ni kweli vijana wengi wa sasa hawataki kuoa single mothers, hamuoni kwamba hali hiyo inaweza kuwafanya mabinti wa Gen Z ambao ndo wengi bado hawajazaa kuwa waangalifu kupita kiasi kuhusu kupata mtoto kabla ya ndoa?
Msichana akiona kwamba dada zake waliizaa halafu wakaachwa soko linapungua, ataamua kutumia zaidi ma p2 mixer kutoa mimba sana na hata kuepuka kabisa kupata mtoto mpaka awe ameolewa rasmi. Tatizo linakuja hapo hapo ambapo vijana wengi nao wanaahirisha ndoa kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi.
Leo hii unakuta kijana ana miaka 30 bado yupo kwa wazazi, anajitafuta, hana uhakika wa kuoa. Miaka inaenda mpaka 35 au 37 ndipo anaanza kushtuka anataka mke ambaye hana mtoto kabisa na hapo ni jobless anaunga unga. anasahau kwamba wakati huo huo mabinti nao wanaogopa kuzaa mapema kwa hofu ya kuachwa na kuitwa single mother.
Swali langu lingine ni hili je, wanaowapinga mahusiano na single mothers wanamaanisha kupinga nao ndoa tu, au hata kupata mtoto nao pia?yaani kwa Mfano, mwanamke ana mtoto mmoja, ana kazi yake, anajitegemea. nyie wapinga single mother mnaonaje hapo naweza kuamua kupata mtoto pamoja bila hata kupanga kuishi kama wanandoa, bali kushirikiana tu kulea mtoto kwa makubaliano. Je, hata mfumo huo nao unaonekana si sahihi?Nauliza hivi kwa sababu inaonekana kizazi hiki kinaanza kubadili kabisa maana ya ndoa, uzazi, na familia kutokana na presha za uchumi na mahusiano.Halafu hii point kwamba eti kutakuwa na mawasiliano kati ya mzazi mwenza wa single mother imekaaje hii kwani nyie mnaishi vijijini mpaka hamuami hio mikoa yenu mara kwa mara ...me nachokiona siku hizi watu wanasafiri sana na kuhama mikoa je kwa mfano baba mtoto yupo mwanza wewe na single mother mnaishi mtwara bado ni sahihi kuwa na hofu ya kupigiwa kwamba mtu awe anatoka mwanza anakuja mtwara kuja tu kupasha kiporo duh..