Kuna watu wanahoji, kwanini Kamati Kuu Chadema imeamua kuhudhuria sherehe za Uhuru leo baada ya kususia kwa miaka kadhaa.
Kuna fununu zinasikika zikifanywa na viongozi wa dini na wazee wastaafu kuhakikisha maridhiano yanapatikana baina ya serikali na vyama vya upinzani hasa Chadema, kama ni kweli basi hatuna budi kuipongeza serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli na kamati kuu ya Chadema kwa uamuzi wake huo. Najua Chadema italaumiwa na wengi hasa wahafidhina wasiopenda mabadiliko, lkn kama imeamua kwa misingi ya kujenga umoja wa kitaifa basi tuipe ushirikiano kwa manufaa ya nchi.
Inawezekana ni udhaifu fulani Chadema imeonyesha, lkn kwa jicho jingine inawezekana pia ni ukomavu wa kisiasa na ni mwanzo mzuri kwa umoja wa kitaifa. Kwanini tuumizane kwa kugombea fito.
Nchi jirani ya Kenya kwa kipindi kirefu kumekuwa na mvutano baina ya Serikali ikiongozwa na Mhe. Uhuru Kenyata dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani Raila Odinga. Lakini baada ya uchaguzi mkuu wa 2017 tumeona juhudi kubwa za wazi za upatanishi zikiongozwa na rais Uhuru mwenyewe, kwa kiasi fulani zimeanza kuzaa matunda na nchi inasonga, ila kwa kufanya hivyo Uhuru amempoteza marafiki wake wengi akiwepo rafiki wake wa karibu Ruto.
Wasiopenda Maridhiano watabeza, wasiotaka amani hawatapenda tukio hili lifanikiwe.
Maendeleo hayana chama.