Iran inajitahidi sana kwa kweli. Ona hizi picha

Wali restore Air defense system saa ngapi hao Iran na walirejesha missile launcher saa ngapi mkuu zile zilizoharibiwa ijumaa???
Kwani Israel aliharibu zote nchi nzima?
 
Hivyo, kwenye huu mzozo, Iran hana kosa lolote.
Iran siyo kwamba hana kosa lolote Iran kinachomuua ni kuwamfadhiri mkuu wa vikundi vyote vya kigaidi vinavyoipiga Israel,ambapo Israel alinza na Hama's Hezbollah na sasa yuko na mfadhiri wao mkuu ambaye ni Iran,anachokifanya Israel hakina tofauti na kile anachokifanya Kagame kule Kongo, hii ni kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi zao.

Japo kuwa kazi siyo ya kitoto mbele ya Iran nchi ambayo inaweza ikawa bora zaidi kijeshi kwa nchi zote za kiislam na zile za mashariki ya kati na za kiarabu.ili kupambana na Iran unatakiwa uwe na akili za kichizi ndiyo unaweza ukathubutu kupambana nayo.

Trump mwenyewe enzi za utawala wake aliigwaya Iran hakulipiza kisasi pale ambapo Iran iliweza kulipa kisasi baada ya Marekani kuua kiongozi mmoja wa Iran.

Israel kupigana na Iran ni kama vile sungura kupigana na tembo halafu wakati huohuo ngumi za sungura ziwe zinatua kwenye kichwa cha tembo.
 
Iran amezidiwa nini? Mm hata sijui mnamaanisha nini mnaposema amezidiwa
 
Ni hivi, Iran ndani ya Iran kuna watu wanatumika na MOSAD (usalama wa Israel) ndio waliotoa michongo ya hao makamanda lakini pia haikutegemewa kwamba Israel wangefanya mashumbulizi kwa Iran ukizingatia wiki hii kulikuwa na kikao na Marekani kule Oman kuhusu masuala ya nuclear kwa Iran.

On top of that., baada ya mashambulizi makubwa ya Israel Iran wamefanikiwa kujibu kwa kishindo dhidi ya hayo mashambulizi toka kwa mazayuni, kumbuka unaposhambuliwa mara zote huwa kwanza unajaribu kutathmini hasara lakini pili kujua mashambulizi yametoka wapi na ni nani lakini kwa Iran waemfanikiwa kirahisi kumjibu adui ndani ya masaa machache na kumuumiza sana zaidi ya sana isivyotegemewa kwa nchi iliyojinasibu kuwa na mfumo bora wa ulinzi duniani including iron dom.

Katika hasara waliyoipata Israel ni pamoja na kufumuliwa kwa mtambo wao mkuu wa nuclear uliopo Haifa lakini kuweza kuichakaza Tel aviv na Jerusaelm vipande vipande kwa siku 2 tu tena kwa mashambulizi mawili tuu.

Wewe ungejiuliza makamanda wameuliwa lakini kwanini wamefanikiwa kiasi hicho? Jibu ni rahisi sana Iran wamejipanga sana na muda mrefu sana akitoka nani ataingia nani kazini.
 
Acha ujuaji, Iran alikua karibu kuingia deal na Trump, netanyahu akaona avuruge
 

Attachments

  • Screenshot_2025-06-15-21-59-51-199.jpg
    345.5 KB · Views: 25
Asilimia 90 za juu ziliharibiwa zilitolewa zingine kwenye maghala.
Ok.. Kwahiyo wakati mchakato huo unaendelea wengine walikuwa wako kwenye mahandaki kufungua vinu vya nyukilia ili kuhamisha?
 
Ayatollah mpaka sasa asingekuwepo angeondoka pamoja na magenerally wake siku ileile ya kwanza amshukuru Trump alimuokoa.
 
Tehran ina watu wengi kuliko nchi ya Israel
Yes Tehran ina watu wengi yaani ni wengi hasa mfano Dar mara 2.5 yake nahisi. Ingawa sina uhakika na Idadi ya Israel ila Tehran ina watu wengi mno hadi mji una joto.
 
Ok.. Kwahiyo wakati mchakato huo unaendelea wengine walikuwa wako kwenye mahandaki kufungua vinu vya nyukilia ili kuhamisha?
Hivyo ndivyo inavyosemekana kwa mujibu wa Iran officials.
Ngoja nitafute Ile article niilete hapa.
 
Anacho fanya Israel kwa sasa ni kubonda mifumo ya ulinzi wa anga na mifumo ya kurushia makombora huko Iran kisha aanze kazi yenyewe sasa,

Lengo lake kuu hasa ni kufanya Iran awe kiwete kijeshi.
 
Hapana huyo boya Kuna kipindi alijifanya kapigana vita ya Kagera.

Tena akajinasibu alistaafu jeshini akiwa na cheo Cha luteni colonel
Kuna kizazi cha ovyo sana aise. Labda angesema ni jambazi lililokosa kijiwe. Watu wa enzi hizo waliopo hapa,na ujinga kama ule wake wangapi?
 
Anacho fanya Israel kwa sasa ni kubonda mifumo ya ulinzi wa anga na mifumo ya kurushia makombora huko Iran kisha aanze kazi yenyewe sasa,

Lengo lake kuu hasa ni kufanya Iran awe kiwete kijeshi.
Kwa hiyo,kwa akili zenu,Iran mmeifananisha na Palestina sasa! Kazi mnayo
 
Duh! Haya,tunayoambiwa yanatua Israel kutoka Iran yenyewe sasa yanatokea wapi? Kama Israel yupo huko angani!!!
 
Kwa hiyo,kwa akili zenu,Iran mmeifananisha na Palestina sasa! Kazi mnayo
Hapana mkuu Irani ni sawa USA.

Saa hii jengo la TV ya Iran limepigwa bom. Unaambiwa hapo ndio propaganda za Ayatollah ndio zinapotokea
 
Mkuu kwa ubora wa makombora ya Iran....
Iran imevurumisha makombora zaidi ya 200 na yalio tua na kuleta uharibifu wote huo ulio utaja ni makombora yasiozidi 10
Kwa muktadha huo kama sio mfumo dhabiti wa ulinzi anga wa Israel saa hii kwa hayo makombora hata 100 tu yangetua Tel Aviv na Haifa zingekua vifusi kama Gaza.

Israel wako very smart kuliko Iran, kuanzia kujua kuwatumia hao MOSSAD ndani ya Iran, kuwatumia majirani yanakopita makombora na kuwa hadaa Iran wakitegemea mazungumzo kumbe wanataka kupigwa

Mkuu kwasasa Iran hali ni mbaya jamaa wanaijua Iran in and out, wana watu wao Iran pia
Sasa hivi anga la Iran lipo UCHIIII
Kurusha tu makombora imekua kipengele maana ndani ya dk sifuri baada ya kurusha fight jet zinaingia na kufumua

Njia ambayo Iran alikua anaitegemea sana na yenye ufanisi kiasi kupenya mfumo wa ulinzi anga ilikua ni kurusha makombora mengi kwa wakati mmoja ambapo mfumo unakua unazidiwa
Lakini sasa Israel ndio ina deal na hizo launcher

Ngoja tuendelee kujionea labda kuna ambayo hatujui
 
Anacho fanya Israel kwa sasa ni kubonda mifumo ya ulinzi wa anga na mifumo ya kurushia makombora huko Iran kisha aanze kazi yenyewe sasa,

Lengo lake kuu hasa ni kufanya Iran awe kiwete kijeshi.
Nadhani kwenye mifumo ya anga ni kama kamaliza maana ndege na drone zinaruka muda wote kwenye anga la Iran zitakavyo

Hapo changamoto ni hizo launcher maana ni magari na yana move kutoka sehemu moja kwenda nyingi

Zinaweza kuwepo launcher nyingi lakini Iran inabidi wawe makini zisibainike maana zikimalizwa hali itakua tete
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…