RESILIENT KATO
JF-Expert Member
- Aug 21, 2024
- 4,504
- 8,842
Mimi hawakujua hata mahafali yangu ni lini.Mimi niliwakata ndugu zangu wasije kwenye mahafali , niliwachimba mkwara .kumbe sister alikuja Dar kuchukua mizgo yake ya biashara , nashangaa napigiwa simu kwamba anakuja yuko njiani tena akitokea Temeke alipofikia .
Mnakumbuka shuka kumeshakucha. Ni muhimu wazazi kufatilia maendeleo ya watoto walau kila semester na kuhakikisha amevuka mwaka salama.habari ya wakat huu wadau? kama tittle inavyojieleza nina mjomba wangu ambae alikuwa akisoma udsm na mwaka huu ndio alitakiwa kuhitimu lakin kama familia tunashindwa kuelewa kama kweli kahitimu au anaidanganya familia, sababu aligoma kuonesha matokeo yake ya mwisho pia aligoma ndugu yoyote asiende kwenye mahafari hayo yaliyo fanyika october 15!
Wadau nilikuwa naomba mdau yoyote humu mwenye kitabu cha wahitimu udsm 2026 anisaidie kwenye website udsm sijafanikiwa kuona, ili niweze kutazama jina lake kama kweli ni miongoni mwa wahitimu!
Ila Udsm kuna course wanakula vichwa balaa, sijui siku hizi hali ikoje... Nina jamaa tulienda intake moja Udsm 2009/2010.. Tulikua tunatoka mtaa mmoja.. Yeye alikua anapiga Law, mimiMkuu,matokeo anapewa vizuri tu.tukiwa mwaka wa pili pale udsm,kuna jamaa alikua haonekani nyumbani kwao kila tukifunga chuo,jamaa story zilikua nyingi mara asingizie kuna kazi temporary kapata,so dada yake aliyekua anamsomesha akaingiwa na mashaka kama kweli jamaa anasoma chuo au kaacha,akafunga safari kutoka kigoma akaenda Dar kuhakikisha kama ndugu yake yupo chuo kweli,bahati siku hiyo anafika pale udbs mimi nikawa nashuka kwenye ngazi akawa ananiulizia huyo ndugu yake,jamaa alikua anasoma bcom banking alivyonionyesha picha yake nikawa nimemtambua lkn bahati mbaya sikuwa na majibu sahihi kama jamaa yupo chuo au hayupo sababu kwa mwaka wa pili tulikua hatushei masomo mengi na watu wa banking, so mimi nikampeleka hadi kwa secretary wa ofisi ya dean akamwelezea shida yake,baada ya kama nusu saa hivi yule secretary akaja na kitu inaitwa provision results ya jamaa akamwonyesha yule dada,ebana yule dada wa jamaa alipiga ukunga pale,kumbe mwamba alikua kaliwa kichwa toka mwaka wa kwanza.ikabidi tu dada wa watu amtafute jamaa akamchana ukweli.
Ok nkuu.Acha kabisa, mambo ya expectations. Wakuu wa shule wakuda Wanalinganisha na matokeo uliyokuja nayo kutoka O level, Yule mkuu sasa HV ana cheo hao walio chini Yake nawaonea huruma
Duuh aiseeKuna mdogo wangu pia aliwahi kufanya huu mchezo,alianza vizuri chuo,.matokeo ya mwaka wa kwanza yakawa poa...tukaamini tusimfatilie ni kwamba anajitambua,kumbe kuanzia mwaka wa pili mpka wa nne maana alikuwa anachukua bachelor ya Law,dogo hakuendelea na masomo.
Akawa anapewa ada pamoja na mahitaji mengine yote,maana hakuwa na mkopo wa loan board,.
Kazi yake ilikuwa ni kutafuna zile ada,,na ni ada kubwa kiasi maana alikuwa anasoma chuo cha private..
Tulikuja kushtuka mwaka wa mwisho,kwenda chuo tukaambiwa huyu aliishia mwaka wa kwanza..
Tuliumia sana,dogo kuulizwa akaamua kusepa almost mwaka mzima hatujui yuko wapi..akaja kurudi na kuomba msamaha...
Mama yetu ana upendo sana,sisi tulikataa kabisa asisaidiwe tena..ni kweli dogo akarudi tena chuo kusomea Education..amemaliza chuo 2023,,mpaka leo yupo anambwela mbwela,ajira hajapata na umri umeenda ana almost 31,anabaki kuomba asaidiwe mtaji.imagine alitakiwa amalize chuo 2018 akiwa na umri mdogo.
Bora angetumia hiyo pesa aliyokuwa a atumia kufungua kibanda cha nyanyaHamdanganyi mtu anajidanganya mwenyewe kama ni hivyo.....
Mwaka flani dogo alitoka kucheki matokeo yake ya form four, akarudi home analiaa vibaya sana kuwa kafeli, bi mkubwa kambembeleza pale kijana wake.
Baada ya siku kupita nikamuuliza ulipata four ya ngapi, points anazosema sio za four, kwenda kwenye shule kucheki matokeo jina halipo. Kumbe hakufanya pepa alitimliwa akiwa form two kwahiyo akawa na kazi ya kula ada kila term, anatumiwa pesa za matumizi akiwa huko mkoa wa tofauti, wakati wa likizo anatumiwa nauli, wakati wa kuondoka anafanyiwa shopping ya shule....kumbe yupo tu kitaa.
Matokeo anayaona leo, alikua anajidanganya mwenyewe
Huyo dogo...Hamdanganyi mtu anajidanganya mwenyewe kama ni hivyo.....
Mwaka flani dogo alitoka kucheki matokeo yake ya form four, akarudi home analiaa vibaya sana kuwa kafeli, bi mkubwa kambembeleza pale kijana wake.
Baada ya siku kupita nikamuuliza ulipata four ya ngapi, points anazosema sio za four, kwenda kwenye shule kucheki matokeo jina halipo. Kumbe hakufanya pepa alitimliwa akiwa form two kwahiyo akawa na kazi ya kula ada kila term, anatumiwa pesa za matumizi akiwa huko mkoa wa tofauti, wakati wa likizo anatumiwa nauli, wakati wa kuondoka anafanyiwa shopping ya shule....kumbe yupo tu kitaa.
Matokeo anayaona leo, alikua anajidanganya mwenyewe
"kuprospond"Iliwah kumtokea brother angu flan.
Situation ngumu sana hii.
Inawezekana ni kweli hajagraduate.
Na sababu inaweza ikawa labda amepata Supp na ameogopa kusema.
Au alikula ada mwaka huu wa tatu na ameamua kuprospond mwaka ili aendelee mwakani.
Au ali disco na kaogopa kusema home.
Bro yeye. Alikuwa anasoma Iringa. Na alivyofika mwaka wa 3. Alijiingiza kwa biashara ya Mbao.
Alikuwa ni Private.
Ada ilikuwa inalipwa yote mwanzon mwa Semister ya 1.
Almost 2.5 Mill.
Akaona ni mtaji afanye biashara ya mbao na ahairishe mwaka wa 3. Biashara ikabuma .
graduation hakufanya.
All in all alipambana na ndan ya miaka 2 akamaliza.
kwahiyo degree ya miaka 3. Alisoma miaka 5.
Cha muhimu gamba alipata at last.
Angefanya la maana sanaBora angetumia hiyo pesa aliyokuwa a atumia kufungua kibanda cha nyanya
SawaWazazi wake ni wazembe sana
ππππ"kuprospond"
Kama ni hivyo, mna haki kujua ukweli...mkuu, tatizo familia tumepambana sana juu yake hasa mimi uncle wake sabab mama yake alifariki alimuacha akiwa kidato cha Nne
Hata sio ishu za genz, ninae shem langu nae ni last born chuo ilikuwa ni kcmc ada per year mil 4,, bado pocket money kaka yake kampeleka achukue pharmacy,, akanogewa na starehe hela zote ni mademu na kula maisha miaka hiyo ya 2010-2012, mwishoni ndo kushtuka ili kuua hilo soo akaenda kuweka majibu ya mitihani kificho,, akadabwa akafukuzwa chuo,, taarifa zikamfikia kaka mtu akasitisha ufadhili,, yupo tu anahangaika na mtaa,, na mtaa usivyo na huruma umemchapa kweli kweli,, kuna rafiki yake alikuwa mazingira magumu alikomaa akapata vyeti saiv ye ndo anakula maisha na shem ndo yupo kajibanza kwakeGen Z hawatoacha kuwashangaza, hapo unaweza kukuta ana hadi familia na pesa za ada alikuwa anazungusha kwenye biashara Kariakoo au Sinza
Watu Wanaku push to the limit kiasi ambacho ni hatari Kwa afya.Maisha ya mateso sana hayo, wewe sio mashine
Wengi wanaofanya haya huishia pabaya mnoKama kawapiga na kitu kizito na yeye maisha yatampiga na kitu kizito ni suala la muda tu
Haifai hiyoWatu Wanaku push to the limit kiasi ambacho ni hatari Kwa afya.