Kwanza nianze na Intro, kumbe nimegundua katika nchi kitengo muhimu kabisa na chenye nguvu ni Jeshi linaloongozwa na CDF, sababu kubwa zikiwa ni Mbili anaweza kuamuru majeshi, lakini pia Ana silaha nzito na za kutosha kuliko jeshi lingine kama Polisi na Magereza.
Sasa haya mambo ya Wizi wa kura yamewatokea puani watawala nchini Gabon , baada ya CDF ambaye ni mteule wa Raisi kutangaza Kuchukua nchi baada ya Wizi mkubwa wa Kura. Nchi nyingi za Kaskazini mwa Africa zimeanza mtindo huo ambao Kwa nchi za SADC yaani kusini bado uwizi wa kura unatokea na jeshi halifanyi chochote. Lakini Kila jambo Lina mwisho.