Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 7,091
- 15,519
Hahahah!Mbona unakuwa mkali chief? Quran ya uthman ilipelekwa Baghdad, Damascus, Mecca na madina. Miji yote hiyo haina copy hata moja,ndiyo maana mfalme wa Misri alitoa amri itengenezwe copy 1.
Lakini pia tukiachana na hiyo Quran ya (Hafs) kutoka chuo kikuu cha Al Azhar university,kuna Quran nyingine pia sokoni zenye idadi tofauti za aya.
Hafs Quran ina aya 6236
Warsh Quran ina aya 6216
Khalaf Quran ina aya 6346
Hiki sio kitabu kimoja kutoka enzi z Mohamed chief .
Ngoja nikupatie mfano ambao utauelewa.
Nguzo za swala ni 17. Lakini wapo wengine watasema 21 na itaandikwa hivyo.
Sasa wewe hutakiwi kuchanganyikiwa bali unahitajika kuhoji ni kwa nini?
Jawabu ni kwamba; kwenye kurukuu na upatikane utulivu ndani yake, mwengine anasema hiyo ni nguzo moja.
Mwengine atasema; kurukuu ni nguzo, na kupatikana utulivu ndani yake ni nguzo nyengine, kwani kila moja ina umuhimu ndani yake.
Wa kwanza kwa jitihada yake atasema hiyo ni nguzo 1. Wa pili kwa jitihada yake atasema hizo ni nguzo mbili tayari, yaani; nguzo ya 1 kurukuu na upatikane utulivu ndani yake ni nguzo ya 2.
Na halikadhalika kwenye jitihada za kuhesabu aya napo zipo hivyo. Kwa mfano hai huo niliyokupa ndivyo kwenye Qur'an napo pia ni vivyo hivyo.
Mwengine atasema hapa kulikuwa na koma (,) mwengine atasema hapana hapa ni kituo.
Kwa hoja hii wakitofautiana mwengine atasema hii ni aya moja kwa vile kuna koma. Huyo mwengine atasema hizi ni aya mbili (2) tayari.
Hawa kwa jitihada zao wakileta idadi zao kiujumla zitatofautiana. Huyu atasema jumla kuu ni moja (1), hiyu mwengine atasema jumla kuu ni mbili (2).
Lakini ukiangalia kuna neno limeongezwa? Jawabu hapana! Kuna neno limepunguzwa? Jawabu ni hapana! Kuna maana imebadilika? Jawabu ni hapana!
Utasemaje hizi ni version tofauti? Au nini maana ya version (toleo) kwako?