nina tatizo moja kubwa sana; mtu ninayemheshimu na kumtumainia sana huwa sina uwezo wa kuendelea kuwa mbele yake pale ninapoona kuna kisichokweli au kisichowezekana anakiongea mbele yangu......inanibidi nitoke tu kumpisha ili nisipate nafasi ya kumbishia au kuwasikia wanaombishia au kumkandia maana nakuwa kwenye wakati mgumu kuvumilia.
namheshimu na kumpenda mno mama samia kiukweli na nilijiandaa kikamilifu kumsikiliza mwanzo mwisho. zilipoanza habari za kumaliza ufugaji wa kuhamahama sijui, mara sijui viwanda, KUTOSHURUTISHA ulipaji kodi nikaona ohoooooo, imeshakuwa tabu sasa na nikaondoka tu eneo la tukio ili niendelee kumsapoti mama yangu kwakuwa maneno hayo nilishayasikia sana kipindi cha kikwete na magufuli na matokeo yake tuliyaona.......bado tupo mlemle na katika yale yale, M/Mungu msaidie mama yangu huyu, natamani aache alama ya kipekee km alivyo pekee katika nafasi ya uraisi kwa mwanamke!!!