Raymanu KE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2022
- 10,644
- 20,009
Sahihi kbsa,malezi Bora ndo jambo la msingiUnaweza kupata mtoto wa kiume akawa tofauti na unavyotegemea, shoga, mwizi, tapeli, jambazi au akaangukia kwa familia ya mke wake.
WAtoto umleavyo ndivyo akuavyo mara nyingi watoto wa kike hawasahau kwao.
Fact si point of view.Wewe kuchukulia "Traditional argument" kama logical fallacy, namna yako unavyotazama mambo "point of view" na sio jambo baya ni mtazamo tuu na nauheshimu.
Swali lako kwamba "Mwanamke ndiye anayebeba mimba kwa miezi tisa takriban, utasemaje haendelezi kizazi chake cha asili?".
Nimeshakujibu, kuhusu hili huko juu, kwamba kisayansi mwanamke hana mbegu ana yai. Mbegu inatunzwa na kuzalishwa kutoka katika kiumbe cha kiume. Hii sio tamaduni ni sayansi. Kwa mantiki hiyo, mwanamke anapokea mbegu toka kwa kiumbe cha kiume, mwanamke ni mapokeo ya mbegu. Mwanaume ndiye mwenye mbegu hiyo, ndipo fact ya kuendeleza "Asili/Ukoo/familia" inapozaliwa.
Mwanamke anapewa mbegu azae mtoto, ni mchakato wa kisayansi.
Ndio maana tamaduni haiwezi ruhusu Mbegu ya Kiranga, mtoto azaliwe aitwe Dangote. Ataitwa Kiranga mwenye mbegu ile. Huyo mzaliwa kuwa na haki ya kujiita atakavyo, hakuindoi fact kwamba asili yake ni Kiranga. Usiibeze tamaduni wakati inaakisi sayansi.
Tamaduni ni matokeo ya sayansi/nature. Tamaduni inatambua jinsia ME na KE, upatikanaji wa jinsia ni sayansi/nature, tamaduni ikatambua hilo, ikatoa utaratibu na majina ya jinsia na asili ya mtu. Kwanini tamaduni ionekane haina fallacy kwenye eneo hili, wakati imeakisi sayansi?
"Mbona kama huelewi kuwa hizi ni tamaduni zlkizowekwa na watu tu na tunaweza kuzikataa kama tunaona zimepitwa na wakati?"
Tamaduni kwamba mwanamke sio mwendelezaji wa kizazi chake cha asili, haiwezi kupitwa na wakati. Tamaduni haiwezi kupitwa na wakati, tamaduni ni matokeo ya nature/sayansi. Tunaweza ikataa tamaduni kwenye baadhi ya mambo, lakini tukaikubali kwenye mambo mengine.
Tamaduni hii inaakisi sayansi inayotuambia kwamba, mwanamke ana yai, mbegu anategemea kiumbe kingine cha kiume. Hii ni fact ya kisayansi.
Kuhusu kujua mtoto ni wa nani; Njia zote za kisanyansi na kitamaduni zinatumika na zina matokeo ya uhakika. Ni suala dogo sana hilo kitamaduni.
Umamaliza vizuri sana mkuu eti utatu mtakatifu wa kiume 😅Nina watoto wa kiume tu,Tena wawili,Niko proud sana juu ya uwepo wako,sijawahi tamani mtoto wa kike,japo mama yao analalamika Kila mara kuwa anataka mtoto wa kike.
Mimi maombi yangu kwa last born wetu awe wa kiume,yaaani utatu mtakatifu wa kiume
Watanzania wengi, hususan kama mtoa mada, hawana uelewa wa msingi kabisa wa mtoto kuwa wa kiume au wa kike mzazi gani ndiye anasababisha.Mkeo hufikirii atakavyojisikia? Haswa ukiwa wewe ndio mwenye XY, hivyo hata huko nje matokeo huenda yawe haya haya.
Kama kutoka basi atoke yeye, akatafute Y.
Sasa mkuu Kiranga hata kwa akili ya kawaida tu mtoto wa kike anawezaje kuendeleza ukoo?Wazo zima kwamba mtoto wa kike haendelezi ukoo ni wazo la kibaguzi sana.
Hakuna Raha bila mtoto wa kikeWatoto wa kike hapana aiseee... Nina vidume vitatu na ni rahaa hataree
Kuliko nipate toto la hivyo Bora wawe wa kike tuu ,kwanza oitaishia kukutesa,zembe na litakufa likuache Ukiwa Mzee.Kwetu hakuna ushoga so sitalea mtoto awe shoga UKOME kuniambia hivyo. Ninachotaka niwe na mrithi. Akiwa jambazi tapeli, jambazi au mwizi ni wangu nitaenda kumuwekea dhamana na kumtoa jela.
Katika watu hatari wasipopata malezi ni Watoto wa kiume,hawanaga faida hata kidogo na hugeuka kuwa majuto Kwa mzazi tofauti na wa kike.Mzee usiseme hivo, yaache tu, Kuna kijana huku, kamuua mama yake, kwa kumchoma, kisu, Kuna kijana Arusha alikua mtukutu, wazazi wanamtetea kaja kaanza kuwapiga wote na ni wazee
Watoto wa kiume ndo huendeleza koo za Baba zao.Kuna ukoo ambao umewahi kuendelezwa bila mwanamke?
Tuanzie hapo kwanza.
sema nimeona huna sababu za maana kabisaNa declare interest. Mi ni Baba wa watoto 4 wote wa kike. Mtoto Mkubwa yupo Form 3 na mdogo yupo Class four.
Kwanza nashukuru Mungu kwa kunipa mabinti 4. Kimsingi baada ya wawili wa kwanza kuwa wa kike, nikiongea hao wengine niliamini nitapata kidume nyumbani kwangu.
Hawana changamoto yoyote na wanaendelea na masomo vizuri tu wakiwa na afya na ukuaji mzuri ila kama baba kuna muda napata mawazo kwa kukosa mtoto wa kiume. Naogopa kuongeza kwa huyu mama kwani tunaweza ambulia wa kike tena.
Kimsingi sasa natafuta niweke mbegu huko Pembeni nipate kidume na nimlete kumlea na hawa wenzake. Kuna changamoto nyingi kwa nyumba kukosa mtoto wa kiume.
Changamoto ya Kwanza ndio mrithi wa familia na atakayeendeleza Jina na damu yangu. So kukosa mtoto wa kiume hadi sasa sina mrithi wa mali yangu na atakayeendeleza jina langu.
Pili, kushindwa kufanyika kwa baadhi ya kazi nyumbani kama utunzaji wa mifugo na mbwa ninazofuga, kukosa wa kunichinjia mbuzi au kuku.
Changamoto ya tatu, kukosa wa kuniuguza uzeeni ambaye atanisaidia pia kama mwanaume mwenzake.
Changamoto ya nne kukosa mlinzi na msimamizi wa nyumba kipindi nasafiri kwani huwa nasafiri sana kikazi na kibiashara.
Kimsingi, ni ngumu sana nyumba kukosa mtoro wa kiume. Sasa natafuta mwanamke ambaye atakuwa tayari kuzaa nami na nitamfungulia na kumjengea alee mwanangu na akiwa na miaka 7, nachukua mwanangu.
Ni raha sana kuwa na jamaa anayecheza mpira hapa nyumbani na atakayeniletea kesi za kutia mimba huko nje.
Je wewe mwenye watoto wa kike tu, una changamoto zipi?
Hiyo ni wewe Mkuu. Mi nataka mrithi na mlinzi nyumbani kwangu.wengine tunaangalia idadi tuu kama watoto ni wawili basi wanatosha haijalishi wakike au wa kiume
Fact si point of view.
Logical fallacy ya argument from tradition ni a logical fact, si point of view.
Zaidi ya hapo labda useme hutaki logic kabisa, in which case uache hata kuandika na kutumia lugha kwa sababu vyote hivyo vinatumia logic.
So what mwanamme anatoa mbegu na mwanamke anatoa yai?
Kwa hiyo kama mwanamke ana yai mwanamme ndiye mwenye mbegu mwanamme anaweza kupata mtoto mwenyewe kwa hiyo mbegu yake bila yai?
Nimekueleza wa Spanish wanawapa watoto majina ya pande zote, kwa baba na mama, huelewi wapi kwamba hili ni suala la watu kupanga tu?
Hakuna sheria ya asili inayozuia mwanamke kuwa na jina au utambulisho wa upande wake, au mtoto kuwa na utambulisho wa upande wa mama.
Hizi ni habari za matokeo ya utamaduni wa kuwadogosha wanawake, ni mfumodume tu.
Ndiyo maana hata nyie mnaleta argument zinaji contradict.
Mnataka kuendeleza bloodline kwa kutafuta mtoto wa kiume hata wa ku adopt kama Dangote, ambaye hana uhusiano wa damu na baba, na kuacha mtoto wa kike ambaye ana uhusianino wa damu na baba.
This is not about bloodline.
Huu ni ubaguzi dhidi ya watoto wa kike tu.
This is about mfumodume.
Kama wanaume ni wa maana hivyo, na wanawake hawana maana hivyo, basi zaaneni wenyewe bila wanawake, tena mzae wanaume watupu, tuone dunia itakuwKwahiyo
Shukuru Mungu amekupa watoto.Swala waridhi wenye kujielewa ni majaliwa ya Mungu mwenyewe,wazazi wengi wanalizwa watoto wao wa kiume mpaka wanatia huruma.Mimi na mke wangu tumejengewa na hao unaowaita watoto wa kikeNa declare interest. Mi ni Baba wa watoto 4 wote wa kike. Mtoto Mkubwa yupo Form 3 na mdogo yupo Class four.
Kwanza nashukuru Mungu kwa kunipa mabinti 4. Kimsingi baada ya wawili wa kwanza kuwa wa kike, nikiongea hao wengine niliamini nitapata kidume nyumbani kwangu.
Hawana changamoto yoyote na wanaendelea na masomo vizuri tu wakiwa na afya na ukuaji mzuri ila kama baba kuna muda napata mawazo kwa kukosa mtoto wa kiume. Naogopa kuongeza kwa huyu mama kwani tunaweza ambulia wa kike tena.
Kimsingi sasa natafuta niweke mbegu huko Pembeni nipate kidume na nimlete kumlea na hawa wenzake. Kuna changamoto nyingi kwa nyumba kukosa mtoto wa kiume.
Changamoto ya Kwanza ndio mrithi wa familia na atakayeendeleza Jina na damu yangu. So kukosa mtoto wa kiume hadi sasa sina mrithi wa mali yangu na atakayeendeleza jina langu.
Pili, kushindwa kufanyika kwa baadhi ya kazi nyumbani kama utunzaji wa mifugo na mbwa ninazofuga, kukosa wa kunichinjia mbuzi au kuku.
Changamoto ya tatu, kukosa wa kuniuguza uzeeni ambaye atanisaidia pia kama mwanaume mwenzake.
Changamoto ya nne kukosa mlinzi na msimamizi wa nyumba kipindi nasafiri kwani huwa nasafiri sana kikazi na kibiashara.
Kimsingi, ni ngumu sana nyumba kukosa mtoro wa kiume. Sasa natafuta mwanamke ambaye atakuwa tayari kuzaa nami na nitamfungulia na kumjengea alee mwanangu na akiwa na miaka 7, nachukua mwanangu.
Ni raha sana kuwa na jamaa anayecheza mpira hapa nyumbani na atakayeniletea kesi za kutia mimba huko nje.
Je wewe mwenye watoto wa kike tu, una changamoto zipi?
Logical non sequitur fallacy.Kwahiyo mbegu za mahindi ambazo huwa tunapanda shambani. Basi tugeuze tuwe tunaita mahindi ni udongo kisa mahindi mbegu hayakujikuza yenyewe???
Kwa sababu watoto wa kiume wanajioa wenyewe kwa wenyewe wa kiume na kuendeleza hizo koo kwa kuzaa wenyewe sio?Watoto wa kiume ndo huendeleza koo za Baba zao.
Wewe hapo ulipo unaendeleza ukoo wenu
Wewe hauko serious, Samia akiondoka madarakani utabadilisha mawazo.Kuliko nipate toto la hivyo Bora wawe wa kike tuu ,kwanza oitaishia kukutesa,zembe na litakufa likuache Ukiwa Mzee.
Angalia mtaani wanaohangaika na maisha na vichaa ni WA kiume