Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Gabon: Jeshi limechukua madaraka baada ya Ali Bongo kutangazwa mshindi wa Urais

Mkuu acha kabisa usiombee mapinduzi ya kijeshi yatokee huku kwetu yaani ni kitu kibaya kabisa, hakuna cha rule of law kwenye nchi yenye mapinduzi ya kijeshi na hujui kesho yako itakuwaje. Ni bora tuendelee kurekebishana hivi hivi kwa kutumia majadiliano. Kwa kweli Mungu apishie mbali!
Huwezi kuirekebisha mijitu iliyojaa viburi na imeshasema kuwa imeamua kukaa kimya yaani kutupuuza.
Kila mabadiriko yana maumivu yake. Acha kuogopa. Ni kwaajili ya mema ya vizazi vijavyo.
 
Kuna baadhi ga vizazi inabidi vifutike kwanza Ili Taifa X lipone

Vijana wa mchonga wapotee.

Baby boomers wengi wapotee.

Taifa X litaokolewa na generation alpha, x na kuendelea.

Taifa X linahitaji vijana jeuri kuanzia jeshini hadi jikoni
 
Huko ni kutesa raia na kuharibu nchi....hakuna keki hapo.
Wanawatesa Vipi Raia.
Yaani kudhibiti Wezi Wa kura ,wezi Wa rasilimali za nchi. Mgawanyo mbaya Wa keki ya Taifa, ukabila, Udini, Matumizi mabaya ya Mali za umma. Madeni makubwa yanayoishia mifukoni mwa watawala. Kutumikisha Watoto Wa maskini Jeshini Kwa mishahara midogo.

Wanaotawala kiraia huku wakiwa wanatumia Majeshi kuwaumiza wananchi na Hata kuwaua na kuwafunga hovyo ni mbaya kuliko Kutawaliwa kijeshi kamili.

Nchi za Afrika ndizo nchi zinazowatumikisha Wanajeshi wake Kwa maslahi Duni wakati huo huo watawala raia wakiwa wanaishi maisha ya starehe na kufuru kubwa na kuhamishia Mali za umma ughaibuni.

Akitokea Mwanajeshi au Kiongozi raia anayeingoza kijeshi ni rahisi sana kujenga umoja, uwajibikaji,utii, Uzalendo na kuimarisha usalama Wa nchi.

Utawala Wa kiraia unatumia fursa ya Demokrasia na Majeshi yanayowalinda , kuiba Mali za umma.
 
Hata hao wanajeshi hukataa kutoka madarakani mfano ni huko Sudan, Mali.
 
Madaraka matamu nyie,
Madaraka yanalevya,
Madaraka ni uraibu,
Madaraka ni nguvu,
Unaamua watu waishi vipi na kwa mfumo gani,
Madaraka yanaheshimisha,
Madaraka ni pesa,
Madaraka ni raha kama unafika kileleni,
Ukiyashika hutotaka kuyaachia.

Daa....! Afrika tunasafari ndefu sana.
 
Kuna siku nilikuwa nina shida kwenye kambi ya jeshi, Kizumbi Shinyanga. Nilikodi pikipiki, kunipeleka huko, kutoka mjini. Hiyo pikipiki, ilikuwa imebandikwa kibao cha CHADEMA, "M4C".
Sasa tumefika getini ninajieleza kwa mlinzi, akatokea mkuu wa kambi. Alivyoiona ile pikipiki, acha agombe. Eti, CHADEMA wamefuata nini hapo? Almanusra atufukuze.
Nilipoonana na mwenyeji wangu, akaniambia jamaa ni kada wa CCM wale LIALIA! Sasa, mabadiliko kupitia hawa, tusahau!
Kumbe hii ndo ID yako??
 
Naona Mabeberu wanazidi kuminywa kila kona[emoji23][emoji23]
Kwani hata hao wanaoingia mbele ya mabeberu wana jipya gani?huyo mbambe wa Niger tayari ameshaanza kuwa mpole baada ya kuomba kipindi cha mpito cha miaka 3!!kukataliwa na ECOWAS!!mikataba yote ya rasilimali za nchi walishagawa,sasa hata ukiingia sio suala la muda mfupi kuirekebisha!!Nao wanavuna tu kipindi cha mpito kikiisha wanawaachia wengine.
 
In the name of the Gabonese people … we have decided to defend the peace by putting an end to the current regime,” the officers said.
"In the name of the mtaani people...we have decided to defend our bodies and viwalos by putting an end to the current people wearing our Magwandas" the officer said
Shaabash!
 
Yule mzee anavyoumwa bado anataka madaraka?
Ujue hawezi kutembea yule jamaa bila fimbo. Tangu nilipoona anazuia jaribio mwaka 2019 akiwa anatibiwa Saudi Arabia nikajua huyu hakai sana.
Jaribio la 2019 liliandaliwa na wasiojipanga wenye vyeo vidogo na wachache. Hili wamejipanga wengi, wamekubaliana na hawana mgawanyiko hivyo angalau nina imani nao kuliko mapinduzi mengine yote yaliyotokea kwenye 2020s.
 
Back
Top Bottom