Haji Manara popote ulipo au ukisaidiwa na Yanga SC Wenzako mkinijibu haya Maswali yangu Muhimu nitashukuru

Haji Manara popote ulipo au ukisaidiwa na Yanga SC Wenzako mkinijibu haya Maswali yangu Muhimu nitashukuru

Amani gani ivunjike kwa huyo mpuuzi mmoja anayeendekezwa tu.
Akae na hiyo ban akimaliza kama hajatafuta deal zingine wamwongeze mpk tumsahau.
Soka ziima la Tanzania haliwezi kuendeshwa na kiroboto mmoja,
Hana elimu,exposure,hajui lolote zaidi yakuongea uchafu na lile domo chafuu.
 
Naiomba serikali, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana, nimedhulimiwa, naiomba Serikali ione nini chakufanya ili kuweka haki kwenye mpira” Manara.

Nami GENTAMYCINE namuuliza Haji Manara je, na Yeye Watu Aliowatukana, Wadhalilisha na Kuwaonea kama akina Shaffih Dauda, Prisca Kishamba, Barbara Gonzalez, Mo Dewji na Jemedari Said na wengineo Wengi tu nao wakashitaki wapi?

Nanyi Serikali endeleeni tu Kumchekea na Kumdekeza Haji Manara ila hii SUMU Kubwa anayoipandikiza kwa Watu Wawili wa Simba na Yanga wanaowakilisha sehemu Kubwa ya Jamii ya Kitanzania Siku si nyingi utakuja Kuzaa Matunda Mabaya Kijamii, Kisiasa na hata Kiusalama kama siyo Kiustawi.

Na huenda hata Haji Manara ameshagundua kuwa Serikali ya sasa ni Ndombolo ya Solo tupu ( nikimaanisha ni ya Mchezo na ipo ipo tu ) ndiyo maana anapata hadi Jeuri ya Kuitajataja na Kuiamrisha kila mara kwa namna atakavyo na apendavyo.

Hivi zingekuwa ni Serikali za Watu serious na wasiohitaji Upumbavu, Upuuzi na Uswahili za akina Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Mkapa na Hayati Rais Dk. Magufuli huyu Haji Manara angekuwa na hizi 'guts' zote alizonazo katika Awamu hii ya Mwana Mama Rais Samia Suluhu Hassan?

Kazi yangu JF ni Kutoa tu Maangalizo.
Hapa alipofikia Haji ni hatari kwa usalama wa Taifa,uchochezi anaofanya na kwa vile idadi kubwa ya wanayanga ni hamnazo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani. Anafikia kumtolea kejeli waziri Mchengerwa kwa vile ni mndengereko mwenzake anataka ampe upendeleo. Huyu afinywe korodani kwanza kisha afichwe store. Naona Mzee Sunday Manara amempa malezi mabaya huyu albino wake.
 
" Wenye Akili Yanga SC nzima ni Watu Wawili tu Rais Mstaafu Kikwete na Baba yangu Mzazi Mzee Manara waliobakia wote hawana," alisema Haji Manara alipokuwa akihojiwa na EFM Radio Kipindi cha Sports Headquarters mwaka 2021.

Baada ya Nukuu ( Kumbukizi ) hii sasa Maswali Kuntu ya GENTAMYCINE yanaanza.

1. Haji Manara hivi ni Wewe ndiyo umetengeneza Brand yako kama unavyojitapa Kutwa au ni Simba SC na sasa Yanga SC uliko ndiyo zimekutengenezea Brand yako kutokana na Ukubwa wa Vilabu hivi Viwili na Ushawishi wao nchini?

2. Haji Manara hivi ungekuwa ni Msemaji wa Ihefu FC au Gwambina FC una uhakika ungejulikana na ungekuwa Maarufu mpaka kuwa na hiyo Brand yako Kubwa inayokudanganya mpaka Unadharau Watu na kujiona uko juu ya Mpira wa Tanzania?

3. Haji Manara kama umesema jana kuwa unajua Siri nyingi za TFF (hasa Maadui zako Rais Karia na Katibu wa TFF Kidau ) je, kwanini hukuzitoa (hukujilipua nazo) Siku nyingi ili utusaidie Wadau wa Mpira kujua tusiyoyajua na badala yake Umeyatoa jana kwa Mtindo wa Kukomoa, Propaganda na Kulipiza Kisasi?

4. Haji Manara je, TFF (Unayoichukia zaidi) ingekuwa inakuonea ingekufungulia ilipoingia Madarakani baada ya Kufungiwa na aliyekuwa Rais wa TFF (Mwana Yanga SC) Jamal Malinzi?

5. Haji Manara bila Busara na Nguvu Kubwa ya TFF Kukulinda unadhani kwa Kosa lile Kubwa na la Jinai ulilomfanyia Mtangazaji wa Kike wa Michezo wa Clouds FM Prisca Kishamba na ile Kauli yako ya HATARI Kiusalama, Kimichezo na Kiutalii uliyoitoa dhidi ya Timu Ngeni zilizokuwa zikija Kucheza na Simba SC ( katika CAFCL na CAFCC ) kuwa wawe Makini kwani Simba SC inatumia Sumu na hata Kuua una uhakika kuwa leo hii usingefungiwa Maisha katika Medani za Soka na pengine hata Kufungiwa na Serikali?

6. Haji Manara aliyekushtaki hadi Kufungwa Kwako huko ni Uliyegombana nae Arusha Rais wa TFF Wallace Karia au ni Sekretarieti ya TFF? Je, ule Msamaha wako wa Kinafiki ulitakiwa uutoe wa Sekretarieti ya TFF au kwa Rais wa TFF Wallace Karia tena Nyumbani Kwake?

7. Haji Manara je, unajua kuwa kwa Kitendo chako cha Jana tu kusema (tena Kijeuri kabisa) kuwa Wewe bado ni Msemaji na Mhamasishaji wa Yanga SC wakati tayari Unatumikia Adhabu Kisheria kinaweza kukufanya Uongezewe Adhabu yako zaidi na sasa ikawa Kali kuliko hiyo Ndogo tu uliyopewa?

8. Haji Manara ni kwanini Matatizo yako Binafsi yakipelekea Wewe Kuadhibiwa na Mamlaka huwa unapenda Kuihusisha Klabu ya Yanga ili upate Huruma na Sapoti yao?

9. Haji Manara je, Maudhui yako ya Jana ( pamoja na Matusi, Dhihaka na Kashfa ) katika ile Press ya Jana yalikuwa ni yako Binafsi au yana Baraka za Yanga SC kwa 100%?

10. Haji Manara je, una uhakika una Washauri wazuri na kwamba Watu wengi Wanaokuzunguka Wanakupenda na Wanakutakia Kheri kama Unavyojidanganya na Kujimwambafai Kutwa?

11. Haji Manara je, ikitokea Rais wa TFF Wallace Karia akiamua Kukushtaki 'Kijinai' kama tulivyohakikishiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya TFF iliyokuhukumu kuwa Ulimtishia Maisha Rais wa TFF Karia huku ukimwambia kuwa ATAKUKOMA na UTAMUONYESHA utaendelea kuwa Salama?

Wachezaji wa Kucheza Mpira ni Kumi na Moja ( 11 ) na Mimi GENTAMYCINE nimekuuliza haya Maswali yangu Kumi na Moja ( 11 ) na nasubiria sasa Majibu yangu kutoka Kwako Haji Manara na wana Yanga SC Wenzako wote hapa JamiiForums ili nijue kama mna Akili au hamna Kabisa kama inavyojulikana tokea Uhuru wa Taifa hili la Tanzania.
 

Attachments

  • 20220726_140633.jpg
    20220726_140633.jpg
    35.8 KB · Views: 5
1. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

2. Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba

3. Waziri 'yupo yupo' Mzee George Huruma Mkuchika

4. Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde

5. Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete

6. Waziri wa TAMISEMI Bashungwa

7. Rtd. CDF Gen. Mabeyo

GENTAMYCINE nalisema hili mapema hivi na kwa nia njema tu kwani tayari kama Kawaida na Maono niliyobarikiwa nayo na Mwenyezi Mungu naona kuna HATARI Kubwa inakuja mbeleni kama Watajwa hawa hawatokaa pembeni ya hizi Jeuri zote za Mfungwa na Mdaiwa Haji Manara.

Msije kulaumu tu sikuwashauri sawa?

[emoji14][emoji1787][emoji1787][emoji12]
 
Alohojiwa na salama kwenye salama na..ndo akasema hivyo japo najua aliongea kiutani tuuu..
 
Back
Top Bottom