Hussein Machozi: Nilitaka nimpige risasi Ruge, show nililipwa milioni 12 akanipa milioni 1 tu

Hussein machozi na bastola wapi na wapi.......nani ana shida nae, amvamie ili apate nini.........huyu alikuwa msanii wa kawaida mno....hata Aslay alikuwa juu yake.
Machozi ambaye nasikia ameolewa italy amepata lini hata ziada ya kumiliki silaa

Mnahangaika na mtu anayeongea uwongo mweupee kabisa.
Yaani wewe umelipwa 12 milioni..Zipo mfukoni tayari...kulipa au kutolipa kupo ndani ya utashi wako...

Hivi ni mjinga gani alipe fedha yote halafu abaki mtupu.....Kwani angegoma Ruge angemfanya nini...hakuna ushahidi hakuna contract.
Sio kweli.
 
Na kwa hiyo miaka ilikuwa ni vigumu Sana kwa msanii kama Machozi kulipwa million 12 kwa show moja. Huu ni uongo na kwa nature ya wasanii wa bongo ilikuwa na haiwezekani kurudisha hiyo pesa wangeuana siku hiyohiyo tu. Machozi kumiliki bastola kama ni kweli basi mamlaka zimhoji aliitoa wapi maana sifikirii kama alikuwa nayo kihalali.
 
Nisingempa hiyo hela abadani
Kwenye bizz middle man anaweza kupiga Hela nyingi kuliko wewe mwenye ujuzi au mali.

Mfano Kuna jamaa nilifanya nae deal Kuna dawa Fulani nimuuzie Mimi sina nikacheki na mdau wangu mmoja akanipa mzigo kwa maneno nikauza nikiwa nimeweka Cha juu yule jamaa alie nipa deal nae kaweka Cha juu...

So Mimi nikapata 300k jamaa akapata 700k pesa yoteee nikawa nayo Mimi so Mimi nikampa middle man 700k kiroho safi kwenye bizz sometimes huwa TUKAKUBALI HATA IYO FAIDA NDOGO MAANA UNAKUTA NI CHAIN..
 
Nakuelewa sana na biashara ni Imani hata mi kariakoo nimefanya sana ila sio kiwango Cha 12-1 hapo kama Ruge achukue 7 mi 4 sawa maana huenda nae Kuna wale atawapoza kupata deal zingine ila 01 hapana
 
Nakuelewa sana na biashara ni Imani hata mi kariakoo nimefanya sana ila sio kiwango Cha 12-1 hapo kama Ruge achukue 7 mi 4 sawa maana huenda nae Kuna wale atawapoza kupata deal zingine ila 01 hapana
Roma mkatoliki Kuna stanza aliwai kusema..

Unaikataa LAKI YA SHOW ( SHOW YA LAKI MOJA) Mwenzako wanaifuata show ya LAKI MOJA KWA KUPANDA BASI mtu ana kwea Basi kuifuata LAKI MOJA MKOA.

MKUU UNACHUKUA TU HATA LAKI 5 SIO MBAYA MAANA ULIKUA HUNA 😂😅😁
 
jina lake anaitwa machozi,lazma aambulie machozi
 
Ruge alikuwa dhulumati sana kmmk wasanii wengi wanajua hilo.

Ndio maana alikufa kifo cha maumivu sana ARV zilidunda.

Hili liwe fundisho kwa wadhulumati wengine mamaé zao
​
Wala siyo ARV zilizodunda, aligusa pabaya tu.
Shiteba Mkolomije anajua kwa kina.
 
Kwangu. mbona ni kama hai make sense.Kwamba show alienda kumuomba Ruge,hivyo Ruge ndiye alikuwa Msimamizi /anayetambulika na Wenye shughuli,sasa iweje tena pesa akalipwa Msanii moja kwa moja?na kama kazi walifanya Wasanii zaidi ya mmoja ni vipi alijiridhisha kuwa yeye alistahili kulipwa kiasi hicho chote? Mwaka 2015 alikuwa mkubwa kiasi gani kulipwa kiasi hicho kwa show?Wenzake walilipwa ngapi ngapi?Kwa Mtu aliyefikia hatua ya kutaka kutumia bastola ni rahisi vipi kuambiwa arudishe pesa aliyokwishaiweka kibindoni na akatii?.Nahisi huyu angezima simu kama sio na kubadili kabisa line.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…