Hussein Machozi: Nilitaka nimpige risasi Ruge, show nililipwa milioni 12 akanipa milioni 1 tu

Bony na kusaga walikuwa wanakuja kupiga mziki hapo Don bosco enzi hizo son bosco kunafanyika ma event
Mimi naona bony aliamua tu kukaa pembeni afanye mambo yake....bony ni brother mmoja yuko humble sana hapendi mkimki
Haya mambo ya unyonyaji kuwakandamiza wasanii yameanza zamani sana haya mambo yana ujanja ujanja sana
Hata wale kim&Boyz tena wao ndy walikuwa waanzilishi wanaanda matamsha Enzo hizo walikuwa wazushi sana

Ova
 
Hizo ni sababu za loosers.

Diamond hajawai kuwa chini ya ruge na alikuwa adui yake mkuu

Ila bado diamond alikuwa anaitwa kwenye shows za serikali nyingi sana
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… hapa diamondplatnumz ni mwamba anasimama mwenyewe.
 
Ndio siri ya utajiri hio, lazma utengeneze mazingira ya kunyonya kwa asilimia flani. Kama humnyonyi mtu maana yake unafanya kazi ya kumtawaza mbwa. Hakuna biashara bila faida. Ndio maana siku zote wenye roho nzuri hufa maskini.
 
Upanga ile waliyokuwa wanakaa wakina kibonde kulikuwa na watu fulani wajanja wamechangamka
Na walikuwa wana link na watoto kutoka kinondoni,obay nk
Ila wale watoto wa upanga Sea view walikuwa wanajitenga wakishuwa sana
Don bosco centre ile ilikuwa kama changanyikeni kuna ma event ,kuna michongo ya kwenda ulaya wewe tu na akili yako kujiongeza
Jack pemba mwenyewe alikuwa mtoto wa upanga kule,wakina kalikawe,wakina Bob fish nk
Kibonde upanga alikuwa maarufu sema alikuwa mtu wa kanisa unawajuwa tena mashahidi wa jehovah,kuna wakati nlikuwa nalala mpaka kwao dada zake wale wakina Lydia,Sarah yaani kama familia ilikuwa sema utata ukawa unakuja mambo ya kwenda kanisani
Wengine donbosco pale ilikuwa tuko kimichongo tu tunachunguliaaa
Ndy kama wakati ule ulisikia zile safari za summer camp kwenda usa idea ilipelekwa pale na watu wengi walichomoka kwa gea hyo

Ila kibonde alikuja tu badilika kawa mtu wa mtungi,madem kwa sana mm mwenyewe mtungi nishapiga naye sana

Ova
 
Sasa kama unapigiwa pande , hujui hizo hela mnagawana na wengine waliofanikisha pande hilo.

Hujui kama ni chain ndefu mpaka pande lifanikishwe.

Bado hujaweka Tax hapo na vibali vingine. Serikali haifanyi biashara na mtu ambaye halipi kodi.
Kikubwa ni kuwa Ruge alikuwa kama Plug ya serikali na wasanii. Ishu yeyote ya corporate inayohitaji tamasha na uhamasishaji ilikuwa inapitishwa clouds kwa Ruge.

Kiufupi serikali haifanyi kazi na mtu binafsi bali inafanya kazi na kampuni proper na clouds media group ni kampuni ambayo tayari ilikuwa kwenye peak, inaaminika na inafanya vizuri kwenye media industry kuliko kampuni zote zingine na walikuwa na lobbyist mzuri ambaye ndiye the late Ruge Mutahaba.

Clouds ilikuwa pia ina pooll ya wasanii sababu ndio ulikuwa mlango wa kuwafanya wasikike hewani. Kumbuka miaka hio hakukuwa na social media wala smartphones ambazo zilifanya accessibility ya nyimbo kwa general public kuwa limited.

Gameplan ilibadilika kuanzia 2009 baada ya ujio wa 3G internet bongo, google android, apple OS kila mtu akaanza race ya kumiliki smartphone, social media zikaanza ku take over anzia facebook, whatsapp, ikaja BBM, Twitter na muendelezo wake zikaja live streaming apps my space, itunes, deezer, youtube n.k.

Hapo sasa ile territory na monopoly ambayo Media nyingi kama Clouds zilijiwekea ikaanza kuwa weak. Diamond ndio alianza kwa kuvunja huo mwiko na kuanza kuwekeza kwenye social medias mpaka leo amefika alipo sababu ali take risk hiyo na imemlipa.
Hizo ni sababu za loosers.

Diamond hajawai kuwa chini ya ruge na alikuwa adui yake mkuu

Ila bado diamond alikuwa anaitwa kwenye shows za serikali nyingi sana
 
Kwahiyo ruge atakuwa alipigwa kipapai sio
Ruge hakupigwa kipapai ila tu Karma ilifika. Alikuwa na mrija wa noti so offer za chupi zilikuwa nyingi na ukiwa mtu wa sketi sana zama zile za giza kuikwaa ngwengwe ilikuwa kugusa tu.

Nafikiri alinasa kwa "Juliana" so katika kupambania kombe ndio ikafikia final stage akang'oka.
 
Yule juliana mwenye kuuza vilevi pale sinza au
 
Mkuu ndio ukweli ulivyo, tuko kwenye dunia ya kibepari ambapo ili upande lazma ukanyage mabega ya wengine. Ukikwepa huo mfumo huwezi sogea.

Serikalini fisadi ni mtu kama wewe ila tu ametanguliza interests zake mbele. Anataka Rollce Royce, Ghorofa Mbweni na Dubai. Ili afanikishe hayo lazma achepushe hela zza kujenga hospitali, barabara na shule kwa ajili ya wananchi wenzie ili azitumie kufanikisha mipango yake. Sio kwamba hajui ni makosa ila ni lazma afanikishe mipango yake. Hio ndio capitalism inavyofanya kazi.

Kwenye makampuni vile vile, bhakressa na Mo wanaingiza billions kwa siku ila kuna watu wanalipwa elfu 6/6 ili tu jamaa apate billions zake zikiwa kamili. Wanatengeneza substandard products zingine ambazo hata wao hawazitumii sababu zina madhara ila ni lazima waziuze ili billions zao ziingie. Hio ndio capitalism.


In short, Capitalism is the art of not giving a flying fucck about what other people think of you but the motive is to keep getting more out of their efforts.
 
Yule jamaa ndio maana zilikuwa haziivi na domomondi halafu wabongo wakamwona domo jau.
Diamond ni mtoto wa uswahilini ila naye ana strong Capitalist mindset kama ya RUGE japo yeye yuko fair. Nachoona aliusoma mchezo mapema akapata washauri wazuri akaamua kuinvest kwenye kujenga brand in full margin.

Diamond sio mtu ambaye anaweza akakudhulumu chako straight to your face kama ilivyokuwa kwa Ruge. Angekuwa hivyo tayari watu wangekuwa washajua roho mbaya haijifichagi.

Nafikiri ndio maana Kusaga alivutiwa kumchukua kufanya nae kazi. It has payed him alot so far. Diamond amekula share ya 45% sababu ni brand name yake inatumika. Hicho anachokiingiza kupitia wasafi radio hata asipofanya show anaishi tu.
 
Bonny na Kusaga wako pamoja hata kabla ya literally uchumi, toka mwenge kijijini walikuwa pamoja
 
Aweke ushahidi hapa kwamba alirudisha pesa zote milioni 12.

Atakuwa mtanzania wa kwanza tangu nimepata ufahamu kuhusu pesa.

Watu wengi hawaelewi somo la "Price and Cost".

Kuna kitu kinaitwa "Total Landed Costs". Gharama ya mwisho baada ya kutoa kila kitu.

Inawezekana kabisa kwamba muandaa show kuna gharama kazibeba kama kuandaa jukwaa, kulipa kodi, kulipa gharama za vinywaji kwa wasanii, usafiri wa wasanii, malazi ya wasanii, umeme, kukodi magari na mafita na vingine vingi.

Akikulipa wewe msanii pesa zote gharama alizoingia yeye atalipa nani?
 
Hii inajulikana mbona

Marehemu alikua dhuluma sana
 
Na wewe utakuwa dizaini yao hao madhulumati. Inakuingia akilini kweli msanii mmoja aliyekuingizia 12m yeye aambulie 1m kwa madai kwamba 11m zote ni gharama ulizotumia? Na hapo siyo kwamba Machozi alikuwa pekee yake kwenye show. Chukulia kwa mfano walikuwa wasanii 20 na kila mmoja aingize 12m jumla 240m. Halafu wewe uwagawie 24m na kudai gharama ulizotumia kwao ni 216m! Nonsense.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…