Endapo chadema itafutwa, unadhani wanachama wake wengi watakaokua wapweke na yatima kisiasa, watajiunga na chama gani cha siasa mbadala wa chadema?

Hakuna mwenye uwezo wa Kuifuta CHADEMA kama chama cha siasa...
uko sahihi ndugu mdau wa jf,
kwasababu hakuna raia hata moja wa Tanzania alie juu ya sheria za nchi.

Na hata,
taasisi na mamlaka zote za umma,
zimeanzishwa na kuundwa kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi,
na kwahivyo zinaweza kufutwa mara moja kwa mujibu wa sheria pia.

na kwahivyo chadema inafutika vizuri tu kwa mujibu wa sheria na hakuna mtu atafanya kitu kwenye hilo humu nchini
 
Watajiunga na upigania Katiba mpya!
 
acha porojo jikite kwenye mada gentleman na itapendeza zaidi
 
Chadema haina wanachama ina wafuasi, km wapo ni wachache sana. Ni km Simba na Yanga, wanachama kabisa hai wenye kadi na wanaolipia ni wachache ila hizo timu zina mashabiki na wapenzi wengi, ndivyo kilivyo chadema.
 
Wee jamaa unajijua jinsi ulivyo na uchizi kichwani?
Sasa nikwambie Chadema ikifutwa kwa mujibu wa uchizi wako tutakuwa kikundi cha waasi na patachimbika kweli kweli!
Unajua hata pa kuanzia? Haitafuatwa ila kitafutika chenyewe
 
Chadema haina wanachama ina wafuasi, km wapo ni wachache sana. Ni km Simba na Yanga, wanachama kabisa hai wenye kadi na wanaolipia ni wachache ila hizo timu zina mashabiki na wapenzi wengi, ndivyo kilivyo chadema.
kwasabau hiyo,
wanachama wa chadema wanaweza kufika laki2 kweli nchi nzima?
 
Kwa nini uwaze CDM kufutwa?
kwanini kisifutwe gentleman kwa mfano mpaka sasa?
Yote yanawezekana, lets wait uamuzi wa Majaji. Hiyo Itakuwa ni bog blow kwa CDM maana walishajitenga na Vyama vyote vilivyopo.
 
Kwa nini uwaze CDM kufutwa?

Yote yanawezekana, lets wait uamuzi wa Majaji. Hiyo Itakuwa ni bog blow kwa CDM maana walishajitenga na Vyama vyote vilivyopo.
nadhani kujitenga ni dalili mojawapo kwamba hicho sio tena chama cha siasa,
huenda kinafanya wajibu mwingine usio wa kisiasa, na huenda ndio maana kinakiuka sheria za vyama vya siasa kila uchwao. Nadhani huo ndio msingi wa kufutwa kwake.

sidhani kama kuna haja ya kusubiri matokeo ya uchunguzi wa tume ya jaji Lila,
huenda hilo likafanyika mapema zaidi kabla ya kuendelea kuspoil waTanzania kwa tamaduni zisizofaa
 
Very possible, analyis iko vizuri.
 
Umeanza na neno .."Kama"... If and but...
Kama tunazungumzia hali ya kudhania kwamba CHADEMA Kitafutwa, haiwezekani kusema kwa uhakika wanachama wake watajiunga na chama gani. Wangeweza kugawanyika: baadhi kuacha siasa za vyama kwa muda, baadhi kuunda au kuunga mkono muundo mpya wa kisiasa, na baadhi kuhamia vyama vingine vya upinzani.

ACT-Wazalendo (CCM B) na mshirika wa serikali huko Zenj, ni chama ambacho kingekuwa muhimu kuangalia katika mazingira hayo kwa sababu tayari ni chama cha upinzani chenye shughuli za kitaifa na nafasi kubwa hasa Zanzibar. Hata hivyo, ACT imekuwa na mkondo wake wa kisiasa; kwa mfano Julai 2026 ACT-Wazalendo Zanzibar na CCM walitia saini makubaliano ya maridhiano baada ya mkwamo wa kisiasa wa uchaguzi wa 2025. Hivyo, hilo pekee halimaanishi kwamba wanachama wa CHADEMA watahamia huko ACT kwa wingi.

Pia kuna sababu ya kutokuwa na haraka ya kudhani kwamba CHADEMA itaondoka kwenye uwanja wa siasa. Julai 2026 chama kilikuwa bado kinafanya maamuzi ya Kamati Kuu na kutangaza kuendeleza kampeni yake ya Katiba Mpya, huku Septemba viongozi wake wakiendelea kuonekana hadharani katika shughuli za kisiasa na kesi ya Tundu Lissu.
Kwa hiyo, swali muhimu zaidi ni: ikiwa CHADEMA ingefutwa, na sio kama itafutwa, maana bado, je ni chama gani kingekuwa na au kitakuwa na uwezo wa kuvutia sehemu kubwa ya wanachama wake? ACT-Wazalendo, chama kipya, au vyama vidogo vilivyopo au CCM kubwa la maadui?
 
Huyu jamaa yuko kazini hapo Lumumba, amekabidhiwa Chadema ahangaike nayo.
Hii shughuli itamtoa roho.
Yaani amekuwa ni kama AI, hakuna analo fanya la maana, siku moja watamgeuza " mind your back, kwa hisani ya Dudubaya"...
 
Gentleman,
nimeleta hoja hii jukwaani kwasabau mpaka sasa kuna asilimia zaidi ya 72% kwa chadema kufutwa kama chama cha siasa nchini, kwa mujibu wa sheria, bila hata kusubiri matokeo ya uchunguzi wa tume ya jaji Lila.

Kama taifa,
nadhani ni muhimu zaidi kulinda maadili ya watoto wetu na kuepusha uovu na athari mbalimbali, hususani za kimaadili wanazopata na kuwathiri waTanzania zinazoenezwa na chadema.

Na mimi kwasababu ni mTanzania muungwana,
ndio maana walau nimeona niwaandae kisaikolojia ili ikitokea isiwe suprise, kwasababu nimewapa na options kabisa na machaguo ya vyama mbalimbali vya siasa vya kujiunga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…