CHADEMA wasitisha safari kuelekea Katesh-Hanang kuwafariji wahanga wa mafuriko kutokana na vikwazo walivyowekewa
Uhuni ule ule toka kwa watu walewale,ikiwa hawajaweka wazi hivyo vikwazo huo ni utapeli ambao chadema imezoea kuufanya kwa wafuasi wake,sasa pesa za wafuasi wao waliochangia jana na juzi ziko wapi,si wazirudishe
Uliza michango ya maafa bukoba iliishia wapi
 
UBAGUZI KATIKA MAAFA YA MANYARA NI AIBU KWA TAIFA!
1701956771005.jpg

Ndugu Watanzania!

Kuna taarifa kuwa Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Manyara limemzuia Mhe. Freeman Mbowe kufika eneo la maafa likisingizia kuwa limepata maagizo ya kutoka juu. Sisi Askofu tunaamini kuwa hakuna maagizo yeyote kutoka zaidi ya hofu za wanasiasa wa Manyara. Sisi hatuamini kama Rais Samia au Waziri Mkuu Majaliwa na wao wanaweza kutoa amri hizo.

Sisi Askofu tunatoa wito kwa Waziri mwenye dhamana kutoka kueleza umma nini kimetokea hadi Jeshi la Polisi likazuia Mhe Mbowe kufika Manyara. Mbona jana alikuwepo msibani kwa Askofu Kweka? Je, kwa nini Mbowe azuiwe kuwatembelea hao wahanga wakati wengine ni wafuasi wake? Je, Jeshi la Polisi halijui kama Mbowe ni kiongozi wa kitaifa katika nchi hii? Askofu au Sheikh akitaka kutembelea Manyara atazuiwa? Je, UN wakitaka kwenda huko pia watazuiwa? Taharuki ya nini kwenye maafa?

Hivi ni taifa gani hili ambalo watu hubaguana hata katika maafa kama hayo? Je, serikali iko tayari kupokea misaada ya kutoka nje ya nchi wakati inakataa misaada kutoka kwa wananchi wake wengine kama viongozi wa upinzani?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

Dar es Salaam, 7 Desemba 2023; 9:30 alasiri
 
Lazima kuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa hasa ukizingatia kuwa rais wa nchi yuko huko. Mngefuata protocol sidhani kama serikali hii ya Samia ingewakatalia.

Mungu Awaponye wahanga wote wa mafuriko haya 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
Kwamba rais akienda mahali hakuna ruhusa watu wengine kwenda eneo hilo? Au ni mkutano wa hadhara kuwa wataingiliana? Chama kikishapoteza ushawishi hakiko tayari kuona wengine wanaokubalika kufikia wananchi.
 
Ila chadema kuna saa mnakua kama wehu vile. Mngesubiria rais amalize yake na nyie muende,kutwa kukurupuka tu
Hayo maafa ni mali ya rais? Au ni sehemu ya faraga ya rais kwamba wengine hawaruhusiwi kwenda huko? Majizi ya kura kwa kulazimisha kukubalika kazi mnayo.
 
Serikali imetoa takwimu za uwongo kuhusu idadi ya waliokufa na waliojeruhiwa.
Kabisa, na wanajua wapinzani wakienda watatoa ripoti sahihi ambayo hawako tayari iifikie jamii.
 
Kwa hiyo michango ndiyo basi tena haiendi Hanang'.

Lakini tuliambiwa siasa za kuhasimiana zimekwisha au kazileta tena Bwana wa Itikadi na uenezi?😁.
 
Rais wa nchi na wapinzani wakatembelea sehemu moja katika siku moja? Sijui mkuu ila kiprotokali nadhani haiko sawa sema tu watu wanataka ku-score political points!
Wanaenda kwenye mkutano wa kisiasa au kutembelea wahanga wa hilo janga? Nadhani mnaona ni kwa kiwango gani kuwa madarakani bila ridhaa ya umma kunaletq shida.
 
Bad Timing Mkuu, CHADEMA wameenda siku ambayo Chief Hangaya akiwa huko kuwapa pole wahanga.

SIDHANI KAMA WANGEPATA UGUMU KAMA WANGEENDA SIKU TOFAUTI NA MH. RAIS

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
..chadema sio sehemu ya serikali.

..tatizo lingekuwepo kama ziara ya Raisi na Makamu wa Raisi zinafanyika kwa wakati mmoja ktk eneo moja.

..kama wako maeneo tofauti sioni tatizo lolote.
 
Back
Top Bottom