Ndugu zangu Watanzania,
Wakati mwingine hasira zinanishika sana napoona watu wazima wanafanya vitu kama vipofu na watoto wadogo,.ni bora watu hao wangekuwa ni vipofu na wakafanya vitu katika ukipofu wao nisingeweza kuwalaumu.lakini inapotokea watu siyo vipofu wakafanya kama vipofu inaleta hasira sana ndani ya moyo.
Hivi CHADEMA wameishiwa akili kiasi hiki? Ndio mwisho wao wa kufikiri ulipofikia kwa sasa? Hivi ndugu zangu Watanzania mtu mwenye akili Timamu au chama chenye viongozi wenye akili Timamu na wanaojitambua na walio makini mnawezaje mkapanga ratiba sawa na ile ya Rais kufika na kutembelea eneo fulani?
Hivi hawa CHADEMA wanaelewa maana ya itifaki? Yaani unafahamu kuwa Rais wa nchi na Amiri jeshi mkuu atakwenda mkoani Manyara katika wilaya ya Hanang mji wa kateshi kulikotokea maafa ya watu.halafu na ninyi kwa kulishana ujinga kama chama ambao mpo humu humu nchini siku zote nanyi mnapanga ratiba hiyo hiyo kwa siku hiyohiyo,mkoa ule ule,wilaya ile ile na mji ule ule na muda ule ule? Hivi CHADEMA mna akili sawasawa kweli ninyi?
Hivi nanyi hapo mlipo mnajiona mpo sawa na Rais? Mnajuwa taratibu za kiulinzi na kiusalama kwa Rais anapotaka kutembelea eneo fulani? Mnajuwa mambo gani yanapaswa kufanyika kabla Rais hajafika eneo fulani,wakati Rais yupo njiani ,wakati Rais amefika eneo husika,wakati Rais akiendelea na shughuli katika eneo husika na kabla ya kuondoka?
Mlitaka mtoe na kuleta picha gani? Mlitaka kushindana na Rais? Mlitaka kwenda kumhujumu Rais wetu? Mlitaka kwenda kufanya vurugu? Mlitaka kwenda kujipima ubavu na Rais? Mlitaka kwenda kufanya uchochezi? Mlitaka kwenda kuleta sintofahamu? Mlitaka kwenda kugeuza eneo la majonzi kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa? Mlitaka kwenda kutega kitu? Mlitaka nini enyi CHADEMA?
Kwanini hamkupanga safari yenu siku tofauti na ya Rais wetu mpendwa? Kwani haya maafa yametokea tangia lini? Ninyi mlikuwa wapi wakati na siku zote? Mlisubiri Rais Anapokwenda ndiyo nanyi muende? Yaani kila mtu anafahamu kuwa Rais wetu alikuwa nje ya nchi katika kikao muhimu kabisa cha kutuwakilisha kama Taifa. taarifa zikatolewa mapema siku Rais atakapokwenda huko kuwapa pole wahanga na kujionea hali ya uharibu uliotokea pamoja na kuwapa pole majeruhi.halafu nanyi ambao mpo humu humu nchini mnapanga Tarehe na muda kama wa Rais?
Kwa hakika CHADEMA mmejiaibisha sana,mmetia aibu sana,mmeonyesha utoto wa hali ya juu sana,mmeonyesha namna mlivyo wajinga wa hali ya juu,mmeonyesha namna chama kilivyokosa uongozi na viongozi wenye akili,mipango,upeo, Dira,mikakati na wenye kuelewa taratibu.mmeonyesha ni chama ambacho hakijajiandaa kwa chochote na kwa lolote lile,mmeonyesha ni chama kichanga sana kisichoelewa kitu. Imedhihirisha kuwa CHADEMA haipaswi kupewa kura za ndio na kuongoza watu wenye akili Timamu.
Hii yote ni kwa kuwa chama hakina viongozi makini,wenye busara , hekima na wenye kutoa uongozi na muelekeo na njia ili wengine wafuate. Ni kwakuwa chama linaongozwa na viongozi walioishiwa mbinu na fikira hai.ni kwa kuwa chama kimebaki kinategemea matukio kama msingi wa kuendesha siasa zake.ni kwa kuwa chama kinaendeshwa pasipo kanuni wala taratibu zaidi ya kufanya ujanja ujanja tu katika kila jambo.
CHADEMA kwa sasa imejaa watu au kusanyiko la watu wasio na mipango zaidi ya mipango ya matumbo yao na familia zao.kimebaki chama kinachopiga hatua kurudi nyuma kila uchwao.kimebaki ni chama ambacho hakiwezi kuwa na mipango hata ya wiki moja mbele.ni chama kilichochoka na kufa kifikira.ndio maana kinajiendea endea tu bila utaratibu wala mpangilio wa kueleweka.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.