Mifano ya tume za nchi kadhaa ikiwemo India, Liberia, Mozambique na The Gambia
TOKA MAKTABA :
15 December 2023
Deus Kibamba Aibua Mazito Mswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi, Atoa Mapendekezo Haya
View: https://m.youtube.com/watch?v=z8MtfR1Ccd8
Atolea mifano ya tume za nchi kadhaa ikiwemo India, Liberia, Mozambique na The Gambia kulinganisha na muswada wetu wa Tanzania kama ulivyo hapa chini. Deus Kibamba anashauri Tume ya Uchaguzi lazima iwe na muonekano kamili yaani Kichwa, Shingo na Kiwillkiwili siyo kama ulivyoanishwa katika muswada huu hapa chini uliowakilishwa na serikali bungeni :
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
No. 12 19th October, 2023
SPECIAL BILL SUPPLEMENT
To The Special Gazette of the United Republic of Tanzania No. 43 Vol. 104 Dated 19th October, 2023
Click to expand...
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
MUSWADA WA SHERIA YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WA
MWAKA 2023
MPANGILIO WA VIFUNGU
Kifungu Jina
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA UTANGULIZI
1. Jina na tarehe ya kuanza kutumika.
2. Matumizi.
3. Tafsiri.
SEHEMU YA PILI
KUANZISHWA, MUUNDO NA MAJUKUMU YA TUME YA TAIFA
YA UCHAGUZI
4. Kuanzishwa kwa Tume.
5. Muundo wa Tume.
6. Hadhi ya Tume.
7. Sifa za wajumbe wa Tume.
8. Muda wa utumishi wa wajumbe.
9. Kamati ya Usaili.
10. Uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Tume.
11. Majukumu ya Tume.
12. Maadili katika utendaji kwa wajumbe.
13. Vikao vya Tume.
14. Akidi katika vikao vya Tume.
15. Uamuzi wa Tume.
16. Posho na stahili za wajumbe wa Tume.
17. Uhusiano kati ya Tume na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.
/ISSN 0856 – 0331X
Page 1
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
2
SEHEMU YA TATU
SEKRETARIETI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
18. Mkurugenzi wa Uchaguzi.
19. Maadili ya utendaji kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.
20. Majukumu ya Mkurugenzi wa Uchaguzi.
21. Watumishi na watendaji wa Tume.
SEHEMU YA NNE
MASHARTI YA FEDHA
22. Fedha za uendeshaji wa Tume.
23. Muundo wa Utumishi wa Sekretarieti ya Tume.
24. Gharama kulipwa kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali.
25. Hesabu na ukaguzi.
26. Taarifa ya mwaka.
SEHEMU YA TANO
MASHARTI MENGINEYO
27. Kanuni na miongozo.
28. Masharti ya mpito.
Page 2
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
______
NOTISI
______
Muswada huu utakaowasilishwa Bungeni unachapishwa kwa ajili ya kutoa
taarifa kwa umma pamoja na maelezo ya madhumuni na sababu zake.
Dodoma, MOSES M. KUSILUKA,
18 Oktoba, 2023 Katibu wa Baraza la Mawaziri
Muswada wa Sheria kwa ajili ya kubainisha muundo, majukumu, utaratibu wa upatikanaji wa Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na sifa za Mkurugenzi wa Uchaguzi, kuweka utaratibu wa uendeshaji wa vikao vya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na
kuweka masuala mengine yanayohusiana nayo.
IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA UTANGULIZI
Jina na tarehe
ya kuanza
kutumika
1. Sheria hii itajulikana kama Sheria ya Tume ya
Taifa ya Uchaguzi ya mwaka, 2023 na itaanza kutumika
katika tarehe ambayo Waziri atateua kwa notisi katika
Gazeti la Serikali.
Matumizi 2. Sheria hii itatumika Tanzania Bara na Tanzania
Zanzibar, isipokuwa kwa masuala yanayohusu uchaguzi wa
Madiwani, itatumika Tanzania Bara.
Tafsiri 3. Katika Sheria hii, isipokuwa kama muktadha
utahitaji vinginevyo-
“jimbo” maana yake ni jimbo la uchaguzi kwa madhumuni
Page 3
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
4
ya uchaguzi wa Wabunge;
Sura ya 2 “Katiba” maana yake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977;
“Mjumbe” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuwa mjumbe
wa Tume kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba;
“Mkurugenzi wa Uchaguzi” maana yake ni mtu aliyeteuliwa
kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi kwa mujibu wa
masharti ya kifungu cha 18 na itajumuisha mtu
ambaye kwa kipindi hicho atakuwa anatekeleza
majukumu yoyote ya ofisi hiyo;
“Mwenyekiti” maana yake ni mtu aliyeteuliwa kuongoza
Tume na inajumuisha Makamu Mwenyekiti;
“Rais” maana yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania;
“Tume” maana yake ni Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya
74(1) ya Katiba;
“uchaguzi” maana yake ni uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani na inajumuisha uchaguzi mdogo wa
Mbunge au Diwani;
“Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na
masuala ya uchaguzi.
SEHEMU YA PILI
KUANZISHWA, MUUNDO NA MAJUKUMU YA TUME YA TAIFA
YA UCHAGUZI
Kuanzishwa
kwa Tume
4. Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano iliyoanzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya
Katiba ambayo pia itajulikana kama “Tume ya Taifa ya
Uchaguzi”.
Muundo wa
Tume
5.-(1) Tume itakuwa na Mwenyekiti, Makamu
Mwenyekiti na wajumbe wengine watano watakaoteuliwa
na Rais.
(2) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi watashika madaraka mara
baada ya kuapishwa na Rais.
(3) Uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu
Page 4
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
5
wa Tume utafanywa kwa misingi kwamba, endapo
Mwenyekiti atateuliwa kutoka upande mmoja wa Jamhuri
ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atateuliwa kutoka
upande wa pili wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Katibu na
Mtendaji Mkuu wa Tume.
Hadhi ya
Tume
6.-(1) Tume itakuwa ni chombo huru na
kinachojitegemea na maamuzi yake hayataingiliwa na
chombo chochote au kulazimika kufuata maagizo ya mtu
yeyote au Idara yoyote ya Serikali au maoni ya chama
chochote cha siasa.
(2) Tume itakuwa ni chombo chenye uwezo wa
kumiliki mali na kuwa na nembo na lakiri yake, na kwa jina
lake Tume inaweza-
(a) kujipatia na kumiliki mali zinazoweza
kuhamishika na zisizoweza kuhamishika;
(b) kushtaki au kushtakiwa; na
(c) kufanya au kutekeleza mambo yote au masuala
mengine yoyote ambayo yanaweza kufanywa au
kutekelezwa na chombo huru.
Sura ya 5
(3) Pale ambapo Tume itakuwa imeshtaki au
kushtakiwa, itapaswa kumtaarifu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ili awe sehemu ya shauri hilo kwa lengo la kukidhi
masharti ya Sheria ya Uendeshaji wa Mashauri dhidi ya
Serikali.
Sifa za
wajumbe wa
Tume
7.-(1) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume
watapaswa kuwa ni Majaji wa Mahakama Kuu au
Mahakama ya Rufani au kuwa na sifa ya kuwa Wakili na
amekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi
na tano.
(2) Wajumbe wengine watano watakuwa na sifa
zifuatazo:
(a) awe raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano
kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Tanzania;
(b) awe mtu mwaminifu na mwadilifu;
(c) awe na uzoefu katika uongozi, utawala au masuala
ya uchaguzi; na
(d) sifa nyingine ambayo Kamati ya Usaili itaona inafaa
Page 5
. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
6
au ni muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya
Tume.
Muda wa
utumishi wa
wajumbe
8.-(1) Mjumbe wa Tume atashika nafasi ya madaraka
kwa kipindi cha miaka mitano.
(2) Mjumbe wa Tume atakoma kuwa Mjumbe
endapo litatokea lolote kati ya mambo yafuatayo:
(a) ukimalizika muda wa miaka mitano tangu
alipoteuliwa;
(b) ikiwa atafariki;
(c) endapo atajiuzulu;
(d) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama
asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya
asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume; au
(e) ikiwa ataondolewa madarakani na Rais kutokana
na-
(i) kutokuwa na uwezo wa kutekeleza
majukumu yake kwa sababu ya maradhi
au sababu nyingine yoyote;
(ii) tabia mbaya; au
(iii) kupoteza sifa ya kuteuliwa kuwa
mjumbe.
(3) Endapo suala la kumuondoa Mjumbe wa Tume
litajitokeza, Rais anaweza kuunda Kamati itakayofanya
uchunguzi na kumshauri ipasavyo.
(4) Kamati iliyorejewa chini ya kifungu kidogo cha
(3) itajumuisha wajumbe wafuatao:
(a) Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye atakuwa
Mwenyekiti;
(b) Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora;
(c) Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma;
(d) Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa
Umma ya Zanzibar;
(e) wajumbe wawili wenye uzoefu wa masuala ya
uchaguzi, mmoja kutoka Tanzania Bara na
mwingine kutoka Zanzibar; na
(f) Mjumbe mmoja kadri Rais atakavyoona inafaa
Page 6
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
7
(5) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (4),
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi atateua mtumishi wa
umma mwandamizi kuwa Katibu wa Kamati.
(6) Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya
Uchunguzi itajiwekea utaratibu wa kujiendesha.
Kamati ya
Usaili
9.-(1) Wakati wowote inapobidi kuteuliwa mjumbe
au wajumbe wa Tume, Kamati ya Usaili itaitishwa.
(2) Kamati itakayoitishwa chini ya kifungu kidogo
cha (1) itakuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye
atakuwa ni Mwenyekiti;
(b) Jaji Mkuu wa Zanzibar ambaye atakuwa Makamu
Mwenyekiti;
(c) Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora; na
(d) mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Rais kwa
kuzingatia jinsia.
(3) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Katibu wa
Kamati ya Usaili.
(4) Wajumbe wa Kamati ya Usaili wataapa mbele ya
Rais kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao.
(5) Ndani ya siku kumi na nne baada ya kuundwa,
Kamati ya Usaili itatoa tangazo kwa umma kupitia
magazeti angalau mawili yenye wigo mpana wa
usambazwaji nchini na vyombo vingine vya habari
kuwaalika wananchi wenye nia ya kuomba kuteuliwa kuwa
wajumbe wa Tume kuwasilisha maombi yao kwenye
Kamati.
(6) Kamati ya Usaili mara baada ya kupokea na
kuchambua maombi ya watu walioomba kuteuliwa kuwa
wajumbe wa Tume, itafanya usaili na kupendekeza kwa
Rais majina ya watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa
wajumbe wa Tume.
(7) Kwa kuzingatia kifungu kidogo cha (6), utaratibu
wa kusimamia mchakato wa usaili utakuwa kama
utakavyoainishwa katika Kanuni.
(8) Kamati ya Usaili itawasilisha kwa Rais majina
manne zaidi ya idadi ya nafasi zinazohitajika kujazwa.
(9) Muda wa Kamati ya Usaili utakoma mara baada
Page 7
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
8
ya
Rais kuteua wajumbe wa Tume.
Uteuzi wa
Mwenyekiti,
Makamu
Mwenyekiti
na wajumbe
wa Tume
10.-(1) Rais atateua Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti wa Tume kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya
74(1)(a) na (b) na (2) ya Katiba.
(2) Rais atateua Wajumbe wengine wa Tume kutoka
miongoni mwa majina yaliyowasilishwa na Kamati ya
Usaili.
(3) Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe
wengine wa Tume wataapa mbele ya Rais kabla ya kuanza
kutekeleza majukumu yao.
Majukumu ya
Tume
11.-(1) Kwa kuzingatia matakwa ya Ibara za 74(6),
75 na 78 za Katiba, Tume itakuwa na majukumu yafuatayo:
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga
kura kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na Wabunge
katika Jamhuri ya Muungano na uchaguzi wa
Madiwani kwa Tanzania Bara;
(b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi
wa Rais na Wabunge na uchaguzi wa Madiwani
kwa Tanzania Bara;
(c) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya
Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya
uchaguzi wa Wabunge;
(d) kuteua na kuwatangaza Wabunge Wanawake wa
Viti Maalum katika Jamhuri ya Muungano na
Madiwani Wanawake wa Viti Maalum kwa
Tanzania Bara;
(e) kuandaa na kusimamia Kanuni za Maadili ya
Uchaguzi;
(f) kutoa elimu ya mpiga kura nchini;
(g) kuratibu na kusimamia taasisi na asasi zinazotoa
elimu ya mpiga kura;
(h) kualika na kusajili watazamaji wa uchaguzi;
Sura ya 298
(i) kuajiri au kuteua watumishi na watendaji wa
Tume kwa kadri itakavyohitajika kwa kuzingatia
masharti ya Sheria ya Utumishi wa Umma na
masharti mengine yatakayowekwa na Tume; na
(j) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama
yalivyoainishwa kwenye Katiba au sheria
Page 8
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
9
nyingine yoyote.
(2) Tume inaweza kukasimu majukumu au sehemu ya
majukumu yake kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, mtumishi au
mtendaji mwingine wa Tume.
Maadili katika utendaji kwa
wajumbe Sura ya 398
12. Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu
ya Tume, kila Mjumbe wa Tume atalazimika kuzingatia
Sheria ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma na
Kanuni za Maadili zitakazoandaliwa chini ya Sheria hii.
Vikao vya
Tume
13.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 74(7) ya
Katiba, Tume itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu
utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao.
(2) Tume itakuwa na vikao vya kawaida visivyopungua
vinne kwa mwaka.
(3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (2),
Tume inaweza kufanya vikao maalumu muda wowote
itakapoonekana kuwa ni lazima kufanya hivyo.
(4) Tume itafanya vikao vyake katika sehemu na muda
utakaopangwa na Tume.
(5) Mwenyekiti atahakikisha kuwa kila mjumbe wa
Tume anapewa taarifa ya kikao mapema kabla ya kikao hicho
kufanyika.
(6) Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, Mwenyekiti
ataongoza vikao vyote vya Tume na endapo Mwenyekiti
hatakuwepo, Makamu Mwenyekiti ataongoza, au ikiwa wote
wawili hawapo, wajumbe waliopo wanaweza kumchagua
mjumbe mmoja miongoni mwao atakayekuwa mwenyekiti wa
muda wa kikao husika.
Akidi katika
vikao vya
Tume
14. Akidi ya kikao chochote cha Tume itakuwa si chini
ya wajumbe wanne.
Uamuzi wa
Tume
15.-(1) Uamuzi wa kikao chochote cha Tume utafikiwa
kwa kuungwa mkono na Wajumbe walio wengi.
(2) Pale ambapo katika kikao chochote cha Tume
italazimu uamuzi kufikiwa kwa kupigiwa kura, Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti au mwenyekiti wa muda atakayekuwa
anaongoza kikao atakuwa na kura ya turufu zaidi ya kura yake
ya kawaida inapotokea kulingana kwa kura zilizopigwa.
Page 9
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
10
Posho na
stahili za
wajumbe wa
Tume
16.-(1) Wajumbe wa Tume watalipwa posho na
stahili nyingine kwa mujibu wa Sheria, kanuni, taratibu na
miongozo itakayotolewa na mamlaka husika.
(2) Wajumbe wa Tume watalipwa kiinua mgongo
baada ya kumaliza muda wa ujumbe wa Tume.
Uhusiano kati ya Tume na
Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar
17. Kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 74(13) ya
Katiba, katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume
itashauriana mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi ya
Tanzania Zanzibar.
SEHEMU YA TATU
SEKRETARIETI YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Mkurugenzi wa Uchaguzi
18.-(1)
Kutakuwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi
atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume.
(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa na sifa
zifuatazo:
Sura ya 357
(a) awe ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya
Muungano kwa mujibu wa Sheria ya Uraia
Tanzania;
(b) awe ni mtu mwaminifu na mwadilifu;
(c) awe na shahada ya chuo cha elimu ya juu
kinachotambuliwa kwa mujibu wa sheria; na
(d) awe afisa mwandamizi katika utumishi wa umma.
Maadili ya
utendaji kwa
Mkurugenzi
wa Uchaguzi
Sura ya 398
19. Mkurugenzi wa Uchaguzi ataapa mbele ya Rais
kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake na atalazimika
kuzingatia Sheria ya Kanuni za Maadili ya Viongozi wa
Umma na Kanuni za Maadili zitakazoandaliwa chini ya Sheria
hii.
Majukumu ya
Mkurugenzi
wa Uchaguzi
20.-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Mtendaji
Mkuu na msimamizi mkuu wa utekelezaji wa majukumu ya
kila siku ya Tume.
(2) Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Afisa Masuuli
wa Tume na atatekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia Sheria,
kanuni na taratibu za fedha.
(3) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), Mkurugenzi
wa Uchaguzi atatekeleza majukumu yafuatayo:
(a) kuandaa na kuratibu vikao vya Tume;
Page 10
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
11
(b) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga
kura;
(c) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi;
(d) kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Tume katika
kutekeleza majukumu yake;
(e) kuandaa bajeti na kalenda ya shughuli za Tume;
(f) kuweka kumbukumbu za vikao vya Tume;
(g) kutayarisha nyaraka mbalimbali za Tume;
(h) kushirikiana na taasisi za ndani na nje ya nchi
ambazo zinafanya kazi zinazohusu uchaguzi,
demokrasia na utawala bora;
(i) kusimamia miongozo kwa watendaji wa uchaguzi
katika kutekeleza majukumu yao kama
itakavyoagizwa na Tume;
(j) kusimamia rasilimali watu na mali za Tume;
(k) kufanya tafiti zinazohusiana na uchaguzi; na
(l) kutekeleza majukumu mengine yoyote kama
atakavyoagizwa na Tume kwa mujibu wa Sheria
hii.
(4) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatekeleza majukumu
yake kwa kusaidiwa na watendaji ambao ni watumishi wa
umma au watu wengine wenye sifa kwa kadri
itakavyohitajika.
Watumishi na
watendaji wa
Tume
21.-(1) Kwa madhumuni ya Sheria hii, mtumishi
aliyeajiriwa, aliyeteuliwa au aliyeazimwa na Tume, kwa
kipindi chote atakachokuwa anatekeleza majukumu ya
Tume, atachukuliwa kuwa ni mtumishi wa Tume na
atatakiwa kuzingatia Katiba, Sheria hii, Sheria ya Uchaguzi
wa Rais, Wabunge na Madiwani na sheria nyingine yoyote
inayohusu utekelezaji wa majukumu ya Tume.
(2) Mtu yeyote aliyeajiriwa kwa madhumuni ya
kutekeleza majukumu ya Tume, ikiwa hajaajiriwa katika
utumishi wa umma, atapokea malipo yanayostahili kwa
kazi hiyo kadri Tume itakavyoona inafaa kuidhinisha.
Page 11
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
12
SEHEMU YA NNE MASHARTI YA FEDHA
Fedha za
uendeshaji
wa Tume
22.
Fedha za uendeshaji wa shughuli za Tume zitatoka katika bajeti ya Serikali. Muundo wa Utumishi wa Sekretarieti ya Tume
23. Tume kwa kushauriana na Waziri mwenye
dhamana na masuala ya utumishi, itaandaa Muundo wa
Utumishi wa Sekretarieti ya Tume.
Gharama
kulipwa
kutoka
Mfuko Mkuu
wa Hazina ya
Serikali
24. Gharama zote-
(a) zilizotumika katika kuandaa daftari, kutoa kadi ya
mpiga kura na kufanya mambo mengine au vitu
vingine vinavyohitajika kufanywa kwa
madhumuni ya kutekeleza masharti ya Sheria hii;
(b) zilizotumiwa na Tume, Mkurugenzi wa
Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na mtu
mwingine yeyote aliyeajiriwa kutekeleza
majukumu ya uchaguzi;
(c) zilizotumika kwa ajili ya malipo ya maafisa
walioainishwa katika kifungu cha 21(2); na
(d) zilizotumika kwa ajili ya malipo kwa afisa yeyote
wa umma kuhusu shughuli rasmi zinazohusiana
au zinazotokana na uchaguzi,
zitatozwa na kulipwa kutoka kwenye Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali.
Hesabu na
ukaguzi
Sura ya 348
25.-(1) Mkurugenzi wa Uchaguzi atatunza vitabu vya
hesabu na kumbukumbu nyingine zinazohusiana na
shughuli za Tume na kuandaa taarifa ya hesabu ya mwaka
kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma.
(2) Hesabu za Tume zitakaguliwa na Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Taarifa ya
mwaka
26.-(1) Ndani ya miezi mitatu baada ya kuisha kwa
mwaka wa fedha, Tume itaandaa taarifa ya mwaka
kuhusiana na mwaka wa fedha uliopita na kuwasilisha
taarifa hiyo kwa Waziri ambaye ataiwasilisha Bungeni.
(2) Taarifa ya mwaka itajumuisha-
(a) maelezo ya kina kuhusu utendaji wa Tume kwa
Page 12
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
13
mwaka husika;
(b) nakala ya hesabu za Tume zilizokaguliwa pamoja
na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali; na
(c) taarifa nyingine yoyote ambayo Tume itahitajika
kutoa chini ya Sheria hii.
SEHEMU YA TANO
MASHARTI MENGINEYO
Kanuni na
miongozo
27. Tume inaweza kutengeneza kanuni na miongozo
na kutoa maelekezo kwa ajili ya utekelezaji bora wa
majukumu yake.
Masharti ya
mpito
28. Mara baada ya kuanza kutumika kwa Sheria hii,
mtu yeyote ambaye ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti
au mjumbe wa Tume ataendelea kushika madaraka hayo
hadi pale ujumbe wake utakapokoma.
________________
MADHUMUNI NA SABABU
_________________
Muswada huu unapendekeza kutungwa kwa Sheria ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ambayo pamoja na mambo mengine itaweka masharti na
utaratibu wa upatikanaji wa wajumbe wengine wa Tume waliotajwa katika
ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 tofauti
na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, itaainisha majukumu ya Tume
pamoja na taratibu nyingine za uendeshaji wa Tume.
Muswada huu umegawanyika katika Sehemu Tano.
Sehemu ya Kwanza ya Muswada inahusu masharti ya utangulizi ambayo
yanajumuisha jina la Sheria inayopendekezwa kutungwa, mawanda ya
matumizi, utaratibu wa kuanza kutumika pamoja na tafsiri ya misamiati
mbalimbali kwa kadri ilivyotumika ndani ya Sheria inayopendekezwa.
Sehemu ya Pili ya Muswada inahusu uanzishwaji wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi. Masharti mengine katika Sehemu hii ni pamoja na muundo wa
Page 13
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
14
Tume, majukumu, sifa za wajumbe wa Tume, muda wa utumishi wa
wajumbe, utaratibu wa vikao vya Tume, posho na stahili za wajumbe wa
Tume na uhusiano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume Uchaguzi
ya Zanzibar. Vilevile Sehemu hii inajumuisha pia masharti kuhusu uteuzi
wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wengine wa Tume.
Kwa mujibu wa Sehemu hii, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
watateuliwa na Rais kwa kuzingatia masharti yaliyopo katika ibara ya 74
ya Katiba. Uteuzi wa wajumbe wengine watano utahusisha Kamati ya
Usaili ambayo itapokea na kufanya uchambuzi wa maombi ya watu
wanaoomba kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume na kupendekeza majina
ya watu wenye sifa kwa Rais kwa ajili ya uteuzi. Aidha, Sheria
inayopendekezwa inaweka utaratibu wa Rais kuweza kuunda Kamati ya
Uchunguzi, endapo ataona inafaa, ambayo itafanya uchunguzi na
kumshauri ipasavyo kuhusu kuondolewa kwa mjumbe wa Tume.
Sehemu ya Tatu ya Muswada inaweka masharti kuhusu Sekretarieti ya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo inajumuisha Mkurugenzi wa
Uchaguzi, watumishi na watendaji wengine wa Tume. Sehemu hii
inaainisha sifa za mtu kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi,
majukumu yake, muundo wa utumishi wa sekretarieti ya Tume pamoja na
kuweka takwa la kuzingatia Kanuni za Maadili ya Viongozi wa Umma.
Miongoni mwa sifa zinazopendekezwa ili mtu aweze kuteuliwa kuwa
Mkurugenzi wa Uchaguzi ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania wa
kuzaliwa, mtumishi wa umma mwandamizi, mwaminifu na mwadilifu na
ambaye hajawahi kusika nafasi ya madaraka ya juu katika chama chochote
cha siasa. Sehemu hii inaweka pia masharti kwamba mtu yeyote ambaye
atakuwa anatekeleza majukumu ya Tume atachukuliwa kuwa mtumishi wa
Tume kwa kipindi chote atakachokuwa anatekeleza majukumu hayo na
atapaswa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utekelezaji wa
majukumu ya Tume.
Sehemu ya Nne ya Muswada inahusu masharti ya fedha ambayo
yanajumuisha vyanzo vya fedha za uendeshaji wa Tume, gharama za
uendeshaji wa shughuli za uchaguzi, ukaguzi wa hesabu na na uwasilishaji
wa taarifa za utendaji wa Tume Bungeni. Inapendekezwa kuwa chanzo cha
fedha za uendeshaji wa Tume kitokane na fedha zitakazoidhinishwa na
Bunge kupitia bajeti ya kila mwaka ya Serikali. Vilevile, kuhusu fedha
zitakazotumiwa na Tume katika uendeshaji wa shughuli za uchaguzi,
Sehemu hii inapendekeza kuwa fedha hizo zitoke katika Mfuko Mkuu wa
Hazina ya Serikali. Aidha, kama ilivyo kwa taasisi nyingine za umma
Page 14
Na. 12. Muswada wa Sheria ya Tume ya taifa ya Uchaguzi 2023
15
zinazoendeshwa kwa bajeti ya Serikali, hesabu za Tume zitakaguliwa na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Sehemu ya Tano ya Muswada inahusu masharti mengineyo. Ili
kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, inapendekezwa
kuipa Tume mamlaka ya kutengeneza kanuni, kuandaa miongozo na kutoa
maelekezo mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji bora wa majukumu yake.
Sehemu hii pia inaweka masharti ya mpito kuhusiana na wajumbe wa
Tume ambao watakuwa madarakani wakati wa kuanza kutumika kwa
Sheria inayopendekezwa. Kwa mujibu wa masharti hayo, wajumbe hao
wataendelea kushika nafasi hizo hadi pale watakapoondolewa au muda
wao wa kuhudumu kuisha. Kwa mantiki hiyo, wajumbe wengine
watakaoteuliwa baada ya kuanza kutumika kwa Sheria inayopendekezwa
watateuliwa kwa kuzingatia utaratibu unaopendekezwa katika Muswada
huu.
Dodoma, KASSIM MAJALIWA MAJALIWA,
17 Oktoba, 2023 Waziri Mkuu
Page 15
MWISHO
..............................................................................
Kongamano la TLS juu ya Muswada wa Sheria za uchaguzi December 15, 2023
Hayo yamejiri katika kongamano leo lililoangazia sheria ya uchaguzi n.k
A National Stakeholders' Engagement Conference on Election Laws and Political Parties Affairs Laws in Dar es Salaam , Tanzania on 15th December, 2023