Dkt. Mollel: Ni ujinga Waziri kutoa Data za Walioathiriwa na Corona kila siku. Bei ya chanjo ni Tsh 400,000

Dah, maskini Tanzania
 
Mwenye CV ya Naibu Waziri wa afya Tanzania tafadhali
Huhitaji CV yake jiulize tu kwa nini waliochanjwa Ulaya na Marekani nchi zao haziwaruhusu kusafiri kwenda popote duniani kama chanjo yao iko vizuri?
 
Hawa maeokta wetu, wengine huo udokta Ni wa jina lakini hakuna uhusiano na kilichomo kichwani.
 
Zendrano!! Ni kupuuzwa kwa raia wa kawaida ndio kumetufikisha hapa. Hivi kweli maneno yanayosema kuwa ugonjwa upo na wengine haupo, hauna athari zozote kwa raia wa kawaida?? Naona raia wa kawaida hapa umeitumia kama ni mwananchi mmoja hivi asiyejitambua wala kufanya maamuzi ya msingi na maamuzi yake yanaongozwa na raia wasio kuwa wa kawaida. Hivi ukisikia kuna kipindupindu mtaani kwako, na watu kadhaa wamekufa - hudhani taarifa hiyo haisaidii?? Acheni kwanza dharau kwa raia wa kawaida, ndio hao hao mnaenda kuomba ridhaa ya uongozi kwao halafu baadae mnawaona wapumbavu na wasiojitambua, wasiowaza na kufanya maamuzi yanayoathiri maisha yao!! Mimi ni raia ninayejitambua na nipewe taarifa ili nifanye chaguo. Kila uamuzi huhitaji taarifa. Ni aibu sana kwa uliyosema - afya ya jamii ni kwa kila mtu bila kujali kama ni kiongozi au la. Wakisema kula balanced diet, hawakununulii kwa sababu jukumu la kujilisha ni lako. Nikupe mfano mtu tu, raia wa kawaida. Huo ndio ushirikiano tunaohitaji!!
 
Uwezo wako wa kufikiria ndio umeishia hapo
Mkuu, achana na watu wa kiwango hiki. Sasa nazidi kujiridhisha uwezo wa kufikiri ndio tatizo la nchi hii!! Tuna vitu vingi vya kufikirika - tunaonewa vitu, tuko katika vita vya kiuchumi, tunachanjwa tusizae, barakoa zina vidudu (huku wakihimiza tuvae zetu wenyewe - sijui kuzuia ugonjwa gani). Sasa free mason. Tumefikia hatua ya kusikitisha sana.
 
Wakuu Logic behind kutoa takwimu za wagonjwa wa Corona ni ipi??

Kwamba ukitoa ndio tiba ama nini??
 
Kutangaza data za waliougua au kufariki kwa kovid ni njia mojawapo ya kuokoa watu, maana huongeza uoga na tahadhari
 
Kibaya zaidi kufikiri huku kipumbavu kuwaongoza na mtu ambaye ndio alifaa awe dira kwa wananchi wake.mtu mwenye PHD aliyoipata kihalali sidhaji kama anaweza kuwaza kwa style yake
 
Abaki kwenye fani yake ya dentistry awaachie md specialist wa internal medicine na nyinginezo watoe mchakato wa magonjwa.
Kumbe ni daktari wa meno! Kapata mkate aendelee kuutetea. Kuna haja hiki cheo cha dkt kuandikwa tofauti kati ya Dkt- binadamu, Dkt - Meno. Dkt- Wanyama na Dkt - PhD.

Ushauri Tunaweza kuandika hivi: Dkt-b, Dkt-m, Dkt- w na Dkt- p.
 

Anajiita Field Marshal wa upande wa masuala ya Afya[emoji91][emoji91][emoji91]
 
Trqined dentist anasema data ni ujinga.

Watu wakienda kwa waganda wa kienyeji siwezi kushangaa.
 
Kulingana na yeye
Kwahio dunia nzima ni wajinga?

Ni ujinga na kukosa busara na hekima kuita wengine wajinga, kila mtu anafanya kila anachokiona ni sawa / kuita wengine wajinga sababu wanafanya tofauti na wewe ni ujinga. Kila mtu ana mbinu zake heshima kitu cha bure.
 
basi watoe takwimu za case ya corona tu si tayari wameshazichambua na kubaini ukweli wa cases za magonjwa na wagonjwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…