Ni ngumu sana kufanya usajili wa wachezaji aina ya sawadogo na ukataka upate matokeo kama wenzako, Sisi tunaoangalia mpira na kuuelewa kiufundi tulikuwa tunajua ni ngumu sana kwa kikosi hiki cha simba kutoboa kimataifa, unapoona timu imewekeza kwenye ushirikina badala ya kufanya usajili ujue kinachofata ni majanga, Simba hii ata hapa ilipofika imejitahidi kwa aina ya wachezaji walionao, Hili nililiona tokea mechi za mwanzo dhidi ya zile timu dhaifu, Bata big bullet na De agosto , tulipokuwa tunasema simba imetinga makundi baada ya kukutana na timu dhaifu tulikuwa tunaona kwa jicho la 3 mambo mengi ya kiufundi, Kibaya zaidi kiwango walichoonyesha walipocheza na Horoya ambayo sio timu ya kutisha ni ya kawaida lakini walipata shida ata kuifunga kigoli kimoja pamoja na kupata nafasi, Na mashabiki wao uwa wanajua kushupaza shingo wakiamini wana kikosi bora kama misimu 2 iliyopita, Unapotaja kwa mkapa atoki mtu pia unaangalia kipindi kile ulikuwa na wachezaji wa aina gani na sasa hivi una wachezaji wa aina gani, Unaweza ukaroga uwanja mwezi mzima na kupigwa ukapigwa vile vile kama auna quality ys wachezaji, Niwatakie usiku mwema mashabiki wa simba kunyweni angalau castle lite moja mpate angalau usingizi leo