Freeman Mbowe: Rais leta maridhiano ya Kitaifa, sisi CHADEMA tuko tayari
Kama alivyosema Mbowe, huo hapo ni mwanzo na mumefungua njia ya maridhiano, mkiendelea hivi ipo siku mtapata hata katiba nzuri kama yetu....


====
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amempongeza Rais John Magufuli kutokana na juhudi mbalimbali anazozifanya katika kuliongoza taifa.

Akizungumza katika maadhimisho ya sherehe za miaka 58 ya uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mbowe amesema kuna ulazima wa kuwepo maridhiano na mshikamano ili taifa lizidi kusonga mbele.

“Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya uhuru kama udhibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, upendo na mshikamano katika taifa letu, ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia ili tujenge taifa lenye upendo na mshikamano.

“Mheshimiwa rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika taifa kwani kuna wengine wanalalamika na kuumia basi utumie nafasi hii kuliweka taifa katika nafasi ya utengamano,” amesema Mbowe.

Mbali na Mbowe, viongozi wengine waliopata nafasi ya kuzungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika uwanja huo ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba ambapo amesema kuna haja ya serikali kuimarisha demokrasia hata wakati tukijiandaa kulekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

"Ninampongeza Rais (Dkt Magufuli) kwa kazi aliyofanya, lakini ninamuomba ajue ana jumuku la kujenga demokrasia katika nchi yetu, hasa tunapoelekea uchaguzi wa mwaka 2020."Amesema Lipumba
 
Mbowe anawaza siasa tu anadhani bila chadema inchi haiendi


USSR
 
Angalia hapo kwenye uzi wangu nimesema hata ushindi wake ulikuwa ni utata mtupu. Kutoka bungeni ilikuwa ni suala lingine. Usichanganye mambo. Kwa taarifa yako hata huo uendaji wa Mbowe kwenye hiyo sherehe sio kwamba naufagilia, bado namshangaa kipi kimemfanya ahudhurie kama sio kufuta madai yote halali ya uonevu?
Wapi nimezungumzia kutoka bungeni?? Nimekuambia siku ya kuapishwa hawakuwepo! Au unafikiri raisi anaapishwa bungeni?
 
Marufuku kumtambua mgonjwa wa akili si unaona anavyofyatuka?
Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.

Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.

Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
 
Mbowe no mfanyabiashara..ameshachanga karata2 zake2 vyema..sababu anatambua mh rais kazi anayofanya ya kuboresha maisha ya watanzania.

Wewe na makarai wenzio mliomo humu mtabaki mkivuvuzera wakati Dj Anakunywa supu ya sato mwanza
 
#HakunaMkateNusuHapa # TunanyooshaMTIsiyoKIVULI, Maridhiano ni hadi mtakapoamua kufanya Siasa siyo Harakati # HapaKaziTu.
 
Safi, tuanze na hivi vikesi kesi vya kisiasa tuvifutilite mbali.

Hata kuundwaji wa Serikali ya umoja wa kitaifa yawezekana come 2020, Katiba ni mali yetu na si biblia ama msahafu...it can be edited, kama kweli tuna nia ya dhati why not.

Tanzania ni mali ya watanzania wote, si mali ya chama cha siasa chochote.
 
Back
Top Bottom