Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Ndio maana nasema mapinduzi Huwa ni mbwembwe,hakuna Cha maana utafanya Kwa hiyo wanaoshangilia ni wapumbavu maana huo mkate hawatakaa waupate isipokuwa familia za waliopindua.

Kama uko Nje ya mfumo utakuwa mpiga vigelegele tuu na ndio maana Huwa sishabikii siasa bila maslahi
 
Bora waneemeke kuliko Vita,hakuna Mtanzania anapenda huo ujinga kama wewe unapenda kufa mapema kabla ya kutuletea shida sie wengine na Watoto Wetu.
Watanzania wa 2023 sio kama wale wa 1983 mliokuwa mnawatishia nyau. Watu sasa wana exposure. Watu wana uwezo mkubwa wa kuchambua masuala ya uchumi na kimataifa. Hakuna tena wa kulishwa propaganda chafu huku nyie na watoto wenu mnajazana kula mema ya nchi. Muda utafika na wote tutaimba wimbo mmoja. It's a matter of time.
 
Swala sio exposure swala ni kusagwa Kwa chuma,Putin na genge lake wanakula Rushwa na kunemeeka huko Russia ukiletwa dogo unaswagwa.

Hivyo hivyo Kwa Korea Kaskazini nk Kwa hiyo hata Tanzania ccm ilitaka inaweza fanya hivyo maana Mwendazake alifanya mbona?

Vipi mlipata Haki awamu ya Mwendazake? Si genge la wachache walijineemesha kupora Mali za matajiri,kutosha na nyie wengine mkawa kama mumeolewa na kina Bashiru.

Upumbavu wa hivyo ndio mnaita Haki? Stupid
 
I have nothing to fear. Alikufa shujaa Patrice Lumumba akipigania wananchi wenzake. Mimi siogopi kitu wewe.
Shujaa Huwa anakufa au ni digidigi tuu huyo Lumumba? Kama huna Cha kuogopa itisha press au fanya hamasa yeyote ya kwenye mtandao inayoashiria uhaini tuone ulivyo mwamba.
 
Wazalendo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ ona haya mapumbavu,linaangushwa genge Moja kwenda.kwa genge jingine unaita Wazalendo.

Wajinga ndio mliwao,wakati kina Jiwe na genge lake wanajinufaisha na utajiri wa kutisha mlikuwa mnaambuliankuitwa Wazalendo πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Shida ya Africa hatujawahi kujiuliza kwanini hatupigi hatua mbele, ni kweli mfumo wetu wa utawala ni shida sana maana hata hili la majeshi tunayofurahia lakini tujiulize kwani haya ndio mara ya kwanza kutokea? jibu hapana. Hakuna nchi yoyote iliwahi kupinduliwa na ikaleta mageuzi ya kiuchumi ay kuboresha maisha ya watu. Najuwa kuna watu watesema nchi za Africa tunautajiri sana, yes ni kweli lakini tunarudi pale pale kwanini sisi tu hatuendelei. Tuchukulie mfano wa mafuta tu, nchi nyingi zinamafuta. Saudia, Kuwait, UAE, Qatar, Nigeria, Venezuela, Iraq, Iran, Gabon sijui Angola lakini je maisha ya wananchi hizi wanafanana? Hapana nchi zote ukiondoa Saudia, UAE, Kuwait na Qatar wananchi wao wanaishi vizuri na wanazidi kuendelea, kwanini hawa wengine wamebaki na matatizo tu? jibu rahisi watawala, wenzetu wana watawala wanaojali maendeleo ya watu wao na nchi sio utajiri wa rasilimali tu, haitoshi. Na hili la Gabon nakuhakikishia hakuna lolote jipya watafurahia tu siku chache tutarudi kulekule.
 
Hauijui Libya ya Gadafi wewe
 
Shujaa Huwa anakufa au ni digidigi tuu huyo Lumumba? Kama huna Cha kuogopa itisha press au fanya hamasa yeyote ya kwenye mtandao inayoashiria uhaini tuone ulivyo mwamba.
Mimi ni mwamba kweli kweli. Mtaishia kuwatisha hao hao wasiojielewa.

Waulize vijana wa chama chenu waliotishia kuniteka eti kisa nimekosoa sera za mwenyekiti wa chama chenu.
 
Nathani kutakuwa na mafunzo maalumu, kama mtu anavyosoma bachelor ya education n.k
 
Hauijui Libya ya Gadafi wewe
Najuwa sana kuhusu Libya na kwa ufupi Libya wana reserve kubwa ya Oil lakini usitake kufananisha maendeleo ya Gulf states na Libya. Libya wana poor infrastructure na tunaona Libya ya leo.
 
1. Gabon ina watu milioni 2
2. Gabon yazalisha magaloni 181000 ya mafuta machafu (crude oil) kwa siku.

3. Gabon ni mwanachama wa nchi zinozalisha mafuta kwa wingi duniani OPEC.

4. Wananchi wake walio wengi ni maskini wa kutupwa.

5. Watu wenye umri wa miaka kati ya 15-24 hawana ajira (kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia)

6. Raisi wa kwanza Omar Bongo alichukua madaraka ya uraisi akiwa na umri wa miaka 31 mwaka 1967 Gabon ilipotwaa uhuru wake wa bendera kutoka kwa Ufaransa.

7. Tangu mwaka 1967 Omar Bongo alikuwa raisi wa nchi hiyo hadi alipofariki mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 73 na mwanae Ali Bongo kutwaa kiti cha enzi.

8. Imeelezwa kuwa familia ya Bongo ina nyumba 33 nchini Ufaransa ambazo zote zimenunuliwa kwa fedha taslimu.

9. Kuna wanajeshi wapatao 400 wa Ufaransa mjini Libreville, idadi ilopunguzwa kutoka 1000 mwaka 2009 baada ya Ali kuchukua madaraka kwani baba yake alikuwa akilindwa na wanajeshi hao ambao pia wapo Gabon kulinda maslahi ya Ufaransa.

Mapinduzi haya ya nchi za Afrika ya kati na magharibi hivi sasa yameitikisa Ufaransa na pia yamezistua nchi nyingi za Jumuiya ya Ulaya.

Mapinduzi ya Gabon yaweza kusemwa ni mapinduzi yalotegemewa kwa kuzingatia kuwa wananchi wameyakubali kutokana na namna familia ya raisi Bongo inavyotumia vibaya rasilimali za nchi hiyo kwa miaka 56 ambayo wananchi wake walipaswa kuwa na uwezo wa kufaidi matunda ya rasilimali hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…