Hivi ni kwanini watu wengi wanaona aibu kuongeza chakula kwenye sherehe?

Hivi ni kwanini watu wengi wanaona aibu kuongeza chakula kwenye sherehe?

Hizi aibu zangu za kula shehereni zilinikosesha layer cream nikaishia kupata ukoko japo sikuula. Siku hizi sina aibu kula shereheni. Wakitangaza sasa ni wakati wa kula nawahi fasta mbele kuwahi vinono vingi vya mwanzo kabla ya wagawaji hawajapunguza mkono wa kugawa chakula. Wa mwishoni hupata kidogo au hukosa kabisa
😅😁😁hata ukiwa na boss unakimbilia mbeleni?
 
Ukitaka kuzoa fedheha, nenda na empted stomach kwenye sherehe za watu.
Shiba kwako kwanza ndiyo uende.
Njaa njaa hizi hupoteza usmart wa mtu.
Tena vyakula vyenyewe wanga mtupu, ya nini bhana?
Hakika mkuu japo waswahili wengi wanatakaga kwenda kushiba kwenye sherehe
 
Aibu yan kuongeza chakula ikiwa wao wenyewe wamesema tukaongeze ni aibu😀😀😀😀😀
Hamna aibu hapo.
Ishu ni kuwa tu mtu unaridhika na ulichopewa unaweza jikuta umepewa kidogo ukaridhika na ukashiba zako.
Kwenye kula hutakiwi kuwa na aibu kama hujashiba
 
Kujifunze kuridhika uepuke aibu ndogondogo kama hizo,kama unapenda msosi flani na kwenye sherehe umekula hujashiba cha kufanya tenga siku ambayo utakuwa nyumbani kwako kanunue Mazaga mwambie wife akupikie jipakulie kula tani yako sio kulialia kwenye shughuli za watu kwamba hujashiba.
 
Back
Top Bottom