“Naiomba serikali, nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana, nimedhulimiwa, naiomba Serikali ione nini chakufanya ili kuweka haki kwenye mpira” Manara.
Nami GENTAMYCINE namuuliza Haji Manara je, na Yeye Watu Aliowatukana, Wadhalilisha na Kuwaonea kama akina Shaffih Dauda, Prisca Kishamba, Barbara Gonzalez, Mo Dewji na Jemedari Said na wengineo Wengi tu nao wakashitaki wapi?
Nanyi Serikali endeleeni tu Kumchekea na Kumdekeza Haji Manara ila hii SUMU Kubwa anayoipandikiza kwa Watu Wawili wa Simba na Yanga wanaowakilisha sehemu Kubwa ya Jamii ya Kitanzania Siku si nyingi utakuja Kuzaa Matunda Mabaya Kijamii, Kisiasa na hata Kiusalama kama siyo Kiustawi.
Na huenda hata Haji Manara ameshagundua kuwa Serikali ya sasa ni Ndombolo ya Solo tupu ( nikimaanisha ni ya Mchezo na ipo ipo tu ) ndiyo maana anapata hadi Jeuri ya Kuitajataja na Kuiamrisha kila mara kwa namna atakavyo na apendavyo.
Hivi zingekuwa ni Serikali za Watu serious na wasiohitaji Upumbavu, Upuuzi na Uswahili za akina Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Hayati Mkapa na Hayati Rais Dk. Magufuli huyu Haji Manara angekuwa na hizi 'guts' zote alizonazo katika Awamu hii ya Mwana Mama Rais Samia Suluhu Hassan?
Kazi yangu JF ni Kutoa tu Maangalizo.