Manara keshaondoka, na hafanyi na hatafanya kazi tena Simba
 

Kapige nae picha kariakoo uyu nyumbu mwenzako
 
Ningewashangaa sana Simba kumwacha Manara yaani msemaji wa klabu timu inakabidhiwa kombe badala ya kuongelea klabu yake anafanya promo Azam media kama anataka kufanya promo ya azam media kwanini asifanye wakati tofauti na matukio ya Simba. Arudi kwenye timu ya baba yake huku tumemchoka kuna kipindi alitukana hadi mashabiki wa Simba ikabidi Mo ndiye awe anaongea na waandishi wa habari baada ya washabiki kutaka kuzira kuingia kwenye mechi ya za Simba.
 
Reactions: mmh
Kwa hali ilivyo ni Manara ila kuna siku baadae huyo binti lazima atafuata
 
Asante sana, wengi wanajadili hii ishu kwa chuki tu ila Manara yuko sahihi.

Nyongeza,kama mo hatoi pesa ndefu unategemea atangaziwe matangazo yake? Uache 10ml ukachukue 700k!!!? Hata kichaa hawezi kuacha hiyo pesa.

Manara ni mfanyakazi wa Simba lakini sio mfanyakazi wa Mo kampuni,msichanganye hapo.
Tumia japo chembe ya akili,Manara kaajiriwa na Simba au na Mwamedi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha iendelee kunyesha ili tujue panapovuja
 
Kwanini asiondoke Simba aende kwa huyo anayempa hizo pesa. Hapo ndipo panamashaka sana. Aende akawe msemaji wa bakhresa au wa GSM apige mpunga, Kuna mtu atakaye msumbua?

Lakini utumie akili yako vizuri pia, kama GSM na bakhresa wanampa mshahara Mara 15 ya anaopewa Simba, kwanini analazimisha kubaki Simba kwa mshahara wa laki 7 ???????[emoji847]
 
Reactions: mmh
unaweza kutuwekea mishahara ya wasemaji wa yanga ili tuilinganishe na kujua kama ananyonywa, unapoajiriwa lazima ufate masharti ya mwajiri kama unaona huwezi kufata masharti ni bora ujiajiri.
 
Mkuu basi utakuwa hujui how business works, kwa hayo makampuni wanayomtumia Hajji kama Balozi wao, target yao kubwa ni loyal followers wa Hajji ambao wengi ni mashabiki wa Simba. Haji akisema aiponde Simba atakuwa kwe hatari ya si tu ya kupoteza followers wengi kwa page zake za social media, bali atakuwa amepoteza credibility kwa kiasi kikubwa sana. Credibility atapoteza kwanza kwa wapenzi wa Simba lakini pia kwa hao wadhamini wake, sababu wataona anakosa maadili ya kazi, wakiamini hata wao siku wakikorofishana kdg ( kitu ambacho ni kawaida ktk maisha) atawaanika hadharani na kuepelekea brand zao kuchafuka. Hivyo basi kwenye hili Haji ana ya kujitafakari kwa upande wa Simba na upande wa hao wadhamini wake. Mimi ningekuwa Haji nisingeendelea tena na huu mvutano, ningeresign kisha nikapiga mishe zangu zingine, kwasababu kuendelea na huu mvutano kunamuharibia zaidi Haji kuliko Barbara na Simba, na siku hizi mbili baada ya hili saga, nafikiri amejua kuwa watu (washabiki, wanachama na wapenzi wa simba) wanaipenda zaidi Simba kuliko Haji wala Barbara.

Hao wadhamini wake haswa GSM wanafurahi tu kwa sasa anapo iponda au kuichafua Simba kwasababu wanapata kick kwa biashara zao, lakini pindi atakapokuwa ignored na washabiki wa Simba na kuacha kazi Simba, Haji kama Haji hatikuwa tena na deal, hata kama atapata endorsement hazitokuwa na manufaa makubwa kama alivyokuwa Simba. Mwisho wa siku Simba ni kubwa kuliko mtu yeyote yule.
Ila akiondoka Simba mjiandae kuoga shombo lake. Huyu jamaa kwa shombo hafai.
 
halafu jana ulitoa post ya kushutumu Manara kulipwa laki saba lakini uliposikia kuwa simba walimpa mkataba wa milioni 4 umekuja na tamko jingine wewe na haji Manara tabia zenu zinafanana.
 
Kuna tofauti kati ya mdhamini na muajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…