Full Time: UEFA Champions League Final: PSG 5-0 Inter Milan | Mei 31, 2025 - Allianz Arena Stadium

Full Time: UEFA Champions League Final: PSG 5-0 Inter Milan | Mei 31, 2025 - Allianz Arena Stadium

Inonyesha kocha wa inter hakujiandaa kucheza final.
Inter wamekosa Kila kombe waliloshiriki msimu huu, Kule Italia wamekosa ubingwa wa ligi wa seria A kutoka Kwa Napoli Kwa tofauti ya point 2 Tena mechi ya mwisho ndio iliyoamua mshindi nahisi morali ya timu ilanza kushuka kuanzia pale, hawana tofauti na Simba.
 
Inter ndiyo mabingwa. Sioni hawa PSG wanawazuia vipi wana wa Italia.
nadhani umeona mkuu. Jamaa anaitwa Luis Enrique kama unaikumbuka ile Barcelona ya MSN, Ivan Rakitic wa motooo huyu ndo alikuwa master wa kile kikosi. ni balaaaaaaa
 
Hv ktk historia ya ucl finals kuna timu ilishawai pigwa 5 mtungi?
 
Nimejifunza kwenye maisha Fanya kazi na vijana ambao wako siriasi sio tu wenye ujuzi.
Barca wanavijana wenye masihara.
Wana masihara gani?

Kufungwa na Inter ilikuwa ni matokeo tu ya mchezo kutokana na weakness ya defence ya Barca.

Pia uzoefu mdogo wa baadhi ya wachezaji kwenye michuano ilikuwa sababu.
 
Nimejifunza kwenye maisha Fanya kazi na vijana ambao wako siriasi sio tu wenye ujuzi.
Barca wanavijana wenye masihara.
shida ya Barca sio masihara, ila shida ni yule mjerumani alieaminiwa kuwa kocha. yaani team haina mfumo mwingine zaidi ya offside trap ila kuscore mabao sio shida zao that's why barca wameshinda sana bila clean sheets 5-4, 5-2, 3-2, 4-3. ila kuhusu talents pale zipo tu.
 
Mkuu Hans Flick ni mkombozi wa Barca.

Kabla ya Hans walishapita makocha wengi na wakafeli.

Akina Ernesto Valverde,Quique Setien,Ronald koeman pamoja Xavi.

Timu ikiwa imefirisika na watu wengi wameikatia tamaa akaibuka Hans kama mkombozi akibeba makombe yote ya ndani na kufika nusu fainali UCL ambayo mwaka wa mwisho kufika ni 2019.

Acha tumpe jamaa heshima yake kwa alichokifanya kwa kutumia wachezaji wengi kutoka La masia tena wakiwa hawana majina makubwa.

Kuhusu mapunguvu ya ulinzi hata yeye alikili kuhusu hilo na aliomba apate muda wa pre season kulifix

Barca imerudi kwa sapalizi sana msimu huu kwa kuangalia misimu mitano iliyopita tumpe Hans credit zake.
 
Inter Ameniangusha sana leo
Kufungwa 5 finali kunaibua maswali mengi ikiwa ni pamoja na kujiuliza timu ilifikaje hapo. Sikumbuki kuona timu inafungwa 5 kwenye final za UEFA. Ni aibu kubwa, Inzagi anapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu.
 
Mkuu Hans Flick ni mkombozi wa Barca.

Kabla ya Hans walishapita makocha wengi na wakafeli.

Akina Ernesto Valverde,Quique Setien,Ronald koeman pamoja Xavi.

Timu ikiwa imefirisika na watu wengi wameikatia tamaa akaibuka Hans kama mkombozi akibeba makombe yote ya ndani na kufika nusu fainali UCL ambayo mwaka wa mwisho kufika ni 2019.

Acha tumpe jamaa heshima yake kwa alichokifanya kwa kutumia wachezaji wengi kutoka La masia tena wakiwa hawana majina makubwa.

Kuhusu mapunguvu ya ulinzi hata yeye alikili kuhusu hilo na aliomba apate muda wa pre season kulifix

Barca imerudi kwa sapalizi sana msimu huu kwa kuangalia misimu mitano iliyopita tumpe Hans credit zake.
Barca bado, ubovu wa Madrid unasababisha tuone kama Barca imepona, ila ni ina nafuu tu.
 
Barca bado, ubovu wa Madrid unasababisha tuone kama Barca imepona, ila ni ina nafuu tu.
Ukisema bado be specific.

Sema bado kwenye defence.

Kwengine Barca hiko vizuri tu.

Barca tukiimarisha defence,madrid hata akikaa vizuri bado atapata tabu sana.
 
Inter imeaibisha soka la Italia, ni fedheha na aibu, itoshe kusema Serie A kwenye big five league ni suala la muda tu wanatoka hapo ligi Haina hadhi kabisa imejaa timu mbovu zisizo na hadhi
 
Back
Top Bottom