu. Soon ita kuwa wazi. Usishangae Lissu akaenda kupokelea huo mchango Lumumba
Humfahamu Lisu vizuri mkuu, kwanza kafanya jambo la busara sana kupokea hizo 5M, karuka kiunzi vizuri sana
 
Kuachana nayo si sahihi, hiyo pesa haijatoka kwenye mfuko wa CCM, kwani Lissu hana ndugu wanachama wa CCM, nao awakatae! Hapana.
Mchango huu angepewa Zito au Mbatia sijui uzi huu ungekuwa kwenye page ya ngapi sasa hivi.

Ila kwa vile kapewa Lisu basi hakuna tatizo na watu wameandaliwa kabisa kuja kumtetea.

Tanzania Mbowe akienda kuonana na viongozi wakuu wa CCM kimya kimya, wakapatana yao bila taarifa za kueleweka haina shida.

Lisu akichangiwa na wana CCM haina shida. Ila shida ni pale tu hayo yaliofanywa na Mbowe pamoja na Lisu yakifanywa na mtu kama Lipumba au Mbatia.

Hii imefanya kina Lisu waamini kwamba bado wana kundi kubwa la wapumbavu nyuma yao. Wanaweza kufanya lolote na ikibidi hata kushirikiana hata na hao wanaojifanya kuwa maadui zao (CCM) kuihujumu nchi kwa vile wanajua fika kuwa baada ya hujuma hizo kuna mipumbavu itakayokuja kuwatetea na hivyo kuendelea kuishi kupitia siasa hizi za kupigania matumbo yao na familia zao.
 
Hatuzitaki lissu asipokee hii politiki ya kinafiki kinachofwata watamuuliza zile walizochangia wananchi zimeenda wapi huo ni mtego.
Itafuata masimango na pia ni drama ya kuzima uhuni uliofanywa na wale wanaoona wanaweza kufanya chochote bila kuhojiwa wakiamini ndio dola yenyewe.
 
Humfahamu Lisu vizuri mkuu, kwanza kafanya jambo la busara sana kupokea hizo 5M, karuka kiunzi vizuri sana
Wengi hawajaelewa ila alichokifanya ndo sahih zaid kakikataa kimbola cha wanasisiemu kiulaini kabisa.
 
Mchango huu angepewa Zito au Mbatia sijui uzi huu ungekuwa kwenye page ya ngapi sasa hivi.

Ila kwa vile kapewa Lisu basi hakuna tatizo na watu wameandaliwa kabisa kuja kumtetea.

Tanzania Mbowe akienda kuonana na viongozi wakuu wa CCM kimya kimya, wakapatana yao bila taarifa za kueleweka haina shida.

Lisu akichangiwa na wana CCM haina shida. Ila shida ni pale tu hayo yaliofanywa na Mbowe pamoja na Lisu yakifanywa na mtu kama Lipumba au Mbatia.

Hii imefanya kina Lisu waamini kwamba bado wana kundi kubwa la wapumbavu nyuma yao. Wanaweza kufanya lolote na ikibidi hata kushirikiana hata na hao wanaojifanya kuwa maadui zao (CCM) kuihujumu nchi kwa vile wanajua fika kuwa baada ya hujuma hizo kuna mipumbavu itakayokuja kuwatetea na hivyo kuendelea kuishi kupitia siasa hizi za kupigania matumbo yao na familia zao.
Aliyetoa ndege ya kumpeleka Lissu Nairobi alikuwa mwanaccm, Ssmia alikwenda Nairobi kumjulia hali hosipitali, na wengine wanaccm ni ndugu zake. Tujifunze kutofautisha chama na maisha ya mtu binafsi, mali yangu si mali ya Simba au Yanga au CCM au CUF.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani humo wamemchangia Shilingi Milioni Tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanyia matengenezo gari yake.

Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza alimuomba Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi kuhamasisha wanachama wa CCM kumchangia Lissu ili gari hilo limuwezeshe kufanya shughuli za siasa.

Kwa upande wake, Dkt Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono pale panapobidi kwani wanasiasa wote wanaijenga Tanzania.
Alipotafutwa kuzungumzia kitendo hicho kilichofanywa na CCM, Lissu amewashukuru CCM kwa mchango na kwamba atazipokea fedha hizo kama ambayo amekuwa akipokea kutoka kwa makundi tofauti ya watu.

"Nawashukuru, kama nilivyosema...hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao, kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa," amesema Lissu.

Mwananchi
Lissu ni Mtu wa Watu.

Huyu Jamaa Mungu yuko pamoja naye.
 
Humfahamu Lisu vizuri mkuu, kwanza kafanya jambo la busara sana kupokea hizo 5M, karuka kiunzi vizuri sana
Walitaka waseme eti unaona ni mbaguzi.....hahaha.

Ofcourse hata matibabu yake waliochanga pesa nyingi ni wale vigogo wenye mapenzi mema na wengine hadi walipata misuko suko kwa kumtibisha Lissu
 
Aliyetoa ndege ya kumpeleka Lissu Nairobi alikuwa mwanaccm, Ssmia alikwenda Nairobi kumjulia hali hosipitali, na wengine wanaccm ni ndugu zake. Tujifunze kutofautisha chama na maisha ya mtu binafsi, mali yangu si mali ya Simba au Yanga au CCM au CUF.
Etwege, Faiza fox na Malaria watapinga hii.

Maana hawa jamaa wamejawa na roho za ajabu ajabu sana
 
Walitaka waseme eti unaona ni mbaguzi.....hahaha.

Ofcourse hata matibabu yake waliochanga pesa nyingi ni wale vigogo wenye mapenzi mema na wengine hadi walipata misuko suko kwa kumtibisha Lissu
Kuna tofauti kati ya kuchangiwa na individuals ambao hawachangi kwa lebo ya CCM na kuchangiwa kupitia harambee ya CCM mkutanoni mwao. Ni vitu viwili tofauti
 
Lissu kategwa na CCM na kapitakana kizeeeembe kwelikweli.

Kuchangiwa na CCM ni tofauti na kuchangiwa na wanaCCM mmoja mmoja!.

Poor Lissu, kaingizwa kingi kilaini. Yaani ananyang'anywa mtaji wake wa Kisiasa hivihivi.

Kama kuna mtu yupo karibu na Lissu mwambieni aache, CCM wanaenda kuitumia hiyo incidence kisiasa na itademoralize watu wenye imani naye kisiasa sana!
Mtaji wa kisiasa? Kwa nani kwa hiyo hilo na wewe limekutoa kwa Lissu likakupeleka ccm?

Wao wamechanga na wametoa mchana kweupe. Hizo ni pesa halali.

Sisi Wanachadema tunahimiza umoja na mshikamano kwa kila Mtanzania mwenye vyama na asiye na vyama.

Lissu ameonesha mfano Bora.

Lissu alihudumiwa na Mzee Mwinyi kwenye matibabu yake.

So kama Ulijua Lissu ana uadui na kila mtu sahahu.
 
Ninakubaliana nawe sehemu kubwa.
Lakini hapo hapo elewa kwamba huko CCM siyo wote ni akina .... eeerrr-eerrr-eh, nani yule polisi anaitwa yule?

Huko ndani ya CCM sasa hivi kuna mashetani kweli kweli, wasioona kitu kingine zaidi ya kumpambania 'Chura Kiziwi'; lakini pia kuna watu wanaoweza kuaminika na kuheshimika; kama huyo Nchimbi.

Hivi kwa maoni yako, hii pesa iliyo changwa ni sawa na ile ya Abdul, ambayo Lissu amekuwa akiipigia kelele? Mimi naona tofauti kubwa.

Kiukweli, milioni tano si pesa ya kudhalilishwa nayo; kama lengo ni kufanya hivyo, Tundu Lissu aachane nayo.
Huyo afande anaitwa Awadh/Hafidh, alisimamia na kuliendesha zoezi la kuwapiga viingozi wa Chadema kule Mbeya.

Hapo kwenye mchango shida yangu imeanzia kwa Msigwa, huyu mtu wote tumekuwa tukiona kazi anayoifanya tangu ajiunge CCM, ni kama vile Mbowe na Chadema ndio agenda yake kuu.

Sasa leo ametoa wazo la kuchangiwa Lissu, wazo ambalo Nchimbi amelifanyia kazi kwa vitendo, kwa tabia ya Msigwa "mdomo mdomo" naamini Lissu asubiri tu "mkate" wake toka kwa Msigwa.
 
Kuna tofauti kati ya kuchangiwa na individuals ambao hawachangi kwa lebo ya CCM na kuchangiwa kupitia harambee ya CCM mkutanoni mwao. Ni vitu viwili tofauti
Either way ni bora kupokea kuliko kukataa.

Hizo pesa hatuendi kutengenezea Gari bali kununulia gari.

Baada ya Hapo Tumuomne Dr Nchimbi aagize Serikali yake ifanye uchunguzi juu ya Tukio hilo lililopelekea kuharibika Gari yake.
 
Kuna tofauti kati ya kuchangiwa na individuals ambao hawachangi kwa lebo ya CCM na kuchangiwa kupitia harambee ya CCM mkutanoni mwao. Ni vitu viwili tofauti
Pesa yangu na hakuna anayenilazimisha kutoa utasemaje CCM imechanga, nyie ndio mnaosema mama Samia ametoa pesa kujenga mtaro!
 
Unafiq......
Ila kwa ninavyomjua Lissu mpunga kapokea na bado ataendelea kuwapiga spana kisawasawa
Wao kama wamefanya kwa unafiki Lissu hajali anachojua wametoa kwa moyo wao.

Lakini Spana zitaendelea kama wataendelea na ufisadi na kuteka watu.
 
Huyo afande anaitwa Awadh/Hafidh, alisimamia na kuliendesha zoezi la kuwapiga viingozi wa Chadema kule Mbeya.

Hapo kwenye mchango shida yangu imeanzia kwa Msigwa, huyu mtu wote tumekuwa tukiona kazi anayoifanya tangu ajiunge CCM, ni kama vile Mbowe na Chadema ndio agenda yake kuu.

Sasa leo ametoa wazo la kuchangiwa Lissu, wazo ambalo Nchimbi amelifanyia kazi kwa vitendo, kwa tabia ya Msigwa "mdomo mdomo" naamini Lissu asubiri tu "mkate" wake toka kwa Msigwa.
Yaani Msigwa hana impact yoyote huku CCM. CDM wala hawana time naye
 
Back
Top Bottom