CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Nilijua tu huu si uchaguzi ni upumbavu mtupu ndio maana sikujisumbua kujiandikisha, jitu linakimbia moshi ruangwa linakuja kumalizia hasira upinzani, huwezi kulazimisha mapendo hata siku moja, kama hupendwi hupendwi tu, haya CCM kamateni mioyo ya watatnzania kwa nguvu sasa...
 
Kosa kubwa mtakuwa mnajitoa mpaka lini fuateni utaratibu kama mlikosea form kubalini lakini jiandaeni mwaka mwingine.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Pia soma
Wajinga, wamesaidia kampeni ya kuhamasisha watu wakajiandikishe, mwishoni wanajitoa haina maana. Sisi wengine tuliliona hili mapema na tulishauri wasishiriki lkn hatukusikilizwa.
 
Ha ha ha! Bora umempa za uso , ajabu eti hawa ndio wote hakuna aliyekosea kujaza fomu za uchaguzi!!! Daah
 
Dah, uhuni hauna cha umri wala eti walau mtu kasomasoma kidogo. Hii ni aibu kubwa sana kwa nchi.

Kumbe hakuna wanaunga mkono juhudi!! Yale tunayoona waga ni maigizo tu.

Magufuli has really outlived his usefulness. He was accorded with the job that does not commensurate with his abilities and experience. He is a disgrace to the country.
 
Afadhali wametuokolea mda na gharama japo hizo gharama sijui km zitarudishwa serikalini.
Lkn gharama na hasara ya chadema kujitoa ni kubwa kwa baadae kuliko ambavyo ingeshiriki lkn hii dhana inahitaji kwa mtu mwenye jicho la mwewe ndio ajue ninamaanisha nini,
Nadhani CHADEMA kujitoa ni sahihi na itarudisha imani kwa wanachama wake, kinachofanywa na chama changu (CCM) ni uhuni uliokithiri. Nasikitika sana kuona chama na serikali wanafanya mambo ya kitoto kiasi hicho. M/kiti wangu na raisi wa nchi hapo unafeli sana na kututia aibu sisi wanaCCM
 
Kubwa kwa Demokrasia ya Tanzania sio Chadema. Hivi kwa akili za kwawaida hauoni jinsi viongozi wanavyosulubiwa? Sasa unataka waingie kwenye kampeni ili wananchi wakapigwe mabomu, vitungu, maji ya kuwashwa na kufungwa juu. Ebu fikilia tena naona jicho lako la mwewe halioni mbali. Wenzako wameangalia kwa jicho la Tai linaloona umbali wa km 8 clearly.
Afadhali wametuokolea mda na gharama japo hizo gharama sijui km zitarudishwa serikalini.
Lkn gharama na hasara ya chadema kujitoa ni kubwa kwa baadae kuliko ambavyo ingeshiriki lkn hii dhana inahitaji kwa mtu mwenye jicho la mwewe ndio ajue ninamaanisha nini,
 
Mlichofanya viongozi wangu wa chama ni kutoa taarifa kwa umma, ambao kwa % kubwa walishajitoa wenyewe kwenye uchaguzi huo.

Maana chaguzi zote zinaofanywa ni kati ya vyama vya upinzani na serekali kwa maana ya polisi na si ccm tena.

Tunaunga mkono hili kwa 1000%.
 
Back
Top Bottom