Hapa Makongoro Nyerere kaamua kusema ukweli mbele ya Rais bila kupepesa macho

Hapa Makongoro Nyerere kaamua kusema ukweli mbele ya Rais bila kupepesa macho

Hii kauli ni kubwa sana. Kuwa watoto wa viongozi wanapata nafasi si kwa sababu wamewahi fanya matendo makubwa ila ni sababu tu ya majina ya watoto wao.

Nadhani alikuwa anamaanisha yeye, Ridhiwani Kikwete, Januari Makamba, Nape Nnauye n...
Uzuri wa mzee wa site ni kuwa yeye keshashiba tayari ni tofauti na hawa watoto wa wachovya asali ambao utamu wa jumba jeupe wameanza kuujua baada ya baba zao kuwa manyapara.
 
Makongoro akiwa anapiga speech live on a national yelevision inahitaji ujasiri maana street language za kutosha
Jamaa kitaa sana na anaweza kutoa boko any moment...
Makongoro ni burudani tosha haboi hata kidogo na moyo wake ni mweupe pee[emoji28][emoji28]
 
..huyu jamaa ni mlevi-mlevi tu anabugia mshahara kwa kodi za Watz kwasababu ni mtoto wa Nyerere.

..ndio maana KATIBA MPYA ni muhimu ili wananchi wasiendelee kubeba mizigo kama hii.
Bora mlevi asiye mwizi kuliko Shekhe jambazi
 
Kaongea tu, lakini Makongoro ni mpambanaji sana tena bila hata kutegemea jina la baba yake.

Alikuwa Jeshini. Akaenda vitani Uganda.

Aligombea Ubunge Arusha kupitia NCCR Mageuzi 1995 baba yake akiwa hai na akashinda.

Na siku zote amekuwa yeye Kama yeye kifikra na Mambo yake.
Sio chawa kabisa
 
Na Makongoro hajawahi kuwa mjinga anaongea kijinga kijinga lakini hapotezagi point wala lengo

Hebu muulize lengo lilikuwa ni nini kwa kusisitiza kwake hii hoja ya kupumzika. Alikuwa anataka habari hizi ziwafikie wakina nani walioko wapi?
 
Hawa watoto wa Nyerere sio chawa, hawajipendekezi kwa viongozi ili wapewe chakula, baba yao alishawakomaza waishi kibishi toka miaka hiyo. Kwa sasa watawala wanawapa madaraka ili kuficha aibu ya watoto wao au wa marafiki zao wanaowabeba...
Sijuhi hata kama watakuelewa!

Anyway. Ujumbe. Mkubwa!
 
Muda huo huo.

Kuna Rais Mstaafu wa nchi ya jirani.

Yeye bado anaongoza nchi.

Mkewe ni Mbunge na Mwanae ni Naibu waziri.
Na mwingine, mtoto ni Generali jeshini, na pia mshauri mkuu wa rais mwenyewe, na hapo hapo mtoto akisuluhisha mtifuano wa baba yake na kiongozi wa nchi jirani.

Dalili zilizopo, baba atakapoamua kukaa pembeni, mtoto anarithi kiti cha baba yake!
 
Back
Top Bottom