Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Hii sio kweli, hata hao waliopindua nao wanakua vibaraka wa wengine. Labda useme wametofautishiwa master tu ila Kwa Dunia ya Sasa ni lazma uwe eastern bloc au western bloc otherwise utapotezwa kwenye ramani.
Ni bora kubadirisha kuliko kukaa nao muda mrefu hadi wanajiona km wanamiliki hadi pumzi zetu.
Na wanapodumu kwa muda mrefu zaidi ndipo roho zao zinapozidi kuwa zakikatili zaidi kwa raia wao.
 
Tume ya uchaguzi ilikuwa tayari imeshamtangaza Ally Bongo kuwa mshindi. Watu wamechoka na demokrasia za mchongo
Kabisa mkuu, demokrasia za maigizo hizo ni upuuzi tu na matumizi mabaya ya fedha.

Upepo wa mapinduzi ya kijeshi unavuma kwa kasi mno, Ila bado hilo sio suluhisho la kudumu la matatizo yanayoikumba Africa.
 
Anafata NIGERIA [emoji1184] akijaribu tu kuongoza jeshi dhidi ya Niger [emoji1183] shughuli ya Nigeria [emoji1184] itakua Imeishia hapo

PMC wargner.......
Nigeria kama hajashtukia haya mapinduzi basi hana akili.Kuna rasilimali nyingi ambazo hawajaweza kuzitumia na huyu naye ni kibaraka wa UK mrusi hana haja nae. Jeshi lenyewe halijielewi.
 
Kikundi cha Wanajeshi 12 kimechukua uamuzi huo ikiwa ni siku chache tangu Tume ya Uchaguzi kutangaza kuwa Rais Ali Bongo ameshinda tena Kiti cha Urais

Wanajeshi hao wametangaza kupitia Televisheni ya Taifa kuwa wanafuta matokeo yaliyoyangazwa na kuzifuta Taasisi zote za Umma pamoja na kulinda amani, kuondoa utawala usiowajibika uliochangia kuvuruga umoja katika jamii

Mapinduzi haya yatakuwa yanamaliza Utawala wa familia ya Bongo iliyotawala Nchi hiyo kwa takriban miaka 53.

==========

Jeshi la nchi hiyo limesema limechukua madaraka baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza Ali Bongo kama mshindi kwa kipindi cha tatu.


Katika tangazo hilo maafisa wa jeshi waliojitokeza kwenye televisheni ya taifa walisema wamefuta uchaguzi uliofanyika Jumamosi ambao ulizusha malalamiko na wamefunga mipaka yote ya nchi hiyo pamoja na kusimamisha utendaji wa kazi wa taasisi zote za kiserikali.

--
Television announcement came shortly after state election body announced incumbent Ali Bongo had won a third term as president.

A group of senior military officers have gone on national television in Gabon saying they have seized power because elections held over the weekend were not credible.

The officers, appearing on Gabon24 in the early hours of Wednesday morning, said they had cancelled the elections, dissolved all state institutions and closed the country’s borders.

They said they represented all security and defence forces of Gabon.

The announcement came shortly after the state election body said President Ali Bongo Ondimba had won a third term in office in Saturday’s disputed elections.

“In the name of the Gabonese people … we have decided to defend the peace by putting an end to the current regime,” the officers said.

The Gabonese Election Centre said Bongo had secured 64.27 percent of the vote compared with 30.77 percent for his main challenger Albert Ondo Ossa, after a process beset by delays.

On Saturday, the opposition camp said the election was a “fraud orchestrated by Ali Bongo and his supporters” after the internet was cut and a curfew imposed. French media outlets France 24, RFI and TV5 Monde were also banned, accused of “a lack of objectivity and balance … in connection with the current general elections”, the government said.

Bongo was the candidate for the Gabonese Democratic Party (PDG), the party founded by his father, Omar Bongo, who ruled Gabon with an iron fist from 1967 to 2009. After his death, his son, then the defence minister, took his place as president and has been in power ever since.

Tensions had been running high amid Saturday’s vote with the opposition pushing for change and an end to the Bongo family’s dominance of Gabon.

Following the military announcement, the Reuters and AFP news agencies reported the sound of gunfire in the Gabonese capital, Libreville.

Source: Gabon military officers claim power, say election lacked credibility
Safi sana. Huku Tanzania kuna familia na zenyewe zinataka kujimilikisha nchi
 
Safi sana.
Nchi imechukuliwa na Wazalendo.

Bila Afrika kupitia changamoto za kuwafuta kazi Wezi na kuwakabidhi Wazalendo , maendeleo watayapata kwenye makatatasi na vikao na makongamano yanayohusomisha Wadau Wa ufisadi.


Mfano nchi kama Tanzania haiwezi kupata maendeleo bila kutumia ubabe kwenye usimamizi Wa Mali za umma.

CCM ni Chama Cha Mapinduzi kilichopinduliwa na Mafisadi.
Wazalendo wakatupwa nje.

Nchi ya Tanzania Kwa Mfano Wafanyakazi karibu wote wamepita JKT. Wote ni majasiri na watiifu endapo wataongizwa na kusimamiwa kijeshi Lakini pakitokea Kiongozi akawaongoza kilegelege wote wanageuka na kukosa nidhamu na kuanza kutegea na kuiba Mali za umma .

Ukiwakabidhi Wafanyakazi Wa Tanzania kazi ujue umewakabidhi askari mana wote wamepita JKT.

Hakuna mtumishi Wa umma aliyepita JKT Atakua mtiifu bila Amri. Askari Siku ZOTE Wana nidhamu ya woga. Hivyo serikali ikiwalegezea mawaziri,wabunge , wakurugenzi, walimu ,madaktari, wafanyakazi Wa Bandari n.k. basi ni wazi Kuwa watageuka Kuwa wategaji ,wababaishaji na watafuta maslahi Binafsi. Hawa wanasimamiwa Kwa mkono Wa chuma.

Ndio maana mashirika Binafsi yanafanya Vizuri kuliko ya umma Kwa sababu mashirika Binafsi yanaendeshwa na Wasomi ambao WENGI wao hawakuwahi kupita JKT. Ni waoga na wananidhamu halisi.

Hongera sana Kwa Nchi ambazo Wazalendo Wa kweli wameanza Kuamka na kuwafukuza Wezi Wa Mali za umma Ili kujenga Kesho ya Vizazi vya wengi.


Bila hivyo Dunia itamilikiwa na Wahalifu huku waliowengi WAKIWA wanateseka chini Yao.
 
Back
Top Bottom