MARIDHIANO NI MUHIMU SANA. ILI TAIFA LIWE NA MAFANIKIO NI LAZIMA MARIDHIANO YA DHATI YAPEWE UMUHIMU. HATA HIVYO MARIDHIANO YASIWE SABABU YA KUFUTA KESI ZA JINAI NA NYINGINE ZIMESABABISHA VIFO. KESI LAZIMA ZIENDELEE AMA SIVYO WATU WATAENDELEA KUFANYA JINAI NA BAADAYE KUDAI MARIDHIANO.
 
Kumuomba Jiwe maridhiano haimaanishi kuwa hayo maridhiano lazima uyashuhudie wewe au mimi, bali hata vizazi vijavyo vinahitaji uwanja sawa wa kufanya siasa.
Vizazi vijavyo vitakuja kushangaa tu ilikuwaje watu wakafanyiwa figisu za hatari kwny uchaguzi wa serikali za mitaa,wakapewa kesi za kutosha mahakamani,mwenzao mmoja mpk akapewa ulemavu wa kudumu na bado watu hao hao wakaenda kwny sherehe iliyoandaliwa na wababe wao na wakitoka hapo bado wataenda kwny hafla kule ikulu ndogo.

Ni maajabu kwa kweli.
 
Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.

Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.

Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Lakini yule waliyemkataa, anawatambua uwepo wao ndio maana kawapa nafasi ya kusalimia Taifa. Tuwe wakomavu tu jamani, hii ni nchi yetu sote!
 
Haijalishi
 
Ngoja niandike kabisa nikichotaka kusema kabla sijasoma comments za mamluki,"Mbowe ni kichwa acha anendelee kukiongoza chama kwa namna itakavyondeza Mungu
 
Hahahaa kamanda umenichekesha sana..kumbe upo hapo?? Niko na delegation ya diplomats nakuja maeneo hayo

Viva Magufuli, Heko watanzania
Ndiyo muwe na adabu na akili ziwarudie muwache kuropoka hovyo
 
Lini chadema walimtambua Magufuli Kama Raisi? Kuapishwa walisusa kuwa hawamtambui,bungeni alipoenda Kama Raisi walitoka kumkataa.

Watoe kwanaza tamko la kumtambua Magufuli Kama Raisi.

Wanataka maridhiano na Magufuli Kama Nani kwao ?
Hiyo haijalishi. Kenya walikuwa na mtifuano mkubwa zaidi yetu.... Lakini Leo Uhuru na Laila wanakaa Meza moja.
 
Hebu punguza jazba
 
Hakika nachukua nafasi hii kuupongeza Uongozi wa juu wa Chadema kuamua kwanza kushiriki Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika nchi yetu sote.Pili naupongeza kwa dhati Uongozi wa Chadema kutaka uwepo wa maridhiano mbele ya Watanzania zaidi ya milioni 25 walioshiriki Sherehe hizo ktk Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza.Naamini Rais Magufuli na Chama cha CCM,Marais Wastaafu,Mawaziri Wakuu wastaafu ,Marais Wastaafu wa Zanzibar na Viongozi mbalimbali wa Dini zetu wote kwa pamoja watakubaliana na mawazo ya viongozi wa Chadema ili Tanzania ya Amani na Demokrasia izaliwe upya na tupige hatua kujiletea maendeleo chini ya Rais Magufuli.
 
Matokeo ya kuhudhuria kwa Mbowe na kamati kuu yanategemea maamuza ya rais Magufuli kwa 99%.
 
Hiyo haijalishi. Kenya walikuwa na mtifuano mkubwa zaidi yetu.... Lakini Leo Uhuru na Laila wanakaa Meza moja.
Huwezi kutaka maridhiano na mtu anaye kuchukulia poa,anaye kuzidi nguvu na kila kitu na anajua hamna kitu utamfanya.

Wanaridhiana watu wanaokaribiana nguvu,kwamba usiporidhia nna uwezo wa kuzingua lkn mtu anajua hamna kitu CDM itafanya unadhani amesikiliza chochote.
 
Maridhiano wanafanya watu walio more or less kwenye level moja.
Mtu aliyeiba uchaguzi na kupata 99.9 percent huwezi kufanya naye maridhiano.
 
Mbowe atimue washauri wote, wanamptosha

Wamemshauri kususia Uchaguzi sasa wanataka maridhiano ya nini
 
Hawa CHADEMA wame kwenda Mwanza kutafuta huruma ya kufutiwa kesi na wengine kuachiwa kugombea ubunge kwa usawa mwaka 2020 bila figisu kama wakati wa uchaguzi wa mitaa.
 
Magufuli aliyepinda na anaye endelea kupindisha Katiba ya Tanzania ndiye anastahili KUNYOOSHWA…!
Umenena kweli tupu. Mimi Ni mmoja ninayemwona Rais Magufuli kama mtawala anayetumia si ushawishi kwa watu wa nchi bali mabavu kufanya anachokifanya. Na mbaya kuliko yote, amekuwa ni adui mkubwa wa demokrasia na haki za binadamu changanya na kupata uungwaji mkono wa wazee wasiojielewa kama Mwinyi na Malecela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…