Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Na umeamini yote aliyosema? Mbona hakusema kuwa Magufuli alifariki tangu tarehe 12? Mbona hakusema alipelekwa Nairobi na iliposhindikana ndiyo akarudishwa Mzena? Unajua ni kwa nini amesema Magufuli alikuwa anasema nirudisheni nikafie nyumbani? Ni kwa sababu alikuwa Nairobi!
Ujuaji mwingi..,
Ashindwe kupelekwa south Africa apelekwe kenya!?
 
Sidhani hili linahusisha mfumo dume. Nadhani hata ikitokea kwa rais mwanamke huenda itakuwa hivi hivi tu. Ukishakuwa rais unakuwa si property ya familia. Hata sasa bila shaka kuna maamuzi mume wa rais hawezi yafanya juu ya mkewe bali yatafanywa na vyombo vya ulinzi
Huyo ni mmoja wa genge linalotumia mianya kama hii kuvumisha na kupotosha taarifa. Kweli halina mahusiano na anajiondoa ufahamu-sawa ni kweli Mama yetu Janet hakuwepo, lakini wakati huo ulikuwa ni wakati wa Janga la corona na tahadhari zote zilikuwa zikizingatiwa.

Hawa jamaa ni karaha.
 
Binafsi siioni maajabu general Mabeyo kulia. Watu wanaleta stori za uaskari. Hivi ni wapi mwanajeshi alisomea ukakamavu wa kutolia akiumizwa au kukuguswa na jambo la kusikitisha au kufurahisha. Hapa ndo huwa tunaona watu hasa wa tz wanavyokuwa waoga kutetea haki zao mbele ya askari kwa kudhani askari huyo yeye kaumbwa tofauti na yeye au ana moyo wa chuma. Huyu ni mwanadamu km wewe isipokuwa yeye kaongezewa tu somo la ukakamavu na ujasiri kitu ambacho hata raia kibao tu wanacho hasa wakazi wa mkoa wa Mara, Wamasai nk. Nafikiri hivi karibuni tulishuhudia Wamasai Zanzibar wakiwatia bakora askari wa Zanzibar hadi kukimbia.

Askari nao wana hisia, mzuka, nk. Hakuna mbabe wa hivyo vitu. Ni sawa na kusema general hawezi kuhisi njaa, kitu ambacho siyo kweli, maana hakuna baunsa wa njaa.

Mtu hulia hata kwenye msiba usiomhusu, wakati unaomhusu anaweza kujikaza. Kwa hiyo mazingira huamua hisia za mtu atende nini. Hivyo mtu kulia sababu ya huzuni au furaha husababishwa na factors nyingi, wengine hulia kwa kuvuta kumbukumbu ya matukio ya nyuma yaliyomkuta na kumuumiza, ndo maana mwingine anaweza kulia hadharani sababu ya mapenzi na mwingine asilie. Tena mwingine akavalishwa tu pete akalia tena mbele ya umati wa watu.

So, kulia kwa general publicly is not a big deal, a big deal is why is he crying repeatedly. Alilia siku ya mazishi lakini nashangaa hadi kwenye kumbukizi.
 
Ujuaji mwingi..,
Ashindwe kupelekwa south Africa apelekwe kenya!?
Unajua umbali uliopo kati ya South Africa vs Kenya? Unajua wakati anapelekwa alikuwa kwenye hali gani? Ujuaji ni kupinga kitu ambacho hujui. Kuna siku utaujua ukweli. Alirudishwa kutoka Kenya na ndiyo maana alikuwa nasema nurudisheni nikafie nyumbani.
 
Na umeamini yote aliyosema? Mbona hakusema kuwa Magufuli alifariki tangu tarehe 12? Mbona hakusema alipelekwa Nairobi na iliposhindikana ndiyo akarudishwa Mzena? Unajua ni kwa nini amesema Magufuli alikuwa anasema nirudisheni nikafie nyumbani? Ni kwa sababu alikuwa Nairobi!
Kwa hiyo tukuamini wewe katika story yako kuliko mabeyo? Ata ya kuitwa kina pengo nayo mabeyo katunga sio? Na ujue jiwe licha ya ukorofi wake lakini alikua mtoto wa mama kweli kwa mama yake na kwa maelezo ya mabeyo alitamani kufia chato sio mikononi kwa doctor wa ushauri tule mara ngapi kwa siku
 
Unajua umbali uliopo kati ya South Africa vs Kenya? Unajua wakati anapelekwa alikuwa kwenye hali gani? Ujuaji ni kupinga kitu ambacho hujui. Kuna siku utaujua ukweli. Alirudishwa kutoka Kenya na ndiyo maana alikuwa nasema nurudisheni nikafie nyumbani.
Wewe ni tahira,
Mabeyo amesema saa ngapi alirudishwa nyumbani!?
Mabeyo amasema walikataa kumrudisha nyumbani hiyo aliyosema walimrudisha nyumbani iko wapi!?
Waweze kumpeleka nairobi washindwe kumpeleka south!?
Lissu alipelekwa nairobi kwa sababu tu za liusalama, hakuna hiyo huduma bora mpaka raisi apelekwe
 
Kwa hiyo tukuamini wewe katika story yako kuliko mabeyo? Ata ya kuitwa kina pengo nayo mabeyo katunga sio? Na ujue jiwe licha ya ukorofi wake lakini alikua mtoto wa mama kweli kwa mama yake na kwa maelezo ya mabeyo alitamani kufia chato sio mikononi kwa doctor wa ushauri tule mara ngapi kwa siku
Kwanza kabisa ondoa maneno ''kwahiyo tukuamini wewe...'' na weka ''kwa hiyo nikuamini wewe....'' Hii ni kwasababu wewe huwakilishi members wengine. Twende: uamuzi wa kumuamini nani, ni wako mwenyewe. Kama umeona Mabeho amezungumza ukweli kwa asilimia zote basi mwamini yeye. Ila jua kwamba anaweza kuwa amezungumza ukweli nusu au robo. Sikushikii mutu bunduki ila naandika nilichoambiwa na mtu wangu.
 
Kwa Tanzania, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Rais kufia madarakani.

Kwa Marekani, ni marais 8 ambao wamefia wakiwa madarakani.

Marekani wana uzoefu juu ya hilo. Tanzania tumeupata uzoefu huo miaka 3 tu iliyopita.

Tujipe nafasi ya kujifunza kuhusu matukio kama hayo.
Kumbe mtaala wa kujifunzia lazima autunge mwanafunzi mwenyewe?

Kwa nini tusijifunze kutokana na uzoefu wa wengine?

^Why isn't you seatbelt on?^

^'Cause I never had an accident.^

Halafu kule kwenye anga za CJ wanasema ^Tumetoa adhabu kali ili iwe funzo kwa...^
 
Kwanza kabisa ondoa maneno ''kwahiyo tukuamini wewe...'' na weka ''kwa hiyo nikuamini wewe....'' Hii ni kwasababu wewe huwakilishi members wengine. Twende: uamuzi wa kumuamini nani, ni wako mwenyewe. Kama umeona Mabeho amezungumza ukweli kwa asilimia zote basi mwamini yeye. Ila jua kwamba anaweza kuwa amezungumza ukweli nusu au robo. Sikushikii mutu bunduki ila naandika nilichoambiwa na mtu wangu.
Endelea kumwamini mtu wako lakini usiendelee kuaminisha ujinga wako na rafiki yako kwa watu wengine. Vinginevyo njoo na ushahidi kama wa mabeyo ambeye alikuwepo mwanzo mwisho wa tukio. Kwa hiyo interview ya cdf ni watu watatu wengine aliowataja wanaweza kua na story tofauti na yake. Akiwemo janab hao ndo kasema walikuwepo muda wote
 
Naweza kuwa mimi ndiye Mabeho nimekuja anonymously! Una ushahidi gani kuwa mimi siyo yeye? Mabeho anaweza kuwa ndiye rafiki aliyeniambia. Una ushahidi kuwa sivyo? Mabeho anaweza kuwa anasema ukweli nusu. Una ushahidi gani yote anayosema ni ukweli? Mabeho anaweza akawa hakuwepo muda wote! Mabeho anaweza kuwa anadanganya kama waziri mkuu alivyodanganya Magufuli ni mzima na anachapa kazi!
 
Kweli wewe ni tahira unajiuliza na kujijibu mwenyewe.
Umekazana mabeho mabeho,
Hata mabeyo tu kuandika huwezi.
Hizo habari zako za niamini mimi peleka kwenye vijiwe vyako vya kahawa
Ohoo sorry. Kumbe anaitwa Mabeyo? Lakini nadhani ujumbe umeupata pamoja na utaahira wangu. Alipelekwa Nairobi na walitumia uwanja wa Wilson airport. Madaktari wakajaribu lakini hawakufanikiwa, akarudishwa akiwa kwenye hali mbaya na kufia Mzena.
 
Nafuatilia Clip Mimi...Angejua hali asingeendelea na yake mpaka mwenzake anakata roho...Kama Kuna mambo ya muhimu kumkabidhi ambayo hayakuwa documented je? Kwani Katiba inasemaje? Nani anakuwa Rais kama aliyepo hawezi majukumu? Kwanini basi hakuwepo hapo wakati huyu ameshindwa majukumu?
Ndiyo maana ni vigumu sana kuamini kwamba hawakuwa wakifahamu kinachoendelea.

Halafu na vile mitandao ya kijamii ilivyokuwa imejam kwa taarifa kibao za taharuki! No way!
 
Back
Top Bottom