Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

Another foolish rhetoric, masikini jamii forums inatufanya tuingie tukikosa la kufanya
Mtu Kama thaatlaa either kwa makusudi au ndio kazi maalumu aliyo pewa kuifanya na anatakiwa kuripoti kwa wakuu wake wa kazi.

Kujivika upofu kwa wadau na kutotaka kurekebishwa kwa yaliyopo na yanayo pigiwa kelele ni kwa maslahi ya viongozi wa CCM na Rais aliyepo madarakani.

Kwa Wana mabadiliko/mageuzi tunaona kwa tume hii na Sheria hizi za UCHAGUZI hazitoi usawa Kati ya Chama Dola vs vyawa pinzani ni muda Sasa kelele za umma kutoka pande zoteee zipigwe ipasavyo mpaka serikali isikie na kufanya mabadiliko kwenye muundo wa tume na Sheria za UCHAGUZI.
 
Maji, elimu, afya kote huko mmefeli, wananchi tumewachoka hatuwataki
sasa gentleman,
kama umechoka kupatiwa mahitaji yako ya msingi ya kila siku uloyaainisha mwenyewe hapo juu,

kuna kitu kingine unaweza kweli na ulivyo mvivu hivyo? :pulpTRAVOLTA:
 
Mtu Kama thaatlaa either kwa makusudi au ndio kazi maalumu aliyo pewa kuifanya na anatakiwa kuripoti kwa wakuu wake wa kazi.

Kujivika upofu kwa wadau na kutotaka kurekebishwa kwa yaliyopo na yanayo pigiwa kelele ni kwa maslahi ya viongozi wa CCM na Rais aliyepo madarakani.

Kwa Wana mabadiliko/mageuzi tunaona kwa tume hii na Sheria hizi za UCHAGUZI hazitoi usawa Kati ya Chama Dola vs vyawa pinzani ni muda Sasa kelele za umma kutoka pande zoteee zipigwe ipasavyo mpaka serikali isikie na kufanya mabadiliko kwenye muundo wa tume na Sheria za UCHAGUZI.
Ukiona jamii zina ukatili wa kutisha ni kwa sababu ya watu kama hawa, wanajua wanachofanya na wako tayari kusaliti ustawi wa taifa kwa maslahi yao
 
Mgombea binafsi itatuletea powerful individuals who together with their friends and relatives will rule everything.
 
Chama Cha Mapinduzi is still a powerful institution in this country helping us to avoid State Capture by Powerful Individuals of any sort. Having a Commander in Chief who have no one to listen except security chiefs will be more dangerous than the current situation.
Voters are emotional by 75%. They can bring you "usiyemtaka kaja."
Voters cannot conduct vetting of individuals seeking their votes.
 
JEURI YA CHAMA DOLA KONGWE TAWALA CCM YENYE BUNGE NA SERIKALI ISIYO HESHIMU HUKUMU JUU YA MFUMO WA UCHAGUZI



Kutoka maktaba:

13 JUNE 2023

Mahakama ya Afrika yaiagiza Tanzania kufanya marekebisho ya sheria inayowapa mamlaka Wakurugenzi wa Halmashauri kusimamia uchaguzi​

Hukumu iliyotolewa katika uamuzi Leo ni kuhusu kesi iliyofunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inapinga Vifungu vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambavyo vinaruhusu wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi, ikidiwa kuwa 'makada wa Chama Cha Mapinduzi' ambacho ni chama tawala hivyo mpeleka maombi anadai kuwa ni vigumu uchaguzi kuwa wa huru na wa haki, lakini pia inadaiwa kuwa vifungu hivyo vinakiuka haki ya usawa mbele ya sheria ikiwa ni pamoja na haki ya wananchi kuchagua viongozi wao wanaowataka kwa uhuru.

UPDATES:
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imeagiza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho ya sheria ya Taifa ya uchaguzi inayotoa uhalali kwa Wakurugenzi (DED) kusimamia uchaguzi.

Uamuzi huo umetolewa kufuatia kutupilia mbali kwa mara nyingine ushahidi wa upande wa Serikali kwenye ile kesi ya kupinga hiyo.

Kufuatia maelekezo hayo mahakama hiyo imeielekeza Serikali ndani miezi 12 kupeleka ripoti ya utekelezaji wa uamuzi huo.

Ikumbukwe Kesi hiyo ambayo uamuzi wake umetolewa leo June 13, 2023, ilifunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inapinga Vifungu vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambavyo vinaruhusu wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi,

Ambapo mlalakaji alidai kuwa Wakurugenzi hao ni 'makada wa Chama Cha Mapinduzi' ambacho ni chama tawala hivyo kumpelekea uchaguzi kushindwa kuwa wa huru na wa haki. Lakini pia inadaiwa kuwa vifungu hivyo vinakiuka haki ya usawa mbele ya sheria ikiwa ni pamoja na haki ya wananchi kuchagua viongozi wao wanaowataka kwa uhuru.

Inaweza kukumbukwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 baadhi ya wadau hususani wanasiasa wa vyama vya upinzani Tanzania na Wanaharakati walikosoa vipengere hivyo vinavyotoa mamlaka kwa Wakurugenzi kusimamia uchaguzi, wakitaja Wakurugenzi hao waliokuwa na dhamana kuwa ni makada wa Chama tawala hivyo ilikuwa ni vigumu kwao kusimamia misingi na taratibu za uchaguzi licha ya baadhi ya wengine kuwa na mtazamo tofauti.

Akizungumza kuhusu kesi hiyo mara baada ya uamuzi,Wakili wa upande wa mleta maombi, Jebra Kambole amesema kuwa walichukua uamuzi wa kufungua shauri hilo wakiamini wanaweza kupata haki licha ya kushindwa kwenye mahakama ya rufaa.

“Baada ya kushindwa hiyo kesi mahakama ya Rufaa tuliamini kuna haki zetu hazijawa sawa kwahiyo tukapeleka kesi kwenye mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kwamba vile vifungu vinavyotoa mamlaka kwa wakurugenzi (DED) vinakiuka mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu”amesema Wakili Jebra Kambore

Ameongeza kuwa “Mahakama imekubaliana na sisi kuwa sheria haijaweka vigezo vya Wakurugenzi hao kusimamia uchaguzi, mahakama imeona kuwa kutokana na kutokuwepo kwa vigezo ni kwamba mtu yoyote anaweza kusimamia uchaguzi. Mahakama imesema Wakurugenzi wasisimamie uchaguzi"

Ikumbukwe Kesi hiyo ambayo uamuzi wake umetolewa leo June 13, 2023, ilifunguliwa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inapinga Vifungu vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambavyo vinaruhusu wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Ambapo mlalakaji alidai kuwa Wakurugenzi hao ni 'makada wa Chama Cha Mapinduzi' ambacho ni chama tawala hivyo kumpelekea uchaguzi kushindwa kuwa wa huru na wa haki. Lakini pia inadaiwa kuwa vifungu hivyo vinakiuka haki ya usawa mbele ya sheria ikiwa ni pamoja na haki ya wananchi kuchagua viongozi wao wanaowataka kwa uhuru.

Inaweza kukumbukwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 baadhi ya wadau hususani wanasiasa wa vyama vya upinzani Tanzania na Wanaharakati walikosoa vipengere hivyo vinavyotoa mamlaka kwa Wakurugenzi kusimamia uchaguzi, wakitaja Wakurugenzi hao waliokuwa na dhamana kuwa ni makada wa Chama tawala hivyo ilikuwa ni vigumu kwao kusimamia misingi na taratibu za uchaguzi licha ya baadhi ya wengine kuwa na mtazamo tofauti.

images%20(8).jpg



Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu imepiga marufuku Wakurugenzi kusimamia chaguzi, yaagiza serikali kufanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi na kupeleka ripoti ya utekelezaji wa marekebisho hayo ndani ya miezi 12.

Mahakama ya Afrika.jpg

Kesi hii ilifunguliwa na mwanasheria Bob Wangwe kupinga wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mtaa kusimamia uchaguzi. Itakumbwa kuwa hii ni mara ya pili kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kupigwa marufuku kusimamia uchaguzi mbali na uamuzi wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania iliyoamua kuwa waendelee kusimamia chaguzi kwa sababu wanakula viapo vya kukana uanachama wao wa vyama vya siasa kabla ya kusimamia chaguzi.
 
Mifano ya tume za nchi kadhaa ikiwemo India, Liberia, Mozambique na The Gambia

TOKA MAKTABA :
15 December 2023

Deus Kibamba Aibua Mazito Mswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Atoa Mapendekezo Haya


View: https://m.youtube.com/watch?v=z8MtfR1Ccd8

Atolea mifano ya tume za nchi kadhaa ikiwemo India, Liberia, Mozambique na The Gambia kulinganisha na muswada wetu wa Tanzania kama ulivyo hapa chini. Deus Kibamba anashauri Tume ya Uchaguzi lazima iwe na muonekano kamili yaani Kichwa, Shingo na Kiwillkiwili siyo kama ulivyoanishwa katika muswada huu hapa chini uliowakilishwa na serikali bungeni :

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

No. 12 19th October, 2023
SPECIAL BILL SUPPLEMENT

To The Special Gazette of the United Republic of Tanzania No. 43 Vol. 104 Dated 19th October, 2023
Click to expand...
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023


MUSWADA WA SHERIA YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WA
MWAKA 2023
MPANGILIO WA VIFUNGU
Kifungu Jina

SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA UTANGULIZI

1. Jina na tarehe ya kuanza kutumika.
2. Matumizi.
3. Tafsiri.
SEHEMU YA PILI
KUANZISHWA, MUUNDO NA MAJUKUMU YA TUME YA TAIFA
YA UCHAGUZI
4. Kuanzishwa kwa Tume.
5. Muundo wa Tume.
6. Hadhi ya Tume.
7. Sifa za wajumbe wa Tume.
8. Muda wa utumishi wa wajumbe.
9. Kamati ya Usaili.
10. Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume.
11. Majukumu ya Tume.
12. Maadili katika utendaji kwa wajumbe.
13. Vikao vya Tume.
14. Akidi katika vikao vya Tume.
15. Uamuzi wa Tume.
16. Posho na stahili za wajumbe wa Tume.
17. Uhusiano kati ya Tume na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
/ISSN 0856 – 0331X

Page 1

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
2

SEHEMU YA TATU
SEKRETARIETI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


18. Mkurugenzi wa Uchaguzi.
19. Maadili ya utendaji kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
20. Majukumu ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.
21. Watumishi na watendaji wa Tume.

SEHEMU YA NNE
MASHARTI YA FEDHA


22. Fedha za uendeshaji wa Tume.
23. Muundo wa Utumishi wa Sekretarieti ya Tume.
24. Gharama kulipwa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.
25. Hesabu na ukaguzi.
26. Taarifa ya mwaka.

SEHEMU YA TANO
MASHARTI MENGINEYO

27. Kanuni na miongozo.
28. Masharti ya mpito.

Page 2

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023

______
NOTISI
______
Muswada huu utakaowasilishwa Bungeni unachapishwa kwa ajili ya kutoa
taarifa kwa umma pamoja na maelezo ya madhumuni na sababu zake.

Dodoma, MOSES M. KUSILUKA,
18 Oktoba, 2023 Katibu wa Baraza la Mawaziri
Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubainisha muundo, majukumu, utaratibu wa upatikanaji wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na sifa za Mkurugenzi wa Uchaguzi, kuweka utaratibu wa uendeshaji wa vikao vya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na
kuweka masuala mengine yanayohusiana nayo.

IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA UTANGULIZI

Jina na tarehe
ya kuanza
kutumika
1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ya mwaka, 2023 na itaanza kutumika
katika tarehe ambayo Waziri atateua kwa notisi katika
Gazeti la Serikali.
Matumizi 2. Sheria hii itatumika Tanzania Bara na Tanzania
Zanzibar, isipokuwa kwa masuala yanayohusu uchaguzi wa
Madiwani, itatumika Tanzania Bara.
Tafsiri 3. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha
utahitaji vinginevyo-
“jimbo” maana yake ni jimbo la uchaguzi kwa madhumuni

Page 3

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
4
ya uchaguzi wa Wabunge;
Sura ya 2 “Katiba” maana yake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977;
“Mjumbe” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuwa mjumbe
wa Tume kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba;
“Mkurugenzi wa Uchaguzi” maana yake ni mtu aliyeteuliwa
kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa mujibu wa
masharti ya kifungu cha 18 na itajumuisha mtu
ambaye kwa kipindi hicho atakuwa anatekeleza
majukumu yoyote ya ofisi hiyo;
“Mwenyekiti” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuongoza
Tume na inajumuisha Makamu Mwenyekiti;
“Rais” maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania;
“Tume” maana yake ni Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya
74(1) ya Katiba;
“uchaguzi” maana yake ni uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani na inajumuisha uchaguzi mdogo wa
Mbunge au Diwani;
“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na
masuala ya uchaguzi.

SEHEMU YA PILI
KUANZISHWA, MUUNDO NA MAJUKUMU YA TUME YA TAIFA
YA UCHAGUZI


Kuanzishwa
kwa Tume
4. Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya
Katiba ambayo pia itajulikana kama “Tume ya Taifa ya
Uchaguzi”.
Muundo wa
Tume
5.-(1) Tume itakuwa na Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine watano watakaoteuliwa
na Rais.
(2) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi watashika madaraka mara
baada ya kuapishwa na Rais.
(3) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu

Page 4

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
5
wa Tume utafanywa kwa misingi kwamba, endapo
Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri
ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka
upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Katibu na
Mtendaji Mkuu wa Tume.
Hadhi ya
Tume
6.-(1) Tume itakuwa ni chombo huru na
kinachojitegemea na maamuzi yake hayataingiliwa na
chombo chochote au kulazimika kufuata maagizo ya mtu
yeyote au Idara yoyote ya Serikali au maoni ya chama
chochote cha siasa.
(2) Tume itakuwa ni chombo chenye uwezo wa
kumiliki mali na kuwa na nembo na lakiri yake, na kwa jina
lake Tume inaweza-
(a) kujipatia na kumiliki mali zinazoweza
kuhamishika na zisizoweza kuhamishika;
(b) kushtaki au kushtakiwa; na
(c) kufanya au kutekeleza mambo yote au masuala
mengine yoyote ambayo yanaweza kufanywa au
kutekelezwa na chombo huru.
Sura ya 5
(3) Pale ambapo Tume itakuwa imeshtaki au
kushtakiwa, itapaswa kumtaarifu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ili awe sehemu ya shauri hilo kwa lengo la kukidhi
masharti ya Sheria ya Uendeshaji wa Mashauri dhidi ya
Serikali.
Sifa za
wajumbe wa
Tume
7.-(1) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume
watapaswa kuwa ni Majaji wa Mahakama Kuu au
Mahakama ya Rufani au kuwa na sifa ya kuwa Wakili na
amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi
na tano.
(2) Wajumbe wengine watano watakuwa na sifa
zifuatazo:
(a) awe raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano
kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Tanzania;
(b) awe mtu mwaminifu na mwadilifu;
(c) awe na uzoefu katika uongozi, utawala au masuala
ya uchaguzi; na
(d) sifa nyingine ambayo Kamati ya Usaili itaona inafaa

Page 5

. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
6
au ni muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya
Tume.
Muda wa
utumishi wa
wajumbe
8.-(1) Mjumbe wa Tume atashika nafasi ya madaraka
kwa kipindi cha miaka mitano.
(2) Mjumbe wa Tume atakoma kuwa Mjumbe
endapo litatokea lolote kati ya mambo yafuatayo:
(a) ukimalizika muda wa miaka mitano tangu
alipoteuliwa;
(b) ikiwa atafariki;
(c) endapo atajiuzulu;
(d) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama
asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya
asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume; au
(e) ikiwa ataondolewa madarakani na Rais kutokana
na-
(i) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza
majukumu yake kwa sababu ya maradhi
au sababu nyingine yoyote;
(ii) tabia mbaya; au
(iii) kupoteza sifa ya kuteuliwa kuwa
mjumbe.
(3) Endapo suala la kumuondoa Mjumbe wa Tume
litajitokeza, Rais anaweza kuunda Kamati itakayofanya
uchunguzi na kumshauri ipasavyo.
(4) Kamati iliyorejewa chini ya kifungu kidogo cha
(3) itajumuisha wajumbe wafuatao:
(a) Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye atakuwa
Mwenyekiti;
(b) Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora;
(c) Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma;
(d) Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa
Umma ya Zanzibar;
(e) wajumbe wawili wenye uzoefu wa masuala ya
uchaguzi, mmoja kutoka Tanzania Bara na
mwingine kutoka Zanzibar; na
(f) Mjumbe mmoja kadri Rais atakavyoona inafaa

Page 6

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
7
(5) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (4),
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi atateua mtumishi wa
umma mwandamizi kuwa Katibu wa Kamati.
(6) Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya
Uchunguzi itajiwekea utaratibu wa kujiendesha.
Kamati ya
Usaili
9.-(1) Wakati wowote inapobidi kuteuliwa mjumbe
au wajumbe wa Tume, Kamati ya Usaili itaitishwa.
(2) Kamati itakayoitishwa chini ya kifungu kidogo
cha (1) itakuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye
atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu
Mwenyekiti;
(c) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora; na
(d) mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais kwa
kuzingatia jinsia.
(3) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Katibu wa
Kamati ya Usaili.
(4) Wajumbe wa Kamati ya Usaili wataapa mbele ya
Rais kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao.
(5) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kuundwa,
Kamati ya Usaili itatoa tangazo kwa umma kupitia
magazeti angalau mawili yenye wigo mpana wa
usambazwaji nchini na vyombo vingine vya habari
kuwaalika wananchi wenye nia ya kuomba kuteuliwa kuwa
wajumbe wa Tume kuwasilisha maombi yao kwenye
Kamati.
(6) Kamati ya Usaili mara baada ya kupokea na
kuchambua maombi ya watu walioomba kuteuliwa kuwa
wajumbe wa Tume, itafanya usaili na kupendekeza kwa
Rais majina ya watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa
wajumbe wa Tume.
(7) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (6), utaratibu
wa kusimamia mchakato wa usaili utakuwa kama
utakavyoainishwa katika Kanuni.
(8) Kamati ya Usaili itawasilisha kwa Rais majina
manne zaidi ya idadi ya nafasi zinazohitajika kujazwa.
(9) Muda wa Kamati ya Usaili utakoma mara baada

Page 7

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
8
ya Rais kuteua wajumbe wa Tume.
Uteuzi wa
Mwenyekiti,
Makamu
Mwenyekiti
na wajumbe
wa Tume
10.-(1) Rais atateua Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti wa Tume kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya
74(1)(a) na (b) na (2) ya Katiba.
(2) Rais atateua Wajumbe wengine wa Tume kutoka
miongoni mwa majina yaliyowasilishwa na Kamati ya
Usaili.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe
wengine wa Tume wataapa mbele ya Rais kabla ya kuanza
kutekeleza majukumu yao.
Majukumu ya
Tume
11.-(1) Kwa kuzingatia matakwa ya Ibara za 74(6),
75 na 78 za Katiba, Tume itakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga
kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na Wabunge
katika Jamhuri ya Muungano na uchaguzi wa
Madiwani kwa Tanzania Bara;
(b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi
wa Rais na Wabunge na uchaguzi wa Madiwani
kwa Tanzania Bara;
(c) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya
Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya
uchaguzi wa Wabunge;
(d) kuteua na kuwatangaza Wabunge Wanawake wa
Viti Maalum katika Jamhuri ya Muungano na
Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kwa
Tanzania Bara;
(e) kuandaa na kusimamia Kanuni za Maadili ya
Uchaguzi;
(f) kutoa elimu ya mpiga kura nchini;
(g) kuratibu na kusimamia taasisi na asasi zinazotoa
elimu ya mpiga kura;
(h) kualika na kusajili watazamaji wa uchaguzi;
Sura ya 298
(i) kuajiri au kuteua watumishi na watendaji wa
Tume kwa kadri itakavyohitajika kwa kuzingatia
masharti ya Sheria ya Utumishi wa Umma na
masharti mengine yatakayowekwa na Tume; na
(j) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama
yalivyoainishwa kwenye Katiba au sheria

Page 8

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
9
nyingine yoyote.
(2) Tume inaweza kukasimu majukumu au sehemu ya
majukumu yake kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, mtumishi au
mtendaji mwingine wa Tume.

Maadili katika utendaji kwa
wajumbe Sura ya 398

12. Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu
ya Tume, kila Mjumbe wa Tume atalazimika kuzingatia
Sheria ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma na
Kanuni za Maadili zitakazoandaliwa chini ya Sheria hii.
Vikao vya
Tume
13.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 74(7) ya
Katiba, Tume itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu
utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao.
(2) Tume itakuwa na vikao vya kawaida visivyopungua
vinne kwa mwaka.
(3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (2),
Tume inaweza kufanya vikao maalumu muda wowote
itakapoonekana kuwa ni lazima kufanya hivyo.
(4) Tume itafanya vikao vyake katika sehemu na muda
utakaopangwa na Tume.
(5) Mwenyekiti atahakikisha kuwa kila mjumbe wa
Tume anapewa taarifa ya kikao mapema kabla ya kikao hicho
kufanyika.
(6) Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, Mwenyekiti
ataongoza vikao vyote vya Tume na endapo Mwenyekiti
hatakuwepo, Makamu Mwenyekiti ataongoza, au ikiwa wote
wawili hawapo, wajumbe waliopo wanaweza kumchagua
mjumbe mmoja miongoni mwao atakayekuwa mwenyekiti wa
muda wa kikao husika.
Akidi katika
vikao vya
Tume
14. Akidi ya kikao chochote cha Tume itakuwa si chini
ya wajumbe wanne.
Uamuzi wa
Tume
15.-(1) Uamuzi wa kikao chochote cha Tume utafikiwa
kwa kuungwa mkono na Wajumbe walio wengi.
(2) Pale ambapo katika kikao chochote cha Tume
italazimu uamuzi kufikiwa kwa kupigiwa kura, Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti au mwenyekiti wa muda atakayekuwa
anaongoza kikao atakuwa na kura ya turufu zaidi ya kura yake
ya kawaida inapotokea kulingana kwa kura zilizopigwa.

Page 9


Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
10
Posho na
stahili za
wajumbe wa
Tume
16.-(1) Wajumbe wa Tume watalipwa posho na
stahili nyingine kwa mujibu wa Sheria, kanuni, taratibu na
miongozo itakayotolewa na mamlaka husika.
(2) Wajumbe wa Tume watalipwa kiinua mgongo
baada ya kumaliza muda wa ujumbe wa Tume.

Uhusiano kati ya Tume na
Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar


17. Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 74(13) ya
Katiba, katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume
itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya
Tanzania Zanzibar.

SEHEMU YA TATU
SEKRETARIETI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Mkurugenzi wa Uchaguzi


18.-(1) Kutakuwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi

atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume.
(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa na sifa
zifuatazo:
Sura ya 357
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya
Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia
Tanzania;
(b) awe ni mtu mwaminifu na mwadilifu;
(c) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria; na
(d) awe afisa mwandamizi katika utumishi wa umma.
Maadili ya
utendaji kwa
Mkurugenzi
wa Uchaguzi
Sura ya 398
19. Mkurugenzi wa Uchaguzi ataapa mbele ya Rais
kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake na atalazimika
kuzingatia Sheria ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa
Umma na Kanuni za Maadili zitakazoandaliwa chini ya Sheria
hii.
Majukumu ya
Mkurugenzi
wa Uchaguzi
20.-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Mtendaji
Mkuu na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa majukumu ya
kila siku ya Tume.
(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Afisa Masuuli
wa Tume na atatekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia Sheria,
kanuni na taratibu za fedha.
(3) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), Mkurugenzi
wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yafuatayo:
(a) kuandaa na kuratibu vikao vya Tume;

Page 10

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
11
(b) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga
kura;
(c) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi;
(d) kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Tume katika
kutekeleza majukumu yake;
(e) kuandaa bajeti na kalenda ya shughuli za Tume;
(f) kuweka kumbukumbu za vikao vya Tume;
(g) kutayarisha nyaraka mbalimbali za Tume;
(h) kushirikiana na taasisi za ndani na nje ya nchi
ambazo zinafanya kazi zinazohusu uchaguzi,
demokrasia na utawala bora;
(i) kusimamia miongozo kwa watendaji wa uchaguzi
katika kutekeleza majukumu yao kama
itakavyoagizwa na Tume;
(j) kusimamia rasilimali watu na mali za Tume;
(k) kufanya tafiti zinazohusiana na uchaguzi; na
(l) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama
atakavyoagizwa na Tume kwa mujibu wa Sheria
hii.
(4) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu
yake kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni watumishi wa
umma au watu wengine wenye sifa kwa kadri
itakavyohitajika.
Watumishi na
watendaji wa
Tume
21.-(1) Kwa madhumuni ya Sheria hii, mtumishi
aliyeajiriwa, aliyeteuliwa au aliyeazimwa na Tume, kwa
kipindi chote atakachokuwa anatekeleza majukumu ya
Tume, atachukuliwa kuwa ni mtumishi wa Tume na
atatakiwa kuzingatia Katiba, Sheria hii, Sheria ya Uchaguzi
wa Rais, Wabunge na Madiwani na sheria nyingine yoyote
inayohusu utekelezaji wa majukumu ya Tume.
(2) Mtu yeyote aliyeajiriwa kwa madhumuni ya
kutekeleza majukumu ya Tume, ikiwa hajaajiriwa katika
utumishi wa umma, atapokea malipo yanayostahili kwa
kazi hiyo kadri Tume itakavyoona inafaa kuidhinisha.

Page 11


Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
12

SEHEMU YA NNE MASHARTI YA FEDHA
Fedha za
uendeshaji
wa Tume

22. Fedha za uendeshaji wa shughuli za Tume zitatoka katika bajeti ya Serikali. Muundo wa Utumishi wa Sekretarieti ya Tume

23. Tume kwa kushauriana na Waziri mwenye
dhamana na masuala ya utumishi, itaandaa Muundo wa
Utumishi wa Sekretarieti ya Tume.
Gharama
kulipwa
kutoka
Mfuko Mkuu
wa Hazina ya
Serikali
24. Gharama zote-
(a) zilizotumika katika kuandaa daftari, kutoa kadi ya
mpiga kura na kufanya mambo mengine au vitu
vingine vinavyohitajika kufanywa kwa
madhumuni ya kutekeleza masharti ya Sheria hii;
(b) zilizotumiwa na Tume, Mkurugenzi wa
Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na mtu
mwingine yeyote aliyeajiriwa kutekeleza
majukumu ya uchaguzi;
(c) zilizotumika kwa ajili ya malipo ya maafisa
walioainishwa katika kifungu cha 21(2); na
(d) zilizotumika kwa ajili ya malipo kwa afisa yeyote
wa umma kuhusu shughuli rasmi zinazohusiana
au zinazotokana na uchaguzi,
zitatozwa na kulipwa kutoka kwenye Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali.
Hesabu na
ukaguzi
Sura ya 348
25.-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatunza vitabu vya
hesabu na kumbukumbu nyingine zinazohusiana na
shughuli za Tume na kuandaa taarifa ya hesabu ya mwaka
kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma.
(2) Hesabu za Tume zitakaguliwa na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Taarifa ya
mwaka
26.-(1) Ndani ya miezi mitatu baada ya kuisha kwa
mwaka wa fedha, Tume itaandaa taarifa ya mwaka
kuhusiana na mwaka wa fedha uliopita na kuwasilisha
taarifa hiyo kwa Waziri ambaye ataiwasilisha Bungeni.
(2) Taarifa ya mwaka itajumuisha-
(a) maelezo ya kina kuhusu utendaji wa Tume kwa

Page 12


Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
13
mwaka husika;
(b) nakala ya hesabu za Tume zilizokaguliwa pamoja
na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali; na
(c) taarifa nyingine yoyote ambayo Tume itahitajika
kutoa chini ya Sheria hii.

SEHEMU YA TANO
MASHARTI MENGINEYO

Kanuni na
miongozo
27. Tume inaweza kutengeneza kanuni na miongozo
na kutoa maelekezo kwa ajili ya utekelezaji bora wa
majukumu yake.
Masharti ya
mpito
28. Mara baada ya kuanza kutumika kwa Sheria hii,
mtu yeyote ambaye ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti
au mjumbe wa Tume ataendelea kushika madaraka hayo
hadi pale ujumbe wake utakapokoma.
________________
MADHUMUNI NA SABABU
_________________
Muswada huu unapendekeza kutungwa kwa Sheria ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ambayo pamoja na mambo mengine itaweka masharti na
utaratibu wa upatikanaji wa wajumbe wengine wa Tume waliotajwa katika
ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 tofauti
na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, itaainisha majukumu ya Tume
pamoja na taratibu nyingine za uendeshaji wa Tume.
Muswada huu umegawanyika katika Sehemu Tano.
Sehemu ya Kwanza ya Muswada inahusu masharti ya utangulizi ambayo
yanajumuisha jina la Sheria inayopendekezwa kutungwa, mawanda ya
matumizi, utaratibu wa kuanza kutumika pamoja na tafsiri ya misamiati
mbalimbali kwa kadri ilivyotumika ndani ya Sheria inayopendekezwa.
Sehemu ya Pili ya Muswada inahusu uanzishwaji wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi. Masharti mengine katika Sehemu hii ni pamoja na muundo wa

Page 13

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
14
Tume, majukumu, sifa za wajumbe wa Tume, muda wa utumishi wa
wajumbe, utaratibu wa vikao vya Tume, posho na stahili za wajumbe wa
Tume na uhusiano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume Uchaguzi
ya Zanzibar. Vilevile Sehemu hii inajumuisha pia masharti kuhusu uteuzi
wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine wa Tume.
Kwa mujibu wa Sehemu hii, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
watateuliwa na Rais kwa kuzingatia masharti yaliyopo katika ibara ya 74
ya Katiba. Uteuzi wa wajumbe wengine watano utahusisha Kamati ya
Usaili ambayo itapokea na kufanya uchambuzi wa maombi ya watu
wanaoomba kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume na kupendekeza majina
ya watu wenye sifa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi. Aidha, Sheria
inayopendekezwa inaweka utaratibu wa Rais kuweza kuunda Kamati ya
Uchunguzi, endapo ataona inafaa, ambayo itafanya uchunguzi na
kumshauri ipasavyo kuhusu kuondolewa kwa mjumbe wa Tume.
Sehemu ya Tatu ya Muswada inaweka masharti kuhusu Sekretarieti ya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo inajumuisha Mkurugenzi wa
Uchaguzi, watumishi na watendaji wengine wa Tume. Sehemu hii
inaainisha sifa za mtu kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi,
majukumu yake, muundo wa utumishi wa sekretarieti ya Tume pamoja na
kuweka takwa la kuzingatia Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma.
Miongoni mwa sifa zinazopendekezwa ili mtu aweze kuteuliwa kuwa
Mkurugenzi wa Uchaguzi ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania wa
kuzaliwa, mtumishi wa umma mwandamizi, mwaminifu na mwadilifu na
ambaye hajawahi kusika nafasi ya madaraka ya juu katika chama chochote
cha siasa. Sehemu hii inaweka pia masharti kwamba mtu yeyote ambaye
atakuwa anatekeleza majukumu ya Tume atachukuliwa kuwa mtumishi wa
Tume kwa kipindi chote atakachokuwa anatekeleza majukumu hayo na
atapaswa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utekelezaji wa
majukumu ya Tume.
Sehemu ya Nne ya Muswada inahusu masharti ya fedha ambayo
yanajumuisha vyanzo vya fedha za uendeshaji wa Tume, gharama za
uendeshaji wa shughuli za uchaguzi, ukaguzi wa hesabu na na uwasilishaji
wa taarifa za utendaji wa Tume Bungeni. Inapendekezwa kuwa chanzo cha
fedha za uendeshaji wa Tume kitokane na fedha zitakazoidhinishwa na
Bunge kupitia bajeti ya kila mwaka ya Serikali. Vilevile, kuhusu fedha
zitakazotumiwa na Tume katika uendeshaji wa shughuli za uchaguzi,
Sehemu hii inapendekeza kuwa fedha hizo zitoke katika Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali. Aidha, kama ilivyo kwa taasisi nyingine za umma

Page 14

Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
15
zinazoendeshwa kwa bajeti ya Serikali, hesabu za Tume zitakaguliwa na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Sehemu ya Tano ya Muswada inahusu masharti mengineyo. Ili
kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, inapendekezwa
kuipa Tume mamlaka ya kutengeneza kanuni, kuandaa miongozo na kutoa
maelekezo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji bora wa majukumu yake.
Sehemu hii pia inaweka masharti ya mpito kuhusiana na wajumbe wa
Tume ambao watakuwa madarakani wakati wa kuanza kutumika kwa
Sheria inayopendekezwa. Kwa mujibu wa masharti hayo, wajumbe hao
wataendelea kushika nafasi hizo hadi pale watakapoondolewa au muda
wao wa kuhudumu kuisha. Kwa mantiki hiyo, wajumbe wengine
watakaoteuliwa baada ya kuanza kutumika kwa Sheria inayopendekezwa
watateuliwa kwa kuzingatia utaratibu unaopendekezwa katika Muswada
huu.

Dodoma, KASSIM MAJALIWA MAJALIWA,
17 Oktoba, 2023 Waziri Mkuu

Page 15
MWISHO
..............................................................................

Kongamano la TLS juu ya Muswada wa Sheria za uchaguzi December 15, 2023​

Hayo yamejiri katika kongamano leo lililoangazia sheria ya uchaguzi n.k

A National Stakeholders' Engagement Conference on Election Laws and Political Parties Affairs Laws in Dar es Salaam , Tanzania on 15th December, 2023
 
Hivi haiwezekani kuupinga uchaguzi mkuu mahakamani hadi marekebisho ya sheria ya uchaguzi yafanyike na tume hurubiundwe?
Petro E. Mselewa
Pascal Mayalla
Kisheria inawezena,ila practicability it is impossible,utatakiwa,ku depost mahakamani,equivalent money ya budget ya maandalizi iliyokwisha kuwa spent kwenye maandalizi ili ukishindwa,hiye fedhaifidie!,nani anaweza ku afford?。 ndio maana nimemshauri TAL na Chadema, waache utopia wa no reforms,no election!。
P
 
TOKA MAKTABA: 2023
TUME YA UCHAGUZI ILIYOSIFIWA NA DEUS KIBAMBA

View: https://m.youtube.com/watch?v=z8MtfR1Ccd8...Atolea mifano ya tume za nchi kadhaa ikiwemo India, Liberia, Mozambique na The Gambia. Tume ya Mozambique ni nzuri kama ile Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar.... nguli huyo mchanganuzi asema...


UKWELI ULIOJIRI BAADAYE NCHINI MOZAMBIQUE
TOKA MAKTABA:
OCTOBER 2024 UCHAGUZI MKUU MSUMBIJI
Kigogo wa Tume ya Uchaguzi Mozambique ktk mahojiano exclusive - Mchakato na Uchaguzi uligubikwa na uchafuzi



View: https://m.youtube.com/watch?v=2B_xQtuZLW8

Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw. Fernando Mazanga asema uchafuzi wa uchaguzi na uchafuzi wa mchakato wa uchaguzi, Tume haiwezi kusema nani alishinda..

Kwanza kiukweli kulikuwa na Tume mbili zinazosimamia mchakato, moja ni Tume ya Uchaguzi halisi isiyo na meno, na nyingine ni Tume Kificho ya Watu Wachache wa Frelimo waliokuwa na meno, rasilimali fedha na maamuzi ya kupika matokeo asema Fernando Mazanga

Alipoulizwa kuhusu Tume Kificho ya Watu wachache wa Frelimo ikifanyaje kufanya uchachuzi wa mchakato wa mzima wa matayarisho ya uchaguzi, uandikishaji na upigaji kura siku ya uchaguzi tarehe 9 Oktoba 2024 kigogo Fernado Mazanga alifunguka ...

Tume ya Ukweli ya uchaguzi ilinyimwa fedha na wizara ya fedha ya Mozambique na hata pesa zikipotolewa kidogo zote zikitumika makao makuu ya tume huku mikoani, wilayani na mitaani wasimamizi na wasimamizi uchaguzi walikuwa hoi si kifedha bali hata kimafunzo ya kuwapa uwezo wa kuandikisha wapiga kura, uteuzi na rufaa za mapingamizi.

Wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi walikuwa hawaelewi kanuni, sheria na miongozo ya kufanikisha uchaguzi ulio wa kiwango cha kukubalika ni huru, usiopendelea upande wowote na wakuweza kutoa matokeo sahihi ya kura zilizopigwa na mgombea yupi kazoa kura halali.

Fernando Mazanga anaongeza kuwa kutokana na Tume halisi kunyimwa uwezo wa kila aina, Tume kificho ya FRELIMO iliingia kazi kutangaza idadi ya watu waliojiandikisha ambayo haiwiani na takwimu za sensa ya taifa ya Mozambique ikiyofanyika 2023.

Wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi katika majimbo na wilaya walikosa kuwa na idadi za kulinganisha idadi ya watu katika maeneo yao ya majimbo, wilaya, kata na mitaa hivyo kura za ziada ya kuongezwa na FRELIMO ziliweza kutangazwa.

Huku wananchi hawafahamu idadi ya watu rasmo ktk maeneo yao kama sensa ya taifa ilivyokuwa ikionesha eneo kwa eneo, kijiji kwa kijiji, mtaa na kata.

Ingawa vyama makini vya upinzani zilipiga kelele kuwa idadi ya kuandikishwa watu katika sensa hailingani idadi ya wapiga kura watarajiwa na kura za matokeo yaliyotangazwa zimezidi kwa mbali idadi ya watu katika ripoti za sensa za taifa .

Wananchi baada ya kustuliwa kuhusu wafanye rejea za idadi ya watu na idadi ya wapiga kura wakabaini uchafuzi uliofanyika na kupelekea maandamano nchini Msumbiji kupinga matokeo yaliyotangazwa.

Mahakama ya Kikatiba iliyopewa mamlaka kusikiliza mapingamizi ya matokeo, imeomba tume ya uchaguzi ya taifa iwasilishe nyaraka ili ukaguzi ufanyike. Tume ilipewa siku 8 iwe imewasilisha nyaraka zote za uchaguzi uliofanyika 9 Oktoba 2024 zipitiwe na kufanyiwa ukaguzi wa kina.

Bw. Fernando Mazanga Naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Mozambique anasema siku 8 zimepita na zinaonesha kuwasilishwa nyaraka zote zilizohifadhiwa katika Ofisi za Majimbo na Wilaya.

Lakini pamoja na nyaraka hizo kukusanywa sehemu, Mahakama ya Kikatiba hawajapewa makaratasi hayo ya kura na rejister za wapiga kura leo.

Inasemekana serikali inalaumu kutofika makaratasi hayo kutokana na vurugu za maandamano, lakini kigogo huyo Fernando Maganza anatillia shaka sababu hiyo kuwa vurugu zimezuia katatasi hizo kufika mji mkuu wa Mozambique Maputo.

Pengine Tume fiche ya Uchaguzi ya FRELIMO imeshikilia makaratasi hayo katika kituo salama (safe house) ikiyapitia matokeo hayo ya uchafuzi wa uchaguzi na kujiuliza wayawasilishe au la. Pia wanatafuta njia nyingine ya kuingilia mchakato wa Mahakama ya Kikatiba n.k n.k kujiokoa kutoka skandali hilo zito.

Fernando Mazanga alipoulizwa kama matokeo yanaweza kufutwa kutokana na uchafuzi wa wazi wa mchakato na uchaguzi sawia, kigogo huyo mzalendo wa Tume Halisi ya Uchaguzi anasema hawezi kutoa mawazo yake sasa kwa kuwa yeye ni mtu wa ndani kabisa katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mozambique.

Hivyo anaiachie Mahakama ya Kikatiba ibebe majukumu yake kuhakiki na kutoa hukumu sahihi baada ya kujiridhisha na ushahidi wote anahitimisha naibu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchi Mozambique Bw. Fernado Mazanga.

Muito Abrigado kwa kutusikiliza
Source : DW Português para África : DW Kireno Africa

More info :
Maputo, Mozambique
Mahakama ya Katiba Mozambique yataka wasimamizi wa uchafuzi wa uchaguzi kujitetea madudu ya wazi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa 9 Oktoba 2024 nchini Mozambique
1740227388560.jpeg


Picha : Waheshimiwa majaji wa Mahakama ya Kikatiba Mozambique
 
Tundu Lissu No Reforms No Election, moja wapo ya reforms ni kuhakikisha uwiano wa watu wanaowakilishwa na wabunge urekebishwe :

"DAR ES SALAAM ILITAKIWA KUWA NA MAJIMBO 25 SIO KUMI" - TUNDU LISSU

View: https://m.youtube.com/watch?v=s4OofpFoCr4

Gerrymandering ni kutengeneza mipaka ya majimbo bunge mengi, mitaa, vitongoji kwa kuweka mipaka / au wingi lengo ili kuhakikishia kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji wengi na kushinda uchaguzi.

MICHEZO MICHAFU YA KUHONGA NA KUGAWA MIPAKA YA MAJIMBO

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu kwa mifano hai ya michezo ngazi ya jimbo akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media
Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha ... Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema..... soma zaidi : source : Hotuba ya Jaji Josefu Warioba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Tanzania
Gerrymandering is to manipulate district boundaries, for political advantage.
 
Wanabodi,

Naomba kuanza na angalizo!
Simple Mind Discuss People
Ordinary Mind Discuss Events
Great Minds Discuss Ideas。

Hili ni moja ya mabandiko yangu ya kiutu uzima,ya ku discuss ideas, hakuna kutaja majina,wala ku discuss watu!。

Naomba wachangiaji tujadili hoja tuu ya msingi bila kutaja jina la mtu yoyote,na ikitokea ukajisikia kuwashwa washwa kutaja majina,wewe ujijue bado ni mtoto,bandiko hili sii saizi yako,nakuomba jipitie zako kimya kimya,nenda kwenye mabandiko ya saizi yako!,na nimuombe mode,turudishe ile nidhamu ya jf ya zamani, ukiona mtu yoyote kataja jina lolote kwenye bandiko hili,futilia mbali hiyo post,tuanze kurudisha ile jf ya enzi zile,watu wanakata issues hivyo kutenganisha mambo kikubwa na mambo ya watoto。

Hili ni bandiko la swali,huu ni mwaka wa uchaguzi,kuna vitu tumekuwa tunaviomba vifanyike kabla ya uchaguzi wa mwaka huu wa 2025, mpaka sasa tumeingia mwaka wa uchaguzi, vitu hivyo havijafanyika!,hii imepelekea mimi kujiuliza,hivi Inawezekana ni kiburi na jeuri ya sifanyi,kwani nisipo wasikiliza,na nisipo fanya,
mtanifanya nini?。

Na kiukweli katiba yetu imemruhusu,anaruhusiwa kushauriwa tuu na yeyote,lakini kwenye kufikia maamuzi,atafikia maamuzi yeye kama yeye,halazimiki kufuata ushauri wa yeyote,na maamuzi yake hayahojiwi na mamlaka yoyote!。

Na hata ikitokea akafanya maamuzi yoyote kwa makosa ya kisheria,kikanuni na kiutaratibu,tumempa kinga ya kutokushitakiwa popote,unless kama makosa hayo ni makosa ya ukiukwaji na uvunjaji wa katiba ya JMT,then anashitakiwa kwa mujibu wa Ibara ya 56A ya katiba, lakini ni mara ngapi viongozi wetu wamekiuka katiba,wamevuja katiba na mahakama imetamka wazi jambo fulani ni kinyume na katiba,lakini viongozi wetu wanalitenda na hawafanywi lolote?itakuwa haya ya kusema na kuandika?!。

Au ni kweli kabisa yuko real very busy sana,na hapati kabisa muda wa kutusoma?,kututazama na kutusikiliza,anawategemea zaidi wasaidizi wake tuu!,wamsomee,wamtazamie na kumsikilizishia,na hao wasaidizi wake nao ikotokea ni wako busy sana,hawajapata nafasi ya kumwambia ukweli wa ubatili wa katiba yetu na ubatili wa hii sheria yetu mpya ya uchaguzi aliyoisaini mwaka jana ambayo ndio tunakwenda kuifanyia uchaguzi wa mwaka huu, kuwa ni sheria batili inauokwenda kinyume cha katiba ya JMT?, hivyo kumlaumu ni tunamuonea bure tuu,kumbe masikini wa watu hajui?!。

Kwa vile huu ndio mwaka wa uchaguzi,hii sheria mpya ya uchaguzi,ni sheria batili kwasababu ina vifungu fulani batili,viko kinyume cha katiba ya JMT,ya mwaka 1977
Mahakama Kuu iliisha utangaza ubatili huo ni kinyume na katiba!。

Serikali ikauchukua ubatili huo,ukauchomekea kiubatili ndani ya katiba yetu,ili sasa ule ubatili wa sheria ya uchaguzi,uliotangazwa na Mahakama Kuu,kuwa ni batili,sasa umehalalishwa kwasababu umechomekewa ndani ya katiba yetu。

Mahakama Kuu ikakomaa kuwa sheria hiyo ni batili,na uchomekeaji wa vifungu hovyo ndani ya katiba ni batili!。

Mahakama ya Rufani,ikakiri ubatili huo,kwa vile sasa ubatili huo,umechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu,na aliyechomekea ubatili huo ni Bunge letu,Mahakama ikaamua,Mahakama haiwezi kuliingilia Bunge,nivyo mpira wa ubatili huo ukarudishwa mezani kwa Bunge,liuondoe!。 Bunge limekula kobisi!

Mpaka leo hii ninapoandika hapa,ubatili huo bado uko ndani ya katiba yetu!,tumetunga sheria mpya ya uchaguzi yenye ubatili ule ule sasa tunajiandaa kufanya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa katiba batilifu na sheria batili!。

A Way Forward
Ikitokea this time akaliona bandiko hili na kuvisikia vilio hivi

Nashauri
  1. Muda uliopo unatosha,kufanya minimum reforms za katiba kwa hati ya dharura,kuucholopoa huo ubatili uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu na kuifanya iwe ni katiba safi na halali。
  2. Sheria mpya ya Uchaguzi,ifumuliwe,vile vifungu batili viondolewe,kila Mtanzania awe huru kupiga kura kumchagua kiongozi anayemtaka kwa mujibu wa ibara ya 5。Kwa sasa Mtanzania hayuko huru kumchagua kiongozi anayemtaka,analazimishwa lazima amchague kiongozi aliyeletewa na chama cha siasa
  3. Ibara ya 21 yakatiba irekebishwe kila mtu aruhusiwe kugombea uongozi,kwa sasa Mtanzania haruhuhusiwi kugombea uongozi,analazimishwa kwanza ajiunge na chama cha siasa,hiko chama ndio kimdhamini,ndipo aruhusiwe kugombea,matokeo yake tunawakosa watu wazuri kutuwakilisha huku tukijaza matutusa kule kwenye vyombo vya uwakilishi,matutusa mengine kazi yao ni kugonga tuu meza kupiga makofi na kusema ndioo,nawengine haswa wale warembo wa vitu maalum,wako pale kuuza tuu sura, na kufanya kazi malum,tungekuwa na watu makini mule,yale madudu yote yalipitishwa yasinge pita kwa mserereko kivile!。
  4. Watanzania walitaka Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi,na sio kuibadili tuu jina kutoka Tume ya Uchaguzi NEC,kuwa Tume,Huru ya Uchaguzi INEC,lakini tume ni ile ile,watu ni wake wale!,tume hii iliyopo ivunjwe,isukwe upya na iwe shirikishi。
  5. Creation of level playing field kwenye the game of politics。
Watanzania tunatakiwa tutafakari kwa pamoja,tufanye nini ili kupata haki zetu za msingi za kidemokrasia na uchaguzi wa 2025 ukawa uchaguzi huru na wa haki?

Paskali
Hii imekaa vizuri sana,tatizo ni Hawa wanaojiita chawa!Hawako tayari kuuusema ukweli kwa kuhofia kukosa ulaji,matokeo yake walionyuma na Machawa nao huwako tayari kuwaambia wenzao.Kilicho Muhimu hapa ni Viongozi kama mkuu wa nchi ,waziri mkuu wawe wenye maamuzi magumu Binafsi bila kujali vyama vyao na hao Machawa kwa kuamua kuruhusu mchakato wa kubadilisha baadhi ya mambo yanayolalamikiwa na wanancnhi.
 
Tundu Lissu No Reforms No Election, moja wapo ni uwiano wa watu wanaowakilishwa na wabunge urekebishwe :


Gerrymandering ni kutengeneza mipaka ya majimbo bunge mengi, mitaa, vitongoji kwa kuweka mipaka / au wingi lengo ili kuhakikishia kupata wabunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa, vitongoji na vijiji wengi na kushinda uchaguzi.

MICHEZO MICHAFU YA KUHONGA NA KUGAWA MIPAKA YA MAJIMBO

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu kwa mifano hai ya michezo ngazi ya jimbo akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media

Gerrymandering is to manipulate district boundaries, for political advantage.
Hakuna kucheka na haya majangili
 
Acha nidhamu ya woga, Mkapa alikwishatuasa tuseme kwa ukweli na uwazi! Unataka tusimtaje kwa kuwa unamuheshimu sana au unamuogopa sana! Acha unafiki mtu mzima wewe!

Ukweli ni kuwa kwa sababu za uroho wake wa madaraka na kutokujiamini kwake Rais Samia anakanyaga Katiba!
Mkuu kama mtu huru na msomi , achana na ukubwa wako katika media za tz
.
Ulitakiwa kuyaweka bayana mapema, leo mkuu wangu umekua wa kurukaruka kwa hoja ,mara ile mara hili ,tukuweke kundi gani?

Ni wakati sasa kwenda kwa Ndugu zetu Wa hadzabe wakufundishe namna bola ya kuishi kiasili na nini wakiaminicho katika maisha yao kwa uaminifu mkubwa , kuliko kuja na mikwara kibao ati asitajwe jina la mtu ,so what! , ni mtoto gani ,mtu gani asiejua unamsema nani
,that's uteuliwi ,

maana hata ningekua mie siwezi mteua mtu ambae sielewi wapi amesimama.

Leo useme mchawi ni mzuri ameweza nipaisha kwa ungo, kesho huyo uliemsifia unasema hafafi ,kaniloga, kauwa wanangu n.k. kweli alafu tukusifie ,hamna iyo kitu.

Wewe majuzi umekuja na andiko ukitaka Lissu asaidiwe katika kile yeye na chama chake wamekuja nacho kama msimamo wa chama (no reforms no election) na blabla kibao .

Leo unakuja na agenda nyingine nyuma ya pazia , mkuu vipi? tueshimiane watz sio mbulula.

Nakueshim mkuu ila ukiendelea na tabia hii, Nitakufungia siku 14 , ili ujue Yesu ni Bwana.



Taifa limefika tulipo kwa ujinga na upumbavu wetu sie wenyewe hasa sie tujifanyao wasomi.

Tunataka msimamo wako twende kwenye uchaguzi bila reform au la full stop ,
Thanks
 
Ugumu uko hapo kwenye "hata nisipofanya watanifanya nini"kwahyo sisi tuendelee kukaa nyuma tukiomba uhai huku tukija kushuhudia mbele ya safari.
Hakika kama kina Nyerere wangesema hivyo..hadi leo tungekuwa tunaitwa Tanganyika iliyo chini ya Mwingereza!
Suluhu hapo ni kusali na kumwomba M Mungu atutibu kwanza huu Ugonjwa wa Akili tulioupata waTanzania..Ugonjwa wa kupofuka macho mara tu tunapopata Madaraka!
 
ni kujidanganya tu kwamba eti kubadili sheria za uchaguzi na katiba ya nchi ndiyo haki,

na kupuuzia nahitaji msingi ya kilasiku ya mwananchi mathalani maji, elimu, afya, kilimo n.k

wananchi wa Tanzania wataendelea kuwaamini na kuwapa dhamana za kuongoza taifa, wale ambao wanajali mahitaji yao ya msingi ya kila siku, na sio matapeli wa kupambania vyeo na madaraka kwa maslahi yao binafsi na familia zao 🐒
Alafu we tulia ,umeambiwa na mtoa mada kwamba hii ni mda kwa watu wenye IQ Kubwa sio ya kila mtu , sasa uchawa kwenye mada hii unatoka wapi, by the way wewe ni mtaka haki ila ccm imekuroga ,nimekwambia mara nyingi.



So far hu jirani yangu , kuanzia leo ujirani ufe , sasa jichanganye , hadzabe mishale nimepewa kazi yangu kucheza / lenga viuno hivyo ambavyo mnakua na kitambi badia na kulegeza majinsi , nitawatungua muone dunia ni chungu , huko kwa hadzabe nimeweka order ya moshale , na nimekaa miezi 4 mpaka sasa mtajua hamjui
 
Back
Top Bottom