Hans Pope: Manara hataki kusaini mkataba ambao atalipwa milioni 4
Kama ilivyo kawaida ya JF kuweka rekodi sawa. Tarehe 22.07.2021 Haji Manara amedai huku akilia kama mtoto mdogo huku akitokwa hadi mafua kuwa kati yake na Barbara basi Barbara ataondoka na kumuacha yeye Smba.

Manara kadai kuwe iwe isiwe lazima mwanadada Barbara aondoke Simba na lazima kumkomesha.

Huu uzi utakuwa kama kumbukumbu kuona nani atakuwa wa kwanza kuondoka Simba
Manara ni lazima aondoke mapema,kumtoa barbara maana yake mo nae atasambaa

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Wanaotaka manara afe njaa kisa mkataba ambao hajaingia yeye ndio wapumbavu .

Otherwise mo na kampuni zake wangeweka Ofa Nene mezani inatakayo muhusisha manara moja kwa moja sio Simba .
Hpa solution iliyopo ni Manara aache kazi simba ili awe huru kufanya kazi na kampuni anayotaka.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kwa sasa Simba ni Mali ya mtu binafsi sio Kikundi mpaka mkae vikao sasa hv Bosi akiamua uondoke hakuna atakae pinga kwahiyo Manara hana chake Simba
 
Bahati nzuri GENTAMYCINE nakujua vyema tu kuanzia ukiwa Mwenezi CCM, wana Familia wako ( hasa Dada zako pale Kwenu Buguruni na Ilala ) na pia ulipokuwa Msemaji wetu Simba SC.

Kabla sijasahau nisiwe mchoyo wa Shukran na Pongezi kwa input yako Kubwa uliyoiweka ndani ya Klabu yetu ya Simba SC na niseme tu Kwako Asante kwa Utendaji wako Klabuni Simba kwa muda wote uliokuwepo.

Sasa naanza Kukusiliba ( Kukusema )

USWAHILI
Haji Manara binafsi nilivyoona Simba SC imeanza kuwa ya Kiustaarabu basi hata nawe pia ungekuwa na huo Ustaarabu ila bahati mbaya ukaendeleza Uswahili wako wa Kariakoo, Ilala Bungoni na Buguruni.

KUDEKA KITOTO SANA
Haji Manara mara nyingi sana pale ukiguswa tu na Wapinzani wako umekuwa ukipenda zaidi Kudeka ili uonekane ni Muhimu zaidi ya Wengineo Klabuni Simba.

ULEMAVU WAKO KUTAFUTA HURUMA
Haji Manara hujaanza leo kupenda kuutumia Ulemavu wako wa Ngozi ulionao kama sehemu ya kutafutia Huruma kwa Mashabiki wa Simba pale tu ukishambuliwa na Maadui zako wa Kimchezo ili utetewe zaidi.

KUJISAHAU NA DHARAU
Haji Manara ulivyoanza Kazi ya Usemaji Simba SC ulikuwa na Nidhamu nzuri ila baadae ukaanza kubadilika taratibu na kuwa na Dharau ambayo ndiyo imekugharimu sasa.

UMAARUFU ULIOKUPA KIBURI
Haji Manara kataa uwezavyo ila ukweli utabaki kuwa ya kwamba Umaarufu ulionao kwa kuupatia Simba SC ndiyo umekupa Kiburi ulichonacho ambacho Kimekugharimu zaidi.

KUKENGEUKA KIMAADILI
Haji Manara hujaanza Kulalamikiwa leo na Waandishi wa Habari ( ambayo pia ni Fani yako ) kwa tabia yako ya kupenda Kuwatukana, Kuwaxhihaki na hata Kuwadhalilisha Kitendo ambacho ni very unprofessional and unethical kwa nafasi muhimu uliyokuwa nayo ndani ya Simba SC.

Haji Manara je, Professional Ethics zako zinasema umtishie na umdhalilishe immediate Boss wako CEO Mitandaoni wakati channels za Kupeleka Malalamiko yako unazijua? Huu ndiyo Usomi wako.ulionao na ulipoishia?

UNA KIPAJI CHA UNAFIKI SANA
Haji Manara ni Wewe huyu huyu mara nyingi ukiwa katika Interviews zako ulikuwa ukimsifia mno Senzo Mazingiza (Former Simba CEO), Barbara Gonzalez (Simba SC Current CEO) na Zackaria Hanspoppe ila leo umegeuka na Kuwashutumu na Kuwachafua kwa wanasimba ili Kuwaharibia kama Wewe ulivyojiharibia.

UWONGO
Haji Manara nadhani kwakuwa CCM ilikupeleka nje Kusomea Propaganda (Uwongo) huenda Masomo ya huko yalikuingia vizuri na sasa unakifanyia Kazi.

Umasema kuwa hapo Simba SC hulipwi Mshahara na kwamba sijui huna Mkataba.

Haji Manara una uhakika wa haya? Haji siyo Wewe ambaye kila Mwezi ( ukitoa Posho ) zako huwa unapewa Tsh Milioni Mbili na Simba SC huku Posho zako za Mwezi zikikaribia Tsh Milioni Moja? Hiyo Tsh Laki Saba unayoisema umetoa wapi wakati hiyo huwa ni Pesa yako ya Vocha ya Simu na Internet yako kwa Mwezi mzima? Haji Manara Uislamu ulionao unaruhusu kuwa Muongo hivi?

Mbona hujasema mpaka leo umekataa Kusaini Mkataba mpya wa Mshahara wa Tsh Milioni Nne ( 4 ) kwa Mwezi?

MCHOCHEA CHUKI NA MGAWANYIKO BAINA YA WACHEZAJI WA SIMBA SC
Haji Manara hivi kuna asiyekujua Wewe kuwa na tabia ya Kuchochea Chuki kwa Wachezaji wa Kigeni na wazawa?

Haji siyo Wewe uliyetukanwa na aliyekuwa Kocha wa Simba SC Patrick Aussems kwa Kukuita Mpumbavu na usimuingilie Kazini alipokuwa hawapangi Wachezaji wako unaokuwa nao sana Baa Kulewa?

HUNA UKOMAVU WA KIUME
Haji Manara ni nani alikuambia kuwa ukigombana na Wakuu ( Viongozi ) basi Suluhu ni Kukimbilia Mitandaoni Kulalamika na kutafuta Huruma kwa Mashabiki?

Haji Manara hivi Yanga SC walipomsimamisha aliyekuwa Katibu Mkuu wao ( Mwanasheria kama sijakosea ) Patrick Simon ulimsikia akipaparika Mitandaoni kama Wewe vile kulia lia na Kudeka?

Simba SC kuna muda ilimsimamisha Meneja wake Patrick Rweymamu ( Mtani wangu wa Kihaya ) je, Yeye nae alipaparika hovyo Mitandaoni kama Wewe?

SIMBA SC ULIIKUTA AU IMEKUKUTA?
Haji Manara acha Kudanganya Watu kuwa Wewe ndiyo umehamasisha Mashabiki wa Simba SC kujaa Viwanjani.

Klabu ya Simba imekuwa na rekodi ya kujaza Uwanja kutokea kwa Mashabiki wake tangia miaka ya 80 mpaka hii leo.

Ni Soka safi la Simba SC ndiyo linavutia na Kuhamasisha Mashabiki kujaa na siyo Sauti yako na maneno yako ya Kihuni na wakati mwingine ya Kishamba.

KUTUMIKA NA YANGA SC NA KUISALITI SIMBA SC KILA IKIKUTANA NAO
Haji Manara nani asiyejua kuwa Wewe ili Kumridhisha Mkeo (Shabiki wa Yanga SC japo unadai umembadili kuwa Simba SC), Baba yako Mzazi (Kipenzi chako kabisa), Gharib Said Mohammed (GSM) na Injinia Hersi Said (Marafiki zako na Mabosi zako wakubwa) na Kiongozi Mmoja Mstaafu Tanzania ambaye uko nae karibu wote hawa huwa wanakutumia kuihujumu Simba SC kila ikicheza na Yanga SC?

Labda leo nikupasulie ukweli wako Haji unadhani wana Simba SC hatujui kuwa Mechi yetu na Yanga SC hii ya Juzi tu Wewe ndiyo uliuza Ramani ya Vita kwa Yanga SC na ukalipwa na GSM kwa Kuwatahadharisha Yanga SC wasipitie Mageti yale makubwa Mawili ambayo Simba SC tulikuwa tayari tumeshafanya Unyangindo (tumeroga mno) na wakapita Kwingineko?

Nilikutana na Kocha Msaidizi wa Simba SC (Mtani wangu wa Kiha) Selemani Matola Veron Mzambia na kumuambia kuwa nina Hasira zaidi nawe na ningebahatika kukutana nawe ningekuzaba Kibao japo najua unatembea na (unamiliki) Bastola yako.

Ulivyo Mpuuzi ukasahau kuwa tayari Simba SC imeshakushtukia ambapo katika muendelezo wako ule ule wa Usaliti na Kuihujumu Simba SC kuelekea Mechi ya Fainali ASFC juzi Usiku ulionekana Avic Town Kigamboni ilipo Kambi ya Yanga SC ukiwa na Tajiri yako Gharib.

UTETEZI WA KIPUMBAVU ZAIDI
Haji Manara sijui ni kwanini unatumia Nguvu kubwa Kujitetea juu ya Shutuma zako wakati wenye Akili kukuzidi na tunaokujua tumeshakudharau.

Leo umekuja tena na Voice Note yako nyingine ukiwa Unalia huku kama vile Ukiilaani Klabu na baadhi ya Watendaji wake kuwa wana Chuki na Wewe.

VITISHO VYAKO VYA KIPUUZI
Naona umetoka Kuuendeleza ule ule Upuuzi wako katika Ukurasa wako wa Instagram ambako umesema kuwa Umechoka Kusakamwa ma kwamba Jumatatu ijayo utasema kila Kitu (utatema) nyongo na kwamba Tanzania itasimama.

KAULI YA GENTAMYCINE KWAKO
Haji Manara nami nakuambia hapa hapa kuwa ukimaliza tu Kuichafua Klabu yangu ( yetu ) ya Simba SC na Viongozi wake nami nakwenda Kuweka hadharani hapa Mabaya yako yote uliyoyafanya na unayoyafanya sasa.

Nakuonya tumia Siku hizi Tatu (3) kabla ya kufika hiyo Jumatatu kujitafakari na nakuambia usije ukathubutu kutuchafua Simba SC kwani Mimi GENTAMYCINE ndiyo nitakuchafua kuliko ( zaidi ) na hutoamini kwani nakujua ndani nje na nina Siri zako kibao tu ambazo Mbili nikiziweka hadharani lazima Central Police ikuhusu na Ofisi ya DCI ikuhusu.

Najua unayopanga Kuyaongea hiyo Jumatatu ijayo ni yafuatayo.....

1. Uhusiano wa CEO na Mwekezaji

2. Suala la Mchezaji Jonas Mkude

3. Kuondoka kwa aliyekuwa CEO Simba SC Senzo Mazingiza

4. Sakata la Bernard Morrison

5. Hanspoppe na Usajili wa Wachezaji

6. Siri za Ushindi wa Simba SC ndani na nje ya Uwanja

7. Uwekezaji wa Mohammed 'Mo' Dewji ndani ya Klabu ya Simba.

HITIMISHO

Haji Manara wana Simba SC tulikupenda sana na hara Kukutetea ila Mafanikio yako ya Umaarufu na Vijisenti vimekufanya Uvimbe Kichwa na ujione uko juu ya Simba SC ukisahau kuwa ni Simba SC ndiyo imekujenga na kukukuza hadi hao Wanafiki na Marafiki zako wa Yanga SC Wanakupenda na Kukutumia Kuihujumu Simba SC.

Ushauri wangu mkubwa tu Kwako ni kwamba nyamaza, achana na Simba SC angalia Maisha yako mengine baada ya Simba SC.

Tena ikikupendeza zaidi bado hujachelewa Kiungwana kabisa unaweza ukatuomba Radhi ( Msamaha ) wana Simba SC, kiri Makosa yako nasi kwa Roho safi na mkunjufu tutakusamehe na hata Kukuombea Jukumu lingine ndani ya Simba SC ila siyo la kuwa Msemaji Wetu tena.

ANGALIZO

Wale ambao mtapenda kutumia hili andiko langu katika Blogs zenu, Redio na Magazeti tafadhali nawaruhusu mtumie ila tendeni Haki tu kwa kufanya Acknowledging au Source Crediting kwa kusema mmetoa hapa JamiiForums na Kwake GENTAMYCINE na siyo Mdanganye imetoka Ubongoni mwenu kwani mtanivunja moyo kuja na 'analysis' zangu zaidi huko mbeleni.

Cc: billduke
Kumbe mlikuwa mmeroga? Yanga haturogeki pussi wewe
 
Inategemea matokeo ya Kigoma. Simba ikifungwa Haji ataibuka kidedea na Barbara na genge lake watakaa mkao wa kuondoka.

Simba ikishinda, Manara hana chake tena pale Simba!

Ni bora Manara atoe ushirikiano kwa Yanga ishinde!!
 
manara ndio ataanza kuondoka .
Ila na wengine wote watakuja kuondoka na kuiacha timu ya simba .
Timu ya simba itaendelea kuwepo akina mo, babra,zacharia nao watakuja kuondoka na kuiacha simba
 
Moo aondoke ili Simba wafurugane wenyewe hapo lzm yanga atakah kileleni ...ila naona kwa jicho lingine kuwa marana anatumika kiakili Sana kudhoofisha Simba ili Azam na yanga waje ije kuwa tisho mbeleni ..mnk moo akiondoka tu yangaa iyoo kwa kas ya ajabu . .manara atakuja kuuvuruga mpira wa tz tusubiri tuone
 
Kabla ya uzi wako kuwasilisha hapa jukwaani tayari Manara keshajipiga chini yeye mwenyewe.
 
yani Mo akiambiwa achague kati ya pisi kali na Manara unadhani atachagua nini?
 
Wapumbavu humu wengi..

Kocha wa Liverpool ana Mkataba na Adidas
Licha ya Liverpool kuwa na Mkataba na Nike

Kuna mipumbavu humu mingi haijui kazi kuongea utumbo
Uwezi kuchangia bila kutukana watu,unafikili mawazo yako wewe ni sahihi,kama ingekuwa mawazo yako ni sahihi, usingekuwa unafungua nyuzi hapa ili watu wachangie mawazo Yao,ungebaki na mawazo yako na kile unachokiamini full stop,jifunze kueshimu watu hata kama ukubaliani na mawazo yako,uenda hujui lolote pia.
 
Heheheh ndio biashara za kibongo! Boss anataka anaowanunia na wewe uwanunie [emoji23][emoji23][emoji23]
ila mzee soka la ulaya sio kama la bongo..Soka la ulaya Ni uwanjani while Soka la bongo Ni Hujuma,Visanga,uchawi,fiigisu nk.
Kwahyo mtu akiwa ndumila kuwili lazima awaharibie tu Na lazima mmshtukie
 
Ugomvi ubakie kwa Manara na hao wahindi, wasiwaingize mashabiki na wanachama wa Simba.
 
Hanspope aache unafiki milioni4 pesa gani walau milioni8 tuwe wakweli Simba ya Manara ni Simba tofauti sana, thamini kazi ya Manara, mnaona wivu thamani anayopata huko nje ndio mnajenga hisia za kiutopolo. Manara hata Yanga itamfaa tu maana kaishi ndani ya Yanga maish yake yote.
Kwahio una amini maneno ya Manara ndio yameijenga Simba?
 
Manara amejivua nguo kirahisi sana, nilishangaa tukielekea game ya Simba na Yanga jpili Manara anakuja na madai ya kijinga tena kupitia Kitenge Tv kumlaumu Barbara kwanini asingepeleka madai yake kwa uongozi?

Jamaa ni msaliti afukuzwe Simba, ameahajiona yuko sawa na klabu ya Simba, wakati Simba ndio ilimuokota akiwa amepauka vumbi kariakoo.
 
Back
Top Bottom