Hussein Machozi: Nilitaka nimpige risasi Ruge, show nililipwa milioni 12 akanipa milioni 1 tu

Hussein Machozi: Nilitaka nimpige risasi Ruge, show nililipwa milioni 12 akanipa milioni 1 tu

Aweke ushahidi hapa kwamba alirudisha pesa zote milioni 12.

Atakuwa mtanzania wa kwanza tangu nimepata ufahamu kuhusu pesa.

Watu wengi hawaelewi somo la "Price and Cost".

Kuna kitu kinaitwa "Total Landed Costs". Gharama ya mwisho baada ya kutoa kila kitu.

Inawezekana kabisa kwamba muandaa show kuna gharama kazibeba kama kuandaa jukwaa, kulipa kodi, kulipa gharama za vinywaji kwa wasanii, usafiri wa wasanii, malazi ya wasanii, umeme, kukodi magari na mafita na vingine vingi.

Akikulipa wewe msanii pesa zote gharama alizoingia yeye atalipa nani?

mkuu na hapo usikute huko serikalini alikopewa hiyo tenda pia watu wanataka na percent yao.
 
Ndio siri ya utajiri hio, lazma utengeneze mazingira ya kunyonya kwa asilimia flani. Kama humnyonyi mtu maana yake unafanya kazi ya kumtawaza mbwa. Hakuna biashara bila faida. Ndio maana siku zote wenye roho nzuri hufa maskini.

Walikuwa wakiwanyonya wasanii wanaenda kusambaza Ngwengwe

Mwisho ngwengwe inakuua ,

Ukiwa Exploiter in capitalism system you need to be smart sio unakuwa Kama Ruge.
 
Muda mwingine wasanii hawana umoja

Mfano kitendo cha kukubali kufanya prostitution business chini ya Ruge huo ulikuwa utoto mkubwa .



Msanii Kama diamond anachofanya au nandi ndo ilibidi wafaye wasanii wote kuandaa matamasha yao
 
Kuna siku mwaka 2011 nilibadili fikra zangu kuhusu vipato vya wanamuziki. Nikiwa nafanya kazi kwenye kituo fulani cha redio Arusha, DJ wetu akawapigia simu kundi zima la Tiptop kuwaambia kuhusu show ambayo redio yetu inataka kuandaa. Kupitia Madee walijibu kuwa wanataka Tsh 1.5m, usafiri wa basi Dar - Arusha, malazi na msosi kwenye hotel nzuri. Nilishangaa sana kundi lote kuhitaji kiasi kidogo kama hicho. Diamond yeye alivyopigiwa alihitaji Tsh 8m, usafiri wa ndege Dar - Arusha wa yeye na madansa wawili pamoja, malazi na msosi.
Ni noma
 
Na wewe utakuwa dizaini yao hao madhulumati. Inakuingia akilini kweli msanii mmoja aliyekuingizia 12m yeye aambulie 1m kwa madai kwamba 11m zote ni gharama ulizotumia? Na hapo siyo kwamba Machozi alikuwa pekee yake kwenye show. Chukulia kwa mfano walikuwa wasanii 20 na kila mmoja aingize 12m jumla 240m. Halafu wewe uwagawie 24m na kudai gharama ulizotumia kwao ni 216m! Nonsense.
Upigaji wa hali ya juu😂
 
Kibonde hajawahi kuwa na nyumba. Baba yake alijenga ghorofa kule Mbeze Beach.

Baada ya Kibonde kufukuzwa kwa wakwe ikabidi ndio ahahime nyumba ya juu kwenye ghorofa la baba yake yeye na watoto wake
​
So hela alikuwa akipeleka wapi?
 
Leo yeye anakula maisha 🇮🇹, huku Ruge akiwa udongoni huko bukoba. 😢😢😢😢
 
Back
Top Bottom