Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

We ni takataka
 
Tanzania sio Nchi ya wajinga kama huyo ukiyemtaja,ndio maana hayupo asingekubaliwa kuleta upuuzi wake
Watu wajinga kama nyie hamuwezi kuzuia mabadiliko.Jpm Alijaribu na lakini mabadiliko yataendelea.hamuwezi kuendesha nchi kama ni ya familia zenu kama yanayofanyika hapa Tanzania kuingia mikataba mibovu ili Watu wachache wafaidishe familia zao.jiandae mabadiliko yanakuja hata hapa Tanzania.watu wa ovyo kama nyie mtahama nchi.
 
Vifaru vilitiwa mitaani Visiwa fulani.
 
Habari hii imeandikwa na Martin Maranja Masese kupitia akaunti yake ya twitter:

Inasomeka hivi:

Rais wa Gabon aliyepinduliwa na jeshi la Gabon leo, Ali Bongo Ondimba na kuwekwa kizuizini, Disemba 2021 aliagiza theluji (snow) kutoka Ulaya, ikasambazwa katika kasri la Ikulu, Libreville ili familia yake ipate mandhari ya “Christmas when it snows”

Rais aliyepinduliwa Ali Bongo Ondimba alitaka Krismasi yenye theluji (snowy Christmas) Gabon kwa ajili yake na familia yake, hivyo aliingiza theluji ambayo iliwekwa mahali ambapo familia yake ilisherehekea sherehe yao ya Krismasi, Libreville.

Rais Ali Bongo alikosolewa vikali kwa kitendo hiki cha kifahari; kwa sababu katika hali halisi, wastani wa 40% ya raia wa Gabon hawana ajira, wakati karibu 60-70% ya wakazi wa Gabon wanaishi chini ya mstari wa umaskini wa chini ya US$1 kwa siku.

Gabon imejaliwa kuwa na utajiri wa maliasili, ikiwa ni pamoja na miti mikubwa kwa ajili ya mbao, madini ya manganese, gesi asilia, na mafuta ghafi. Katika miaka 22 tangu 2000, mafuta yalichangia, kwa wastani, 50% ya Pato la Taifa, 60% ya mapato yote ya serikali, na 80% ya risiti zote za mauzo ya nje.

Misitu inachukua 85% ya ardhi ya Gabon, na kuifanya kuwa eneo la pili la misitu kwa ukubwa barani Afrika. Gabon inachukua karibu 25% ya biashara ya kimataifa ya manganese. Akiba ya gesi asilia iliyothibitishwa ilikadiriwa kuwa takriban mita za ujazo bilioni 33 mnamo 2008.

Huku akiba ya mafuta ikikadiriwa mwaka 2011 kuwa mapipa bilioni 3.7, ikiwa ni hifadhi ya saba kwa ukubwa barani Afrika, wakazi wa Gabon wapatao milioni 2.3, theluthi moja yao wakiishi katika umaskini mkubwa. Ndiyo sababu Jeshi limeamua kumpindua Ali Bongo Ondimba.

Pamoja na kwamba Gabon ni nchi inayochimba na kuuza mafuta yake hadi kuwa mwanachama wa OPEC lakini leo raia wa Gabon wananua lita 1 ya petroli kwa US$1.004 (sawa na Tsh. 2,515.02). Bei sawa na ambayo KIPARA alikuwa anauza Tanzania mwezi Julai, 2023.

Ali Bongo Ondimba anaonekana alipenda kuagiza sana vitu vyake kutoka Ulaya. Mke wa
@PresidentABO ni raia wa France amezaliwa Paris. Ni mtoto wa Édouard Valentin, CEO of the Omnium gabonais d’assurances et de réassurances (OGAR)
 
Nakazia,Africa hamna demokrasia, uhuni tu
 
Viongozi uliowataja wakae mguu pande[emoji4]
 
Afrika magharibi wanajitambua.hapakwetu waom(mboga mboga FC) wameongoza sasa yakaribia miaka 70 bilabila jeshi Lina Shangaan tuu.🤣🤣🤣🤣🪑
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…