Hizi ni stori za kwenye Biblia ambazo zimeniacha na maswali sana

Hizi ni stori za kwenye Biblia ambazo zimeniacha na maswali sana

Usinilazimishe niamini, umburula wako. Hakuna kitu ndani ya Biblia kisicho na majibu. Ila kama huamini,, hata ukielezwa hutakubal, chochote. Maana tayari umejenga mashtaka na kukataa.
Kaa kimya
 
Wewe ni msomaji mzuri wa biblia,ukitaka kuifaidi biblia isome kwa kujiuliza maswali,utafaidi

Swali hili la kwanza linajibiwa na uwepo wa Mungu katika utatu mtakatifu
Mungu baba,mwana na Roho mtakatifu.
Soma mwanzo 1:2b(Roho ya Mungu ikatulia juu ya maji)
Usihangaike kumjibu, mtu huyu hana nia kujifunza ila kashfa tu na matusi.
 
Kwani Wanyama wana Fanya vipi?,
Quran kariim imekataza zinaa, fanya ilo katazo halipo (assume) mimi/kidume chochote nakuja kwenu nagonga mlango una fungua nakwambia niitie mama yako, una fanya hvo ana Toka, naongea nae na kisha tunaingia chumbani kula Raha huku wewe uki shuhudia,
swali je utakubali huu mfumo wa maisha?,
Kwa taarifa yako watu wali ishi hv, na jamii nyingi zilikua potofo na watu wengi hawakupenda, uislamu ulipo simama na kusema (Quran kariim) zinaa ni haramu kila mtu alikubali bila ya mjadala papo hapo
Endelea na huo uelewa wako.
 
Anayenisaidia kuelewa Mambo ya Kiroho ni Roho Mtakatifu....!

Yote yaliwezekana baada ya kuacha kuufanya Moyo wangu kuwa Mgumu, nilifungua Moyo wangu, nikajikuta naanza kuelewa Mambo ya Ulimwengu wa Roho...!

Maisha yetu yanaanzia kwenye Ulimwengu wa Roho, kila kinachotokea kwenye Ulimwengu wa Mwili, kilianzia kwenye Ulimwengu wa Roho..!

Ndo maana Biblia inasema Kwa Wenye Akili (Wanaotumia Akili za Kibinadamu) habari ya Mungu kwao ni Upumbavu...!
Ni huyo huyo roho mtakatifu aliyekuwa anamuongoa nabii Dominik (kiboko ya wachawi) na akapata wafuasi wa kutosha.
 
Mimi ni mkristo na ninaamini Mungu yupo na anatenda. Ila kuna mambo ukisoma kwenye biblia lazima ujiulize maswali mengi sana yanayokosa majibu. Leo nitashea nanyi mambo ambayo naona kama yana ukakasi;

1. Kwenye Mwanzo 1:26 imeandikwa kuwa Mungu alisema tuumbe mtu kwa mfano wetu. Nimejiuliza ina maana uumbaji ulifanywa nae kwa kushirikiana na wengine? Hakuwa peke yake? Hao wengine kina nani?

2. Mwanzo 6 - 10 kuna stori maarufu ya Nuhu. Hii ni stori ina ukakasi zaidi. Nikiandika maswali yote niliyojiuliza uzi utakuwa mrefu. Ninashauri mkaisome ili tuifungulie uzi wake.

3. Kutoka 11:5-6 kuna maandiko yanayosema kuwa wazaliwa wa kwanza wote wa wamisri kwa upande wa binadamu hadi wanyama watauwawa na Mungu mwenyewe ili waisraeli wapewe ruhusa ya kwenda nchi ya ahadi. Kiukweli haya yalikuwa ni mauaji ya halaiki kwa wasio na hatia. Unaambiwa hadi mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, kuku, ng'ombe, mbwa na farasi waliuwawa. Kwanini isingetumika njia nyingine hao waisraeli wakaondoka?

4. Kitabu kizima cha Joshua kimejaa stori za mauaji matupu. Ikumbukwe Joshua alichukua nafasi ya Musa kwenye kuwaingiza waisraeli nchi ya ahadi baada ya kifo cha Musa. Nchi waliyoahidiwa ilikuwa tayari ina wakazi wake ambao ilibidi wauwawe wote ili kuwapisha waisraeli. Hivi ilishindikana vipi kufanya kama alivyofanya Mama Samia kuwatoa wamasai Ngorongoro na kuwapeleka Msomera kwa amani kabisa bila kumwaga damu? Kama leo 2024 bado kuna maeneo duniani hayajakaliwa na binadamu ilikuwaje enzi za Joshua? Ukisoma kitabu cha Joshua utaona kila sehemu waliyopita walikuwa wakiua wenyeji watakaowakuta. Kulikuwa na sababu zipi za msingi za mauaji haya yote?

5. Ayubu 1:6-12 utaona stori ya shetani alipojiunga na wana wa Mungu kupita mbele ya Mungu kumwabudu hadi Mungu akashangaa imekuwaje shetani akawa eneo lile? Baada ya hapo Mungu na Shetani wakakubaliana kwenda kumjaribu Ayubu kwa sharti la kutogusa mwili wa ajabu (kumuua). Katika yale majaribu watoto wa Ayubu waliuwawa na shetani. Naweza kusema ni mauaji yaliyokuwa na approval toka juu. Ilikuwa kazi maalum. Je, sio kwamba wawili hawa hukutana na kukubaliana baadhi ya mambo? Sio kwamba kuna kazi za shetani zina kibali maalum?
Sir100 amewatoa lini Kwa Amani wamasai Ngorongoro..... Hivi kwenu Amani ni kitu gani hasa hatuna Amani hapa tuna ujinga,ubwege,upumbavu na umbumbumbu uliokithiri basi hakuna Amani hii nchi.
 
Biblia ni hadithi za kimapokeo. Uongo mwingi na kinaonyesha waandishi wake wengi walikuwa na upeo mdogo wa dunia yetu.
Niambie kitabu tofauti cha KIROHO duniani kilicho Bora cha kweli kuliko Biblia. .
 
Niambie kitabu tofauti cha KIROHO duniani kilicho Bora cha kweli kuliko Biblia. .
Kuwa bora hakimaanishi yote yaliyoandikwa humo ni sahihi, hakimaanishi kimeandikwa chini ya usimamizi wa Mungu. Kiufupi ni masimulizi ya uhusiano wa watu wa wakati huo na utamaduni huo na huyo waliyemwamini kama Mungu wao. Kina mapungufu mengi sana na hakipaswi kuunganishwa na Mungu moja kwa moja. Kila utamaduni una hadithi zao dhidi ya Mungu wao.
 
Sawa, unapokikosoa kitabu cha Biblia, nipe kitabu cha KIROHO hapa duniani unachoona kina uhakika kuwa cha MUNGU tofauti na Biblia. Kama sivyo niendelee kuamini kuwa huna hoja
 
Sawa, unapokikosoa kitabu cha Biblia, nipe kitabu cha KIROHO hapa duniani unachoona kina uhakika kuwa cha MUNGU tofauti na Biblia. Kama sivyo niendelee kuamini kuwa huna hoja
Wewe endelea na imani yako, hiyo ni haki yako ya msingi. Wale wanaokosoa wasikupe shida hata kidogo. Ila jua kuwa unaweza ukamuamini na kumtii Mungu bila kupitia hicho kitabu chenu. Mungu alikuwepo hata kabla ya hiyo Biblia. Kuna Imani nyingi tu zisizotumia hiyo biblia na wako sahihi kabisa na wanaishi vizuri kweli kweli. Mwisho Mungu ni zaidi ya biblia na biblia ina mapungufu lukuki kwa sababu haikuandikwa na Mungu.
 
Kila mtu anajua kusoma kitabu cha mwenzake. Ziko kasoro za hovyo mpaka unashangaa kwenye hicho kitabu chako unachokificha kukitaja. Lakini hatuna muda kuzijadili maana waumini wake hawajui kujenga hoja, kuvumilia, zaidi ya vurugu, mapigano na muaji.
 
Biblia unaweza kuiweka katika namna mbili ,mja ni kitabu kianacho elezea historia ya wayahudi namna walivyokuwa wanaishi na Imani zao. Pili biblia ni kusanyiko la vitabu ambavyo vinatumika kama mwongoza kwa Imani Fulani namna ya kumwabudu Mungu wao
 
Kama kweli unataka kujua ilitakiwa umtafute anayejua akufundishe

Quran imeletwa Kwa lugha ya kiarabu na kiswahili ni mtoto wa lugha ya kiarabu Yani 95% ya misamiati ya kiswahili ni kiarabu hivyo kiswahili akina uwezo wa kutafsiri Kwa ufasaha lugha ya kiarabu

Ila maana halisi ya hiyo Aya ni hii yapa

Sema:Anayemfanyia uadui Jibrail(anajisumbua),hakika yeye(Jibrail) ameiteremsha (Qur’an) moyoni mwako,kwa idhni ya Mwenyeezi Mungu,inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake,na ni uongofu na bishara ya waumini”.

Lakini pia kama kweli unataka kujua nani aliyekuwa anamletea mtume Muhammad hiyo Quran mbona Aya nyingine zipo nyingi tu ambazo hazina lugha ngumu Kwa Nini usizisome hizo

Quran 16:102 -
Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu.
Sio asilimia ulizo taja ni iUongo
 
Kila mtu anajua kusoma kitabu cha mwenzake. Ziko kasoro za hovyo mpaka unashangaa kwenye hicho kitabu chako unachokificha kukitaja. Lakini hatuna muda kuzijadili maana waumini wake hawajui kujenga hoja, kuvumilia, zaidi ya vurugu, mapigano na muaji.
Mkuu, ubishani kwenye hivi vitabu mlivyoletewa ni upuuzi mkubwa sana. Siko kati ya hizo imani zenu 2, bahati nzuri nimevisoma vitabu vyenu vyote viwili. Vina mafundisho mazuri sana kumshape binadamu kwa maisha yake hapa duniani. Mimi nitaishia hapa
 
Back
Top Bottom