Hans Pope: Manara hataki kusaini mkataba ambao atalipwa milioni 4
Mvimbisheni kichwa huyo ndezi, siku akitimuliwa Simba akakosa support ya mashabiki wa Simba kwenye aacount zake za mitandao ndio atafurahi, anajidai mjanja wakati ujanja alionao ameupata toka kwa mashabiki wa Simba, hao followers wake watasambaratika abaki na utopolo peke yao.
 
ila mzee soka la playa sulaya bongoio kama la bongo..Soka la ulaya Ni uwanjani while Soka la bongo Ni Hujuma,Visanga,uchawi,fiigisu nk.
Kwahyo mtu akiwa ndumila kuwili lazima awaharibie tu Na lazima mmshtukie
Ni balaa mala mzee mpili anahusika vitimbi kibao
 
kila siku unakumbushwa kuchunga domo lako unajifanya kichwa ngumu

Ban zitakukimbiza jf mwaka huu
Bahati nzuri GENTAMYCINE nakujua vyema tu kuanzia ukiwa Mwenezi CCM, wana Familia wako ( hasa Dada zako pale Kwenu Buguruni na Ilala ) na pia ulipokuwa Msemaji wetu Simba SC.

Kabla sijasahau nisiwe mchoyo wa Shukran na Pongezi kwa input yako Kubwa uliyoiweka ndani ya Klabu yetu ya Simba SC na niseme tu Kwako Asante kwa Utendaji wako Klabuni Simba kwa muda wote uliokuwepo.

Sasa naanza Kukusiliba ( Kukusema )

USWAHILI
Haji Manara binafsi nilivyoona Simba SC imeanza kuwa ya Kiustaarabu basi hata nawe pia ungekuwa na huo Ustaarabu ila bahati mbaya ukaendeleza Uswahili wako wa Kariakoo, Ilala Bungoni na Buguruni.

KUDEKA KITOTO SANA
Haji Manara mara nyingi sana pale ukiguswa tu na Wapinzani wako umekuwa ukipenda zaidi Kudeka ili uonekane ni Muhimu zaidi ya Wengineo Klabuni Simba.

ULEMAVU WAKO KUTAFUTA HURUMA
Haji Manara hujaanza leo kupenda kuutumia Ulemavu wako wa Ngozi ulionao kama sehemu ya kutafutia Huruma kwa Mashabiki wa Simba pale tu ukishambuliwa na Maadui zako wa Kimchezo ili utetewe zaidi.

KUJISAHAU NA DHARAU
Haji Manara ulivyoanza Kazi ya Usemaji Simba SC ulikuwa na Nidhamu nzuri ila baadae ukaanza kubadilika taratibu na kuwa na Dharau ambayo ndiyo imekugharimu sasa.

UMAARUFU ULIOKUPA KIBURI
Haji Manara kataa uwezavyo ila ukweli utabaki kuwa ya kwamba Umaarufu ulionao kwa kuupatia Simba SC ndiyo umekupa Kiburi ulichonacho ambacho Kimekugharimu zaidi.

KUKENGEUKA KIMAADILI
Haji Manara hujaanza Kulalamikiwa leo na Waandishi wa Habari ( ambayo pia ni Fani yako ) kwa tabia yako ya kupenda Kuwatukana, Kuwaxhihaki na hata Kuwadhalilisha Kitendo ambacho ni very unprofessional and unethical kwa nafasi muhimu uliyokuwa nayo ndani ya Simba SC.

Haji Manara je, Professional Ethics zako zinasema umtishie na umdhalilishe immediate Boss wako CEO Mitandaoni wakati channels za Kupeleka Malalamiko yako unazijua? Huu ndiyo Usomi wako.ulionao na ulipoishia?

UNA KIPAJI CHA UNAFIKI SANA
Haji Manara ni Wewe huyu huyu mara nyingi ukiwa katika Interviews zako ulikuwa ukimsifia mno Senzo Mazingiza (Former Simba CEO), Barbara Gonzalez (Simba SC Current CEO) na Zackaria Hanspoppe ila leo umegeuka na Kuwashutumu na Kuwachafua kwa wanasimba ili Kuwaharibia kama Wewe ulivyojiharibia.

UWONGO
Haji Manara nadhani kwakuwa CCM ilikupeleka nje Kusomea Propaganda (Uwongo) huenda Masomo ya huko yalikuingia vizuri na sasa unakifanyia Kazi.

Umasema kuwa hapo Simba SC hulipwi Mshahara na kwamba sijui huna Mkataba.

Haji Manara una uhakika wa haya? Haji siyo Wewe ambaye kila Mwezi ( ukitoa Posho ) zako huwa unapewa Tsh Milioni Mbili na Simba SC huku Posho zako za Mwezi zikikaribia Tsh Milioni Moja? Hiyo Tsh Laki Saba unayoisema umetoa wapi wakati hiyo huwa ni Pesa yako ya Vocha ya Simu na Internet yako kwa Mwezi mzima? Haji Manara Uislamu ulionao unaruhusu kuwa Muongo hivi?

Mbona hujasema mpaka leo umekataa Kusaini Mkataba mpya wa Mshahara wa Tsh Milioni Nne ( 4 ) kwa Mwezi?

MCHOCHEA CHUKI NA MGAWANYIKO BAINA YA WACHEZAJI WA SIMBA SC
Haji Manara hivi kuna asiyekujua Wewe kuwa na tabia ya Kuchochea Chuki kwa Wachezaji wa Kigeni na wazawa?

Haji siyo Wewe uliyetukanwa na aliyekuwa Kocha wa Simba SC Patrick Aussems kwa Kukuita Mpumbavu na usimuingilie Kazini alipokuwa hawapangi Wachezaji wako unaokuwa nao sana Baa Kulewa?

HUNA UKOMAVU WA KIUME
Haji Manara ni nani alikuambia kuwa ukigombana na Wakuu ( Viongozi ) basi Suluhu ni Kukimbilia Mitandaoni Kulalamika na kutafuta Huruma kwa Mashabiki?

Haji Manara hivi Yanga SC walipomsimamisha aliyekuwa Katibu Mkuu wao ( Mwanasheria kama sijakosea ) Patrick Simon ulimsikia akipaparika Mitandaoni kama Wewe vile kulia lia na Kudeka?

Simba SC kuna muda ilimsimamisha Meneja wake Patrick Rweymamu ( Mtani wangu wa Kihaya ) je, Yeye nae alipaparika hovyo Mitandaoni kama Wewe?

SIMBA SC ULIIKUTA AU IMEKUKUTA?
Haji Manara acha Kudanganya Watu kuwa Wewe ndiyo umehamasisha Mashabiki wa Simba SC kujaa Viwanjani.

Klabu ya Simba imekuwa na rekodi ya kujaza Uwanja kutokea kwa Mashabiki wake tangia miaka ya 80 mpaka hii leo.

Ni Soka safi la Simba SC ndiyo linavutia na Kuhamasisha Mashabiki kujaa na siyo Sauti yako na maneno yako ya Kihuni na wakati mwingine ya Kishamba.

KUTUMIKA NA YANGA SC NA KUISALITI SIMBA SC KILA IKIKUTANA NAO
Haji Manara nani asiyejua kuwa Wewe ili Kumridhisha Mkeo (Shabiki wa Yanga SC japo unadai umembadili kuwa Simba SC), Baba yako Mzazi (Kipenzi chako kabisa), Gharib Said Mohammed (GSM) na Injinia Hersi Said (Marafiki zako na Mabosi zako wakubwa) na Kiongozi Mmoja Mstaafu Tanzania ambaye uko nae karibu wote hawa huwa wanakutumia kuihujumu Simba SC kila ikicheza na Yanga SC?

Labda leo nikupasulie ukweli wako Haji unadhani wana Simba SC hatujui kuwa Mechi yetu na Yanga SC hii ya Juzi tu Wewe ndiyo uliuza Ramani ya Vita kwa Yanga SC na ukalipwa na GSM kwa Kuwatahadharisha Yanga SC wasipitie Mageti yale makubwa Mawili ambayo Simba SC tulikuwa tayari tumeshafanya Unyangindo (tumeroga mno) na wakapita Kwingineko?

Nilikutana na Kocha Msaidizi wa Simba SC (Mtani wangu wa Kiha) Selemani Matola Veron Mzambia na kumuambia kuwa nina Hasira zaidi nawe na ningebahatika kukutana nawe ningekuzaba Kibao japo najua unatembea na (unamiliki) Bastola yako.

Ulivyo Mpuuzi ukasahau kuwa tayari Simba SC imeshakushtukia ambapo katika muendelezo wako ule ule wa Usaliti na Kuihujumu Simba SC kuelekea Mechi ya Fainali ASFC juzi Usiku ulionekana Avic Town Kigamboni ilipo Kambi ya Yanga SC ukiwa na Tajiri yako Gharib.

UTETEZI WA KIPUMBAVU ZAIDI
Haji Manara sijui ni kwanini unatumia Nguvu kubwa Kujitetea juu ya Shutuma zako wakati wenye Akili kukuzidi na tunaokujua tumeshakudharau.

Leo umekuja tena na Voice Note yako nyingine ukiwa Unalia huku kama vile Ukiilaani Klabu na baadhi ya Watendaji wake kuwa wana Chuki na Wewe.

VITISHO VYAKO VYA KIPUUZI
Naona umetoka Kuuendeleza ule ule Upuuzi wako katika Ukurasa wako wa Instagram ambako umesema kuwa Umechoka Kusakamwa ma kwamba Jumatatu ijayo utasema kila Kitu (utatema) nyongo na kwamba Tanzania itasimama.

KAULI YA GENTAMYCINE KWAKO
Haji Manara nami nakuambia hapa hapa kuwa ukimaliza tu Kuichafua Klabu yangu ( yetu ) ya Simba SC na Viongozi wake nami nakwenda Kuweka hadharani hapa Mabaya yako yote uliyoyafanya na unayoyafanya sasa.

Nakuonya tumia Siku hizi Tatu (3) kabla ya kufika hiyo Jumatatu kujitafakari na nakuambia usije ukathubutu kutuchafua Simba SC kwani Mimi GENTAMYCINE ndiyo nitakuchafua kuliko ( zaidi ) na hutoamini kwani nakujua ndani nje na nina Siri zako kibao tu ambazo Mbili nikiziweka hadharani lazima Central Police ikuhusu na Ofisi ya DCI ikuhusu.

Najua unayopanga Kuyaongea hiyo Jumatatu ijayo ni yafuatayo.....

1. Uhusiano wa CEO na Mwekezaji

2. Suala la Mchezaji Jonas Mkude

3. Kuondoka kwa aliyekuwa CEO Simba SC Senzo Mazingiza

4. Sakata la Bernard Morrison

5. Hanspoppe na Usajili wa Wachezaji

6. Siri za Ushindi wa Simba SC ndani na nje ya Uwanja

7. Uwekezaji wa Mohammed 'Mo' Dewji ndani ya Klabu ya Simba.

HITIMISHO

Haji Manara wana Simba SC tulikupenda sana na hara Kukutetea ila Mafanikio yako ya Umaarufu na Vijisenti vimekufanya Uvimbe Kichwa na ujione uko juu ya Simba SC ukisahau kuwa ni Simba SC ndiyo imekujenga na kukukuza hadi hao Wanafiki na Marafiki zako wa Yanga SC Wanakupenda na Kukutumia Kuihujumu Simba SC.

Ushauri wangu mkubwa tu Kwako ni kwamba nyamaza, achana na Simba SC angalia Maisha yako mengine baada ya Simba SC.

Tena ikikupendeza zaidi bado hujachelewa Kiungwana kabisa unaweza ukatuomba Radhi ( Msamaha ) wana Simba SC, kiri Makosa yako nasi kwa Roho safi na mkunjufu tutakusamehe na hata Kukuombea Jukumu lingine ndani ya Simba SC ila siyo la kuwa Msemaji Wetu tena.

ANGALIZO

Wale ambao mtapenda kutumia hili andiko langu katika Blogs zenu, Redio na Magazeti tafadhali nawaruhusu mtumie ila tendeni Haki tu kwa kufanya Acknowledging au Source Crediting kwa kusema mmetoa hapa JamiiForums na Kwake GENTAMYCINE na siyo Mdanganye imetoka Ubongoni mwenu kwani mtanivunja moyo kuja na 'analysis' zangu zaidi huko mbeleni.

Cc: billduke
 
Mzee punguza povu, eleza huo mkataba wa jurgen klopp unavyompa mipaka. Ndiyo maana haji mwenyewe amegoma kusaini kandarasi ya milioni 4 kwa mwezi, kwa sababu kandarasi hiyo itampa mipaka. Ndiyo maana yupo hapo Simba na ameridhika na laki 7 lkn anapiga mpuga wa zaidi ya milioni 5 huko kwenye hizo kampuni zingine. Kumbuka haji anapata hizo kandarasi zingine kwa sababu yupo Simba, nje ya simba hawezi kupata! Na Simba hatuhitaji tena kuibeba hii takataka..haji alibaki Simba kwa sababu huruma, lkn siyo kwa umuhimu. Haji ni mlemavu wa ngozi, ukimchukulia hatua bila tahadhari, watu watasema ulemavu wake ndo sababu. Hilo ndo limefanya tubaki naye pamoja na makosa yake. Haji ana barua za kuonywa hata 16 zinafika. Lkn bado anajiona yy ni mkubwa kuliko hata Simba!
Simba ni genge la wezi wenye uzoefu
 
Kipindi hicho simba haikuwa na mdhamini mwenye bidhaa zinazofanana na azam, mo alipoanza kuidhamini Simba Mambo yalitakiwa kubadilika. Kwani haji anapotangaza bidhaa ambazo hazihusiani na mdhamini wa Simba ushawahi kusikia mtu akilalamika.
Pia mkataba alionao Sasa na azam kausaini wakati akiwa Simba.
Haji anatumia Media za club kutangaza bidhaa za wateja wake??

MO amesema mauzo ya bidhaa zake yameshuka kutokana na hili??

Muda umefika wa MO na genge lake kutuachia timu yetu.
 
Hivi msemaji wa timu ya Brazili ya River Plate, aonekana anatangaza biashara za Boca junior, unachinjwa siku hiyohiyo.
Kama angechinjwa msemaji wa Yanga, angethubutu kutangaza biashara za MO Dewji. Angeshazikwa.
 
Wapumbavu humu wengi..

Kocha wa Liverpool ana Mkataba na Adidas
Licha ya Liverpool kuwa na Mkataba na Nike

Kuna mipumbavu humu mingi haijui kazi kuongea utumbo
Haji anaweza jitofautisha kiasi hicho?

kibongobongo wangapi really respect mikataba kiasi hicho?..
 
Haji niwakupiga makofi na bora hajaenda kigoma tungepiga sana,, ngoja tumalize hili la kigoma ili tumsaidie kubeba mizingo vizuri kuelekea GSM sehem ambayo atakua huru sana kufanya mambo Yake sisi simba hatumtaki kabsa
Hakuna wakumtisha Haji
 
Mkataba huo wa milioni 4 ungempunguzia sana mapato Manara na kumfunga.

Manara alitaka kupewa mkataba wa kizamani na hovyo kabisa, yani hata account ya instagram ya manara ingekuwa chini ya kina Mo, kwa umaarufu wa Manara na watu wanavyomfatilia wangeigeuza account kuwa sehemu ya kujitangazia bure matangazo yao wakati mmiliki ni manara,

Mkataba pia ungemfunga manara kutoweza kusaini dili lolote nje ya usemaji wa club simba, yani awe i msemaji tu, pidi ikitokea dili basi wazee wa mgao inabidi wale jasho lake

Huu mkataba ni wa kizamani sana na umekaa kufungiana ridhiki tu, kwa wenzetu huko nje mtu anaweza kufanya kazi kampuni ya NIKE wakati mdhamini wa jezi ya timu anayofanyia kazi ni ADIDAS ambao ni wahasimu wakubwa wa Nike na wala hakuna migongano, hii yote ni kumfungulia mtu fursa za kimaendeleo na kiuchumi.

Tatzo wivu tu a roho za kwanini haji apate mafanikio nje ya kuisemea simba? Angalia mfano tu mdogo haji manara ana nyumba yake,magari yake, na mali nyingine, hii ni kutokana na mikataba minono kutoka kwa asas, gsm na azam ambao pasi na shaka wanampa pesa za kutosha manara, pengine hata ile faini ya milioni 5 aliyoambiwa aende kuilipa tff alipewa na hayo makkampuni mengine ili atunze brand yake, mfano mwengine angalia siku ya harusi ya haji wale GSM walifanya kufuru kumtunza haji.

Manara kauppiga mwingi hapa, kakataa kubanwa kweye mtego wa kuifanyia kazi simba pekee kitu ambacho kingembana awe anatangaza bidhaa za MO pekee ama ndugu zake, Manara ana familia na inamtegemea kuna kipindi atatoka simba ila maisha yake mke wake na wanae bado watabaki kumtegemea, kwahio ni haki yake kutafuta deals nje ya simba ili kuongeza kipato na kuweza kusimama hata pakle akiacha kuitegemea simba, so hongera kwake manara.

HITIMISHO: Simba wakae upya, utauzi wa hili jambo sio kumfukuza manara bali wanaweza kurekebisha kasoro za mkataba
Sasa kama anapata hela zote hizo nje ya Simba analialia nini si aondoke..aende uko anakolipwa vizuri aendeleze mapambano
 
Hizi ni propaganda za kutaka kututoa wana jangwani mchezoni wanajifanya wanalumbana kumbe ni trik tu ya kutufanya tuwe overconfidence hiyo j2 halafu tupotee nasema kwa hili HAMTOBOI
 
Kwa muda mrefu Haji amekuwa akijihusisha na GSM kama one of the brand ambassador na pia amekuwa brand ambassador wa wafadhili wa azam. Tatizo ni kwamba kuwa ambassador huko kwingine kunamnyima yeye nafasi ya kutangaza bidhaa za mtu ambaye amewekeza pesa nyingi pale Simba kwa sababu za kimikataba na hao wengine.

Sasa haiingii akilini, muajiriwa wasimba anashindwa kutangaza bidhaa za mdhamini wa Simba, ila anaenda kutangaza bidhaa za madhamini wa Yanga!

Hivi ishawahi kufikiria leo Hasan bumbuli awe na mkataba wa kibiashara na Mo dewji kutangaza bidhaa zake na mashabiki wa yanga wamuangalie tu?

Linapokuja swala la mshahara, Simba wanampa laki Saba huku hao wengine wanampa wakimpa zaidi ya million 5 Sasa unafikiri huyo anayempa million 5 akija kumuomba taarifa za huyu anayetoa laki 7 atakataa?? Ni halali viongozi wa Simba kuwa na mashaka na haji manara.
Ndugu Simba au Yanga si baba sio mama yako linapokuja swala la pesa piga pesa kwani pilika za ujana ndizo zitakazochagua uzeeke kama Kikwete au Mzee Mpili..mwana FA,Ommy dimpoz wanafanya kazi na GSM na mashabiki wa kutupwa wa mnyama...Manara ni kweli anakera kushirikiana na GSM lkn bado itabaki kuwa MoneyIsOverEverything.
 
Back
Top Bottom