Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaenda kumpigia magoti mtu aliyemtandika risasi 38 nduguyo utadhani anaua CHATU na kama haitoshi akaendelea kumshughulikia vivyo hivyo huku akiwa hoi kitandani.
CHADEMA hakuna kitu
Fununu zilizopo ni kuwa mishale ya saa kumi jioni watakuwa na kikao Cha maridhiano kitakachoshirikisha cdm's crew, baadhi ya maaskofu, mawaziri wakuu wastaafu na aliyepo, Marais wastaafu na mkulu mwenyewe hapo ikulu ndogo jijini mwanza. Sio kikao Cha kitoto!Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani
Kwanini Mbowe analazimisha ionekane kuna ugomviMwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtaka Rais Magufuli kuleta maridhiano ya kitaifa na kwamba yeye na chama chake wamenyoosha mkono wa mapatano
Ifuatayo ni Hotuba Fupi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini Tanzania Freeman Aikael Mbowe mbele ya Watanzania katika kuadhimisha miaka 58 ya Uhuru:
Mheshimiwa Rais,
Waheshimiwa viongozi wote mlioko mahali hapa,
Waheshimiwa watanzania wenzangu!
Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, kuwepo upendo, na kuwepo mshikamano katika Taifa letu.
Nawapongeza sana watanzania kwa siku hii ya leo na ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia. Tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano.
Na Mheshimiwa Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia. Basi Mheshimiwa Rais tumia nafasi hiyo ukaliweke Taifa katika hali ya utengamano.
Nakushukuri sana. Asante sana.
_____________
Hotuba fupi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na KUB, Mh *Freeman Mbowe* katika sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika Jijini Mwanza leo 9 Disemba 2019
Uasi misituni Tz tulizika rasmi siku kama ya leo 1961 hivyo hatuwezi kuongelea tena uasi wa msituni. Hata hivyo tuliambiwa uvumilivu unakikomo baada ya uchaguzi tutaambiwa mwelekeo na hatua za kuchukua. Kwahiyo hayo maridhiano yanayoombwa sehemu isiyoombea ndiyo mwisho wa uvumilivu??Ebu tueleze wew ungekua Mbowe utafanyeje. Je aunde kikundi cha uasi mşituni. Mambo sio marais km unavyofikiria.
Whatever the case, kitu tunachotaka amani iwepo kwa wote.Hizi zingine ni mbwembwe tu dogo.
Ukweli ni kuwa kishindo cha awamu ya tano maji yake hamuwezi kuogelea kamwe.
Viva Magufuli
Unaona mbali mno !Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa Mbowe ameenda Mwanza kibwege bwege. Na sio yeye tu, yaani Heche, Mnyika, Sugu, Lema, Boniface waende Mwanza bila kuwa na jambo la maana? Sidhani
Kuna watu wanahoji, kwanini Kamati Kuu Chadema imeamua kuhudhuria sherehe za Uhuru leo baada ya kususia kwa miaka kadhaa.
Kuna fununu zinasikika zikifanywa na viongozi wa dini na wazee wastaafu kuhakikisha maridhiano yanapatikana baina ya serikali na vyama vya upinzani hasa Chadema, kama ni kweli basi hatuna budi kuipongeza serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli na kamati kuu ya Chadema kwa uamuzi wake huo. Najua Chadema italaumiwa na wengi hasa wahafidhina wasiopenda mabadiliko, lkn kama imeamua kwa misingi ya kujenga umoja wa kitaifa basi tuipe ushirikiano kwa manufaa ya nchi.
Inawezekana ni udhaifu fulani Chadema imeonyesha, lkn kwa jicho jingine inawezekana pia ni ukomavu wa kisiasa na ni mwanzo mzuri kwa umoja wa kitaifa. Kwanini tuumizane kwa kugombea fito.
Nchi jirani ya Kenya kwa kipindi kirefu kumekuwa na mvutano baina ya Serikali ikiongozwa na Mhe. Uhuru Kenyata dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani Raila Odinga. Lakini baada ya uchaguzi mkuu wa 2017 tumeona juhudi kubwa za wazi za upatanishi zikiongozwa na rais Uhuru mwenyewe, kwa kiasi fulani zimeanza kuzaa matunda na nchi inasonga, ila kwa kufanya hivyo Uhuru amempoteza marafiki wake wengi akiwepo rafiki wake wa karibu Ruto.
Wasiopenda Maridhiano watabeza, wasiotaka amani hawatapenda tukio hili lifanikiwe.
Maendeleo hayana chama.
Ok. kama ndivyo hivyo kuna ubaya gani.Viongozi wengi wa chadema wameshaambiwa na wanasheria wao kuwa kifungo kipo njiani ndio maana wanajipendekeza ili wapate huruma
USSR
Hawakuwepo sababu waligoma kutambua matokeo na kumtambua raisi! Ila leo wamemtambuaIlikuwa lazima wawepo?
una akili duni isiyoona popoteKwanini Mbowe analazimisha ionekane kuna ugomvi
CHADEMA ni nini? Kwani nayo ni serikali ndani ya serikali? Hicho chama cha watu kadhaa ndo kinajipa hadhi ya kutaka maridhiano na serikali?Kuna watu wanahoji, kwanini Kamati Kuu Chadema imeamua kuhudhuria sherehe za Uhuru leo baada ya kususia kwa miaka kadhaa.
Kuna fununu zinasikika zikifanywa na viongozi wa dini na wazee wastaafu kuhakikisha maridhiano yanapatikana baina ya serikali na vyama vya upinzani hasa Chadema, kama ni kweli basi hatuna budi kuipongeza serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli na kamati kuu ya Chadema kwa uamuzi wake huo. Najua Chadema italaumiwa na wengi hasa wahafidhina wasiopenda mabadiliko, lkn kama imeamua kwa misingi ya kujenga umoja wa kitaifa basi tuipe ushirikiano kwa manufaa ya nchi.
Inawezekana ni udhaifu fulani Chadema imeonyesha, lkn kwa jicho jingine inawezekana pia ni ukomavu wa kisiasa na ni mwanzo mzuri kwa umoja wa kitaifa. Kwanini tuumizane kwa kugombea fito.
Nchi jirani ya Kenya kwa kipindi kirefu kumekuwa na mvutano baina ya Serikali ikiongozwa na Mhe. Uhuru Kenyata dhidi ya Kiongozi Mkuu wa Upinzani Raila Odinga. Lakini baada ya uchaguzi mkuu wa 2017 tumeona juhudi kubwa za wazi za upatanishi zikiongozwa na rais Uhuru mwenyewe, kwa kiasi fulani zimeanza kuzaa matunda na nchi inasonga, ila kwa kufanya hivyo Uhuru amempoteza marafiki wake wengi akiwepo rafiki wake wa karibu Ruto.
Wasiopenda Maridhiano watabeza, wasiotaka amani hawatapenda tukio hili lifanikiwe.
Maendeleo hayana chama.
Siku ya kuapishwa rais Magufuli Chadema walisusa Zitto alihudhuria na akampongeza, leo Zitto kasusa Chadema wamehudhuria, ndiyo siasa zilivyo.Hamna maridhiano wala nini ni udhaifu tu, nampongeza Zito na chama chake kutokuhudhuria hiyo hafla na hao wahuni wanaobaka demokrasia yetu. Kwahili cdm wamechemsha.
Hii inanikumbusha walivyokaribishwa na Kikwete ikulu, wakapewa chai, baadaye wakahakikishiwa maoni yao juu ya katiba mpya yanafanyiwa kazi. Baadaye wakaonekana walikwenda kunywa chai tu!Hivi kweli baada ya miaka 4 ya Magufuli bado Mbowe anamatumaini ya kuwa na maridhiano ya kitaifa?.
Baada ya yote yaliyotokea kwenye uchaguzi 2015 na serikali za mitaa 2019 Mbowe unaomba maridhiano!!! Hivi haya maridhiano ya kitaifa yatafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kurudiwa?
Nasubiri kauli ya Mh. TLS baada ya kamati kuu ya Chadema kuhudhuria sherehe za maridhiano na alichokiomba Mbowe kwa rais!
Wabunge wa chadema na wanachama wao wasubiri matusi, kejeli na vijembe kutoka kwa wabunge wa CCM kuwa walipandishwa ndege na kula ubwabwa siku ya Uhuru.
Hii nchi ilipofika inahitaji kulazimishwa sio kufanya maridhio!!
Mbowe anaiona jela kibri kimeisha na sasa anatafuta pa kutokeaHakika namsifu sana mh Mbowe kwa kuona mbele maana hayo mabadiliko siyo lazima tuyashuhudie sisi leo hii
Ebu vaa viatu vya Mbowe. Wafuasi wa upinzan wanataka mabádiliko yaletwe na viongoz huku wao wamejifungia ndani. Mara ngapi Mbowe amehamasisha civil disobidience bara support ya wafuasi wa mabádiliko?Badala ya kulalamikiána Mbowe ungekuja na option. Mange Kimambi alipata support gán otherwise wew utakua vuvuzerá la Lumumba unafitinishaUasi misituni Tz tulizika rasmi siku kama ya leo 1961 hivyo hatuwezi kuongelea tena uasi wa msituni. Hata hivyo tuliambiwa uvumilivu unakikomo baada ya uchaguzi tutaambiwa mwelekeo na hatua za kuchukua. Kwahiyo hayo maridhiano yanayoombwa sehemu isiyoombea ndiyo mwisho wa uvumilivu??
Hata hivyo nimependa comment ya Mambo sio rahisi kama ninavyofikiri!!