Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Hii sio kweli, hata hao waliopindua nao wanakua vibaraka wa wengine. Labda useme wametofautishiwa master tu ila Kwa Dunia ya Sasa ni lazma uwe eastern bloc au western bloc otherwise utapotezwa kwenye ramani.
Ni bora kubadirisha kuliko kukaa nao muda mrefu hadi wanajiona km wanamiliki hadi pumzi zetu.
Na wanapodumu kwa muda mrefu zaidi ndipo roho zao zinapozidi kuwa zakikatili zaidi kwa raia wao.
 
Tume ya uchaguzi ilikuwa tayari imeshamtangaza Ally Bongo kuwa mshindi. Watu wamechoka na demokrasia za mchongo
Kabisa mkuu, demokrasia za maigizo hizo ni upuuzi tu na matumizi mabaya ya fedha.

Upepo wa mapinduzi ya kijeshi unavuma kwa kasi mno, Ila bado hilo sio suluhisho la kudumu la matatizo yanayoikumba Africa.
 
Anafata NIGERIA [emoji1184] akijaribu tu kuongoza jeshi dhidi ya Niger [emoji1183] shughuli ya Nigeria [emoji1184] itakua Imeishia hapo

PMC wargner.......
Nigeria kama hajashtukia haya mapinduzi basi hana akili.Kuna rasilimali nyingi ambazo hawajaweza kuzitumia na huyu naye ni kibaraka wa UK mrusi hana haja nae. Jeshi lenyewe halijielewi.
 
Safi sana. Huku Tanzania kuna familia na zenyewe zinataka kujimilikisha nchi
 
Safi sana.
Nchi imechukuliwa na Wazalendo.

Bila Afrika kupitia changamoto za kuwafuta kazi Wezi na kuwakabidhi Wazalendo , maendeleo watayapata kwenye makatatasi na vikao na makongamano yanayohusomisha Wadau Wa ufisadi.


Mfano nchi kama Tanzania haiwezi kupata maendeleo bila kutumia ubabe kwenye usimamizi Wa Mali za umma.

CCM ni Chama Cha Mapinduzi kilichopinduliwa na Mafisadi.
Wazalendo wakatupwa nje.

Nchi ya Tanzania Kwa Mfano Wafanyakazi karibu wote wamepita JKT. Wote ni majasiri na watiifu endapo wataongizwa na kusimamiwa kijeshi Lakini pakitokea Kiongozi akawaongoza kilegelege wote wanageuka na kukosa nidhamu na kuanza kutegea na kuiba Mali za umma .

Ukiwakabidhi Wafanyakazi Wa Tanzania kazi ujue umewakabidhi askari mana wote wamepita JKT.

Hakuna mtumishi Wa umma aliyepita JKT Atakua mtiifu bila Amri. Askari Siku ZOTE Wana nidhamu ya woga. Hivyo serikali ikiwalegezea mawaziri,wabunge , wakurugenzi, walimu ,madaktari, wafanyakazi Wa Bandari n.k. basi ni wazi Kuwa watageuka Kuwa wategaji ,wababaishaji na watafuta maslahi Binafsi. Hawa wanasimamiwa Kwa mkono Wa chuma.

Ndio maana mashirika Binafsi yanafanya Vizuri kuliko ya umma Kwa sababu mashirika Binafsi yanaendeshwa na Wasomi ambao WENGI wao hawakuwahi kupita JKT. Ni waoga na wananidhamu halisi.

Hongera sana Kwa Nchi ambazo Wazalendo Wa kweli wameanza Kuamka na kuwafukuza Wezi Wa Mali za umma Ili kujenga Kesho ya Vizazi vya wengi.


Bila hivyo Dunia itamilikiwa na Wahalifu huku waliowengi WAKIWA wanateseka chini Yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…