Hii ndio mikoa ambayo Rais Samia amewekeza nguvu kubwa kuiletea maendeleo

Hii ndio mikoa ambayo Rais Samia amewekeza nguvu kubwa kuiletea maendeleo

Habari zenu wanaJF wenzangu,

Wakuu.... wengi wetu hapa JF na nchini kwa ujumla, tunajua kwamba raisi wa JMT mh Samia S. Hassan anapambana usiku na mchana, ili kuhakikisha serikali yake inaleta maendeleo katika wilaya, mikoa na nchi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini kama ilivyo desturi ya sisi binadamu unapokuwa na mambo, vitu au watu zaidi ya watatu ubavuni kwako, ni wazi kuwa hautoweza kubalance upendo wako kwao yani iwe mia kwa mia kwa kila mtu au kitu. Ni lazima mtu au kitu kimoja utakipenda zaidi ya kiingine.

Hili hutokea hata kwa mzazi mwenye watoto mfano wa5 hujikuta anampenda mtoto mmoja au wawili zaidi ya awapendavyo waliobaki, japo kama mzazi huwa haoneshi moja kwa moja upendeleo wake huo kutokana na kutaka wale wengine wasijisikie kubaguliwa nk.

Hivyo basi hata raisi wetu, ni raisi wa nchi nzima, lkn ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mikoa ambayo amekuwa akionesha kuipenda na kuijali zaidi ya mikoa mingine, na hili limekuwa likionekana kupitia miradi mbali mbali kabambe aliyoielekeza katika mikoa hiyo hata kama anajaribu kutokuonesha kuwa ana baze zaidi huko, lkn wafuatiliaji tunaona wenyewe kwa macho yetu na kusikia pia kwa masikio yetu.

Mikoa hiyo ambayo inabahati mno na serikali hii ni 👇

1. Dodoma.
Mkoa huu pamoja na kwamba raisi aliekuwepo madarakani hayati John P. Magufuli aliupenda na kuelekeza zaidi macho yake huko, pia umeendelea kuneemeka na uongozi huu wa awamu ya 6 chini ya raisi Samia na kupelekea miradi mingi ya maendeleo kupelekwa huko.

Nafikiri haya yamesababishwa na hadhi yake kama mji wa serikali na makao makuu ya nchi.

2. Kigoma.
Mkoa wa Kigoma pia unazali na uongozi huu wa raisi Samia. Japo mkoa huu una kiongozi mmoja mkubwa wa chama cha upinzani, na historia yake ya kupenda kuunga mkono wapinzani mbali mbali, lkn raisi Samia hakujali hayo.

Ameelekeza nguvu na miradi katika mkoa huo kuliko kiongozi mungine yoyote aliewahi kutawala kabla yake. I hope hiyo miradi ikikamilika basi Kigoma itakuwa small "Chicago", achilia mbali zile stori za mh Kikwete kwamba angeigeuza Kigoma kuwa Dubai kwa maneno tu matupu bila vitendo wala kutoa hela za miradi husika.

3. Mbeya.
Huu mkoa nao ni miongoni mwa mikoa inayofaidika kwa kasi kupitia uongozi huu wa awamu ya tano. Kabla ya hapo mkoa huo ni kama vile ulikuwa umesahaulika kimtindo, maana hata miundo mbinu ya mkoa huo kwa upande wa barabara, shule, hospital nk vilikuwa hovyo, ila toka raisi Samia aingie amekuwa akionesha kushirikiana na mbunge Mbeya mjini ambae pia ni spika wa bunge kuleta maendeleo ya kweli katika mkoa huo.

Kwa kuonesha kuwa anaupenda mkoa huo kwa vitendo, serikali ya raisi Samia tayari imeshatoa mamilioni ya miradi kwa ajili ya shule, barabara nk. Japo kuna baadhi ya watumishi wa serikali kutoka mkoa huo wanaonekana kutohitaji maendeleo katika mkoa huo kwa kutafuna mamilioni ya baadhi ya miradi kama alivyosema raisi Samia alipokuwa ziarani mkoani huko, lkn ni kama vile bado hajachoka kuendeleza miradi katika mkoa huo, bila kujali baadhi ya wapinzani ambao wao wanachotaka ni kuingia bungeni tu bila kujali maendeleo anayowaletea raisi Samia katika mkoa wao.

4. Mwanza.
Mkoa wa Mwanza pia ni kama Dodoma. Ulikuwa na zali chini ya serikali ya awamu ya 5 ya hayati Magufuli, na bado umeendelea kuwa na bahati pia chini ya serikali hii ya awamu ya 6 ya raisi Samia.

5. Mtwara....

6. Lindi....

Kama kuna mikoa mingine ambayo imeneemeka na uongozi wa raisi Samia alaf sikuiandika basi ndugu msomaji unaweza kuiandika hapo chini....

Karibuni.
Huu mradi vipi?

View: https://youtu.be/nonXm0hA3-k?si=7T2f-4uqPPqUazXS
 
Tanga inazidiwa sana kimaendeleo na mikoa mingine. Hawana msemaji- fuatilia michango ya wabunge wao katika vkao vya bunge. Hao viongozi wa kitaifa wala hawafiki wilayani hata wakti wa uchaguzi....Tanga ccm watapata kura tu. Zao la mkonge, alilofufua JPM ndio kitu pekee kinachong'ara katika uchumi wa Tanga. Mradi kama wa reli umekarabatiwa kwa fedha nyingi miundo mbinu inaanza kuchakaa tena. Mradi wa barabara ya Tga-Pangani unasuasua - who cares?
 
Mbeya hawapendeki hao na ninwajuaji sio sehemu sahihi kimkakati sana sana anamsaidia Spika Tulia tuu maana bila huyo huo Mkoa wangeshautelekeza una watu jeuri wajuaji na wabishi wanaotaka Ligi mda wote ndio maana ujenzi wao ni hovyo hovyo Bora liende.

Kuna Mikoa ni ya CCM hakuna Cha Upinzani kama Ruvuma,Manyara,Tabora,Katavi,Rukwa,Njombe,Iringa, Morogoro,Pwani,Tanga ,Lake zone yote kasoro Mara.

Kiufupi Tanzania hakuna upinzani labda ccm wakosee kuchaguana
Mbona unataka Kulia come down
 
Ndio maana maji na umeme vinasuasa hampati [emoji16][emoji16][emoji16]

Wenzenu Swax town Airport inajengwa,Tactic inaanza mwezi ujao Kwa sababu Kuna mbunge wa CCM.

Ni wakati Sasa wa kudai maendelea Kwa mbunge na madiwani wenu wa Chadema [emoji23][emoji23]

Mwisho Bora na Samia Mwendazake aliwapa nini hapo Nkasi? Miradi mtapata ila midogo midogo [emoji1787][emoji1787]
Kwa taarifa tu ni kwamba Kirando hakuna shida ya maji maana mradi wa maji umesha kamilika muda mrefu sana kuhusu umeme upo muda sana.

Hiyo Swax ni miongoni mwa manispaa masikini ndani ya Tanzania,na Jimbo la Swax-Town toka uhuru lipo chini ya Ccm ni kwa mara ya kwanza ndani ya mkoa wa Rukwa kupata MP kutoka upinzani.

Na kama kigezo Cha maendeleo ni kuchagua Ccm basi mkoa wa Rukwa ungekuwa mbele kimaendeleo,unapo sema CDM ndo walete maendeleo kwani ndio wenye serikali?
 
Huku rukwa kama kawaida yetu tulishazoea kutengwa na viongozi wa kitaifa.

Kufungua tu njia ya Namanyere-kirando kisha mizigo ivuke maji kwenda congo hawataki wanaishia kujenga bandari sehemu ambazo hazina uchangamfu walianza kipili pakafeli, saizi wako kabwe nayo itafeli.

Poor government support
Namanyere-kirando njia unatisha mnoo, nmepita majuzi huko for the first time. Kama unatoka namanyere, mbele mbele kule kuna ki daraja flan, ukiwa unapita, yaan ata kama huna dini, lazima usalie ata mizimu. Tena sio daraja moja, yapo kama matatu ivi, walaah!
FB_IMG_1695216485776.jpg
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Wakuu.... wengi wetu hapa JF na nchini kwa ujumla, tunajua kwamba raisi wa JMT mh Samia S. Hassan anapambana usiku na mchana, ili kuhakikisha serikali yake inaleta maendeleo katika wilaya, mikoa na nchi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini kama ilivyo desturi ya sisi binadamu unapokuwa na mambo, vitu au watu zaidi ya watatu ubavuni kwako, ni wazi kuwa hautoweza kubalance upendo wako kwao yani iwe mia kwa mia kwa kila mtu au kitu. Ni lazima mtu au kitu kimoja utakipenda zaidi ya kiingine.

Hili hutokea hata kwa mzazi mwenye watoto mfano wa5 hujikuta anampenda mtoto mmoja au wawili zaidi ya awapendavyo waliobaki, japo kama mzazi huwa haoneshi moja kwa moja upendeleo wake huo kutokana na kutaka wale wengine wasijisikie kubaguliwa nk.

Hivyo basi hata raisi wetu, ni raisi wa nchi nzima, lkn ukweli ni kwamba kuna baadhi ya mikoa ambayo amekuwa akionesha kuipenda na kuijali zaidi ya mikoa mingine, na hili limekuwa likionekana kupitia miradi mbali mbali kabambe aliyoielekeza katika mikoa hiyo hata kama anajaribu kutokuonesha kuwa ana baze zaidi huko, lkn wafuatiliaji tunaona wenyewe kwa macho yetu na kusikia pia kwa masikio yetu.

Mikoa hiyo ambayo inabahati mno na serikali hii ni 👇

1. Dodoma.
Mkoa huu pamoja na kwamba raisi aliekuwepo madarakani hayati John P. Magufuli aliupenda na kuelekeza zaidi macho yake huko, pia umeendelea kuneemeka na uongozi huu wa awamu ya 6 chini ya raisi Samia na kupelekea miradi mingi ya maendeleo kupelekwa huko.

Nafikiri haya yamesababishwa na hadhi yake kama mji wa serikali na makao makuu ya nchi.

2. Kigoma.
Mkoa wa Kigoma pia unazali na uongozi huu wa raisi Samia. Japo mkoa huu una kiongozi mmoja mkubwa wa chama cha upinzani, na historia yake ya kupenda kuunga mkono wapinzani mbali mbali, lkn raisi Samia hakujali hayo.

Ameelekeza nguvu na miradi katika mkoa huo kuliko kiongozi mungine yoyote aliewahi kutawala kabla yake. I hope hiyo miradi ikikamilika basi Kigoma itakuwa small "Chicago", achilia mbali zile stori za mh Kikwete kwamba angeigeuza Kigoma kuwa Dubai kwa maneno tu matupu bila vitendo wala kutoa hela za miradi husika.

3. Mbeya.
Huu mkoa nao ni miongoni mwa mikoa inayofaidika kwa kasi kupitia uongozi huu wa awamu ya tano. Kabla ya hapo mkoa huo ni kama vile ulikuwa umesahaulika kimtindo, maana hata miundo mbinu ya mkoa huo kwa upande wa barabara, shule, hospital nk vilikuwa hovyo, ila toka raisi Samia aingie amekuwa akionesha kushirikiana na mbunge Mbeya mjini ambae pia ni spika wa bunge kuleta maendeleo ya kweli katika mkoa huo.

Kwa kuonesha kuwa anaupenda mkoa huo kwa vitendo, serikali ya raisi Samia tayari imeshatoa mamilioni ya miradi kwa ajili ya shule, barabara nk. Japo kuna baadhi ya watumishi wa serikali kutoka mkoa huo wanaonekana kutohitaji maendeleo katika mkoa huo kwa kutafuna mamilioni ya baadhi ya miradi kama alivyosema raisi Samia alipokuwa ziarani mkoani huko, lkn ni kama vile bado hajachoka kuendeleza miradi katika mkoa huo, bila kujali baadhi ya wapinzani ambao wao wanachotaka ni kuingia bungeni tu bila kujali maendeleo anayowaletea raisi Samia katika mkoa wao.

4. Mwanza.
Mkoa wa Mwanza pia ni kama Dodoma. Ulikuwa na zali chini ya serikali ya awamu ya 5 ya hayati Magufuli, na bado umeendelea kuwa na bahati pia chini ya serikali hii ya awamu ya 6 ya raisi Samia.

5. Mtwara....

6. Lindi....

Kama kuna mikoa mingine ambayo imeneemeka na uongozi wa raisi Samia alaf sikuiandika basi ndugu msomaji unaweza kuiandika hapo chini....

Karibuni.
Mikoa ambayo Rais ameipa kisogo;
1. Kilimanjaro
2. Rukwa
3. Songwe
4. Tabora united
5. Shybush
6. Singida fountain gate united
Mingine nimeisahau
 
Kwa taarifa tu ni kwamba Kirando hakuna shida ya maji maana mradi wa maji umesha kamilika muda mrefu sana kuhusu umeme upo muda sana.

Hiyo Swax ni miongoni mwa manispaa masikini ndani ya Tanzania,na Jimbo la Swax-Town toka uhuru lipo chini ya Ccm ni kwa mara ya kwanza ndani ya mkoa wa Rukwa kupata MP kutoka upinzani.

Na kama kigezo Cha maendeleo ni kuchagua Ccm basi mkoa wa Rukwa ungekuwa mbele kimaendeleo,unapo sema CDM ndo walete maendeleo kwani ndio wenye serikali?
Najua Kirando Kijijini hakuna shida ya Maji,Mimi nazungumzia Jimbo la Aida-wa Chadema kiujumla ikiwemo Namanyere yenyewe hakuna Maji Wala umeme.

Pili kusema Swax ni Jimbo Maskini ni stori za kujifariji 😂🤣 Swax Ina Barabara za mtaani safi kabisa kushinda Miji Mingi sana hapa Tanzania,Mji umepangika nk.

Tangu lini Makao Makuu ya Mkoa yakawa mabaya? Kuna Miji mingapi hapa Tanzania Ina Stand nzuri kama ya Swax? Huo umaskini uko mdomoni kwako kisa mumeangishiwa kitu Kizito.

Narudia kukwambia wewe jifariji ila mtakula sana vumbi hapo Namanyere -Kirando.

Mwisho Mkoa wa Rukwa ulichekewa kidogo sababu ya Barabara ila tangu Barabara ya Tunduma-Swax-Mpanda ijengwe na wewe unajua kwamba uko on 🔥🔥🔥

Na Sasa Barabara ya Swax-Kasanga done

Ntendo-Muze-Majimoto & Kilyamatundu Iko under construction

Matai-Kasesya Border(Zambia) Iko under construction

Laela-Mwimbi-Kizombwe Iko under construction

Sumbawanga Airport Iko under construction

Tactic 12 km mjini ziko under construction

Na soon tunaanza ujenzi wa Lyazumbi-Kabwe Port Road

Hiyo ni miradi michache tuu sijataja sekta zingine,Kwa hiyo acha wivu na chuki.

Mwisho badala ya kulalamikia ccm walalamikieni Chadema maana Kila mtu atakula alikopeleka mboga 🤣🤣
 
Mikoa ambayo Rais ameipa kisogo;
1. Kilimanjaro
2. Rukwa
3. Songwe
4. Tabora united
5. Shybush
6. Singida fountain gate united
Mingine nimeisahau
Msiwe mnaropoka kama hakuna kitu unakijua.

Ameipa kidogo Kiaje? Au wewe Kwa umbumbu wako ndio hujui kinachoendelea kwenye Mikoa hiyo?

Nitataja miradi mikubwa tuu,ya size ya kati na midogo sitaji

Kilimanjaro
-Amajemga Moshi Airport

-Anajenga Barabara ya KIA,Tarakea Rombo nk

Rukwa-Sirudii nimeshaeleza sana humu

Songwe
Anajenga Barabara ya Tunduma-Songwe njia 4 via EPC

Anajenga Barabara ya Njiapanda ya Iyula-Nyimbili-Katumba

Amekamilisha Daraja la Kulinganisha na Malawi Kasumulu na Sasa ujenzi wa Barabara ya lami Kutoka Kasumulu Hadi Ngana Kyela unaendelea

Anajenga hospital ya Rufaa ya Mkoa

Vwawa na Tunduma Zina miradi ya TACTIC nk.

Tabora
Anajenga Barabara ya Urambo-Kigoma kabla ya desemba utasafiri kutoka Dar Hadi Kigoma via Tabora Kwa lami.

Anapeleka maji Sikonge na Igunga kutoka Ziwa Victoria , wakandarasi wako site Kupitia mradi wa Miji 28.

Mradi wa Tactic Tabora mjini

Anajenga skimu za umwagiliaji Nzega na Igunga.

Shinyanga.
Anajenga Shinyanga Airport

Tactic Kahama & Shy town

Ujenzi wa Dry Port Isaka via SGR

Amepeleka Tawi la Chuo Kikuu Cha Ardhi Shy Mjini via mradi wa Kupeleka vyuo vikuu kwenye Mikoa ambayo Haina(Najua hili hulijui).

Singida
Anajenga Barabara ya Singida-Manyara via Sibito River

Anajenga Barabara ya Singida-Kiteto

Anajenga Barabara ya Ndago

Anajenga Barabara ya Mkiwa-Itigi-Rungwa

Mradi wa Tactic Singida MC

Mwisho Kuna substation kubwa ya Umeme inajengwa Manyoni plus One stop Inspection Centre.

Kiufupi hakuna Mkoa ambako Rais Samia hajasambaza Upendo yaani watu wako Mikoa Yao harafu hawaelewi kinachofanyika ila rangi ya chupi za kina Lisu &Diamond wanazijua 😂😂
 
Kumbe unaongea Kwa maana ya miradi kwamba ndio kuwekeza nikajua wapi kuna Nguvu ya ccm.

Kwa taarifa Yako Rais hafanyi kazi kufurahisha Mikoa Bali Kwa faida ya Nchi.Mwanza Kuna miradi ambayo aliikuta ndio kwanza inaanza lazima imalizike kwanza ndio mengine yaanze ,stand zote 2 tayari,Daraja kinaisha desemba,Sgr labda 2026 ,mradi wa Maji Butimba olmost done ,uwanja wa ndege keshatoa pesa ujenzi unaanza maana ulisimama.Mwisho ameanza ujenzi wa Barabara ya lami kuanzia hapo Sengerema Hadi Nyehunge bila kusahau meli Mpya kibao huko,anajenga hospital kubwa ya Rufaa ya Mkoa Ukerewe na mengine mengi kama magorofa ya Watumishi hapo Ghana street nk.

Dodoma ni case Moja na Mwanza lazima miradi aliyoirithi ikamilike ambapo Sgr na station Tayari,Barabara za Mji Mkuu tayari, airport na ring road ndio zinaendelea, hospital ya Jeshi,Makao Makuu ya jeshi nk

Japo Kwa Dom Kuna miradi mipya imeanza ambayo ni ya Kitaifa na sio ya Dodoma mfano ujenzi wa Hospital kubwa ya kina Mama ,Ujenzi wa Bwawa la Farkwa,ujenzi wa Barabara za lami kuunganishwa na mvumi,kongwa nk bila kusahau ujenzi wa Makao Makuu ya Nchi unaendelea.

Kuhusu Mbeya naona unaongea pumba na kuleta chuki zako za kina Mwambukusi.Nchi haijawahi ishiwa mipango ,Kuna mipango Toka awamu ya Nyerere hata bwawa la umeme ni Mpango wa Mwalimu.Hivyo basi amekamilisha ujenzi wa uwanja wa Songwe Airport,kuanzia runway,taa Hadi passenger terminal na Sasa wanajenga cold room,amekamilisha hospital ya Rufaa-Meta.
Ujenzi Mpya ni Barabara ya Njia 4,Barabara ya igawa-Tunduma,Ujenzi wa mradi wa Maji wa mto kiwira na ujenzi wa jengo la magonjwa ya Moyo Rufaa Mbeya,ujenzi wa Barabara za lami Rungwe,Kyela na Busokelo nk.

Kuhusu Arusha ni kwamba mama amekamilosha ujenzi wa mradi wa Maji,amekamilisha ujenzi wa Barabara ya EAC ,ameanza ujenzi wa Barabara ya kijenge,Kilombero na ujenzi wa Barabara ya kutoka Arusha-Dodoma via Kiteto ila miradi ya size ya kati haihesabiki.

Kuhusu Dar hapo usiseme miradi haihesabiki, mengine chuki zinakusumbua [emoji16][emoji16]View attachment 2758968
Upo Deep sana mkuu
 
Back
Top Bottom