Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Mimi sichangii chochote nasikilizia wachambuzi kutoka Nantumbo
Ngoma hii tete haiwezi Kaa tu pembeni najua ulijifunza kitu kwenye vita vya Oct 07,2023 maana uliokuwa unawaramba miguu wote walifyekelewa mbali najua sasa hutaki kutumia makosa.** Usiyempenda kaja**
 
Linapokuja suala la war strategies, waajemi always wapo mbele ya muda. Hawatumii hisia kufanya maamuzi.

Wana udanganyifu wa kimkakati (strategic deception), huwezi tabiri next move wanafanya nini, na hapo ndipo huwauza Israel na wanapoteza muelekeo wa intelejensia yao.

Mfano Israel anashambulia akiwa anafahamu Iran itajibu kwa namna hii ama ile, halafu ajabu Iran inakaa siku 2 bila kujibu huku Israel ikiwa inajiuliza kuna nini kinaendelea, hio ndio strategic deception (udanganyifu wa kimkakati).

Iran pia wana uwezo wa juu wa kubadili mbinu kwa haraka(operational maneuvering).. kwa kifupi waajemi strategies zao za kivita inapelekea kuwa unpredictable .

Kitu ambacho kinapelekea adui atumie vibaya silaha zake, aingie kwenye mtego bila kujua au abadili mikakati..

Ile vita sya iku 12, US aliweka meli za kivita mashariki mwa bahari ya Mediterranean ili kulenga missiles za Iran, zile destroyers zilikuwa na interceptors aina ya SM-3, destroyers zililenga missiles hadi SM-3 zikawa zinaelekea kuisha..


Iran bila shaka atawaingiza tena cha kike safari hii maana hawaishiwi mbinu hao jamaa.. hapo unaweza shangaa inapita siku kadhaa hawarushi hypersonic kumpoteza adui, ama wakatumia silaha ambayo haijawahi kuonekana.
Unapozungumzia suala la kushambulia kimkakati na statergies kama utaweka ushabiki pembeni basi utaona Israel huwa yupo mbali sana kumshinda Iran
 
Ngoma hii tete haiwezi Kaa tu pembeni najua ulijifunza kitu kwenye vita vya Oct 07,2023 maana uliokuwa unawaramba miguu wote walifyekelewa mbali najua sasa hutaki kutumia makosa.** Usiyempenda kaja**
You are Pathetic Scumbabag , sijawahi kushabikia vita humu Jf kama Simba na Yanga .

Kwa ushahidi zaidi kaanagalie uzi wa October 7 mapema kabla ya Mayahudi kuanza kushambulia Gaza nilionya kwa wanashangilia ambush ya Hamas kuwa matokeo ya hii vita yatakuwa mabaya zaidi kwao.
 
Waajemi nadhani hauwafuatilii vyema waajemi sio wanyonge that's why unaona Tayari wameshaanza kugawa dozi pia na wao Je Maduro alishawahi kufanya hivyo !? Iran sio Libya
time wili tell, but still unaona jinsi iran inavyopokea kipigo, hii regime inaangushwa mjuba jionee mwenyewe
 
You are Pathetic Scumbabag , sijawahi kushabikia vita humu Jf kama Simba na Yanga .

Kwa ushahidi zaidi kaanagalie uzi wa October 7 mapema kabla ya Mayahudi kuanza kushambulia Gaza nilionya kwa wanashangilia ambush ya Hamas kuwa matokeo ya hii vita yatakuwa mabaya zaidi kwao.
Aksante kwa kulikuwa hiyo!!
 
US na Israel wana kinyongo na wanajaribu kuficha aibu walioipata kwenye 12 days war...
Mataifa mawili yenye uchumi, silaha za kisasa kuichangia nchi yenye vikwazo karibu miaka 50 na bado wakashindwa.. ni jambo la aibu..

Ni kitu kinawasumbua sana...

Iran inaitishia Israel tokana na vikwazo kutoizuia kukua kiteknolojia na uwezo wa jeshi, wanataka iwe weak kama Yemen, Syria, Iraq an the like, ili Israe ikose mpinzani ME..

Ila tukumbuke Israel leo usiku inakwenda kupigwa vibaya... kama kawaida muajemi moto wake huwa ni usiku...
Pia mara Hii Muiran anaanza na Radar, Radar iliopigwa Qatar ni kubwa kushinda zote ME hapo, Kilomita 5000 ina detect, so alimaliza Base panakua peupe hapo vitu vitapita Tu.
 
Unawapemda sana Iran. Ila this time wamefika mwisho wao.
SI kuwapenda bali nakubali uwezo walionao, kufikia uwezo ule wa kutengeneza silaha ambazo hata US na ISrael hawana, na kutengeneza centrifuges za kisasa na Air defense huku wakiwa kwenye vikwazo nusu karne, aisee inabidi kukubali tu jamaa wana akili. Middle east yote hakuna nchi imeweza hivyo licha kuwa ni nchi tajiri. ZAidi wananunua teknolojia nje.

Ndicho kitu kinaiogopesha Israel na US, Iran inaonekana kabisa miaka 10 ijaya nchi za middle east zitaanza kuitegemea kikanda kama super power wao dhidi ya Israel. Na ikifika hio hatua maisha kwa Israel yatakua magumu. Ndio maana wanawahi na kufanya mashambulizi kuidhoofisha kila siku kwa kutumia vita.

Kwa jinsi Israel walichofanya Gaza, nchi za middle east hazijapenda, hilo linaweza pelekea nchi hizo siku zijazo kuegemea upande wa Iran, Iran pia inaweza kuwauzia silaha za hypersonic , air defense na vifaa vingine, au pengine kutengeneza umoja wa kikanda.

Kiufupi Iran ni threat kwa US na Israel, inaleta picha mbaya vita ya siku 12, US alishindwa kulinda anga za washirika wake, which means Iran inazidi kuonekana mbabe. Hivyo usije shangaa Jordan, Bahrain, Qatar n.k wakataka kupewa ulinzi na Iran. Na ikifikia hio hatua US ndio bye! bye! anafungasha vilivyo vyake na kutoa kambi zake, kitu ambacho ni pigo kubwa sana kwa US.
 
Ndiyo walianza Marekani na Tomahawks (nimeona video kutoka page za Iraq)
Kisha Israel nao wameweka Video wakishambulia Launchers kwa F15

Mi nawalaumu Iran kutegemea ulinzi toka China na Urusi.

Pia Iran hakutumia akili ye kaona kila siku Marekani anapeleka zana Middle East ila hashtuki
Sasa mkuu ulitaka wafanye nini, unajua lakini kwamba USS GERALD FORD ipo middle east? Ile USS GERALD FORD inaweza zima 80% ya anga la Iran kama sio 100%.

Ile ni Military Base na Command Post inayotembea baharini.
 
Pia mara Hii Muiran anaanza na Radar, Radar iliopigwa Qatar ni kubwa kushinda zote ME hapo, Kilomita 5000 ina detect, so alimaliza Base panakua peupe hapo vitu vitapita Tu.
Safari hii inabidi Israel ipigwe haswa, yaani itandikwe haswa hakuna cease-fire..
Israel ipigwe ichakae ili kusudi siku za mbeleni wasijifikirie tena kuivamia Iran.
 
Trump na Europe pamoja na washirika wao wote ni wajanja sana, wanajifanya kama wamegombana, kumbe lao moja.

Hii vita ya tatu ya dunia wanaiendesha ki mkakati sana.

from no where:
1)Trump akaanza kuwatusi viongozi wa umoja wa ulaya
2)Trump anaitaka Green land
3)Mafaili ya Epstein(naskia putin ana picha mjongeo za trump na vibinti.)
4)Wahamiaji wakala deportation

Pamoja na mengine mengi hayatokei kwa bahati mbaya.


hizo ni geresha, kuna watu wanadanganywa na wanadanganyika ni urusi, China, Iran, North Korea.

Muhindi yeye ni double agent ndio maana umoja wa ulaya baada ya kujifanya wamegombana na trump wakampa dili kubwa la kupeleka wataalamu wengi umoja wa ulaya yote.

unaambiwa hili ni bonge moja la dili India kupata.


View: https://youtube.com/shorts/vGC0bhSMI88?si=kDGwebVTGzQHTjYj.

Sasa zamu ya muiran imefika, mwanzo walitaka kuanza nae, alivyojibu mapigo wakaona chizi mabomu huyu atatumaliza ngoja tujipange.

Us ili kujifanya kaamulia ugomvi akashambulia vinu vya nyukria, haikuwa bahati mbaya ile ilikua ni tactic ya kumpunguza nguvu Iran ili ikija phase ya pili(hii iliyoanza leo) asiwe na nguvu hata kama kaanza kutengeneza vingine.

Phase ya pili marekani katika kupasha pasha kabla ya mechi, akaamua kumchukua moduro ghetto kwake.

Na huu ni ujumbe kwa nchi ndogo ndogo zilizopo BRICS kama vile South Africa, Brazil kwamba nyie hakuna haja ya vita, natuma kikosi kinakuchukua(kwenye kundi hili ndio hata sisi tumo)

Sasa mechi imeanza leo baada ya maandamano kufeli.

Iran atapigwa vizuri tu, na atachagua mwenyewe akimbilie Russia kama Al asad au ajifiche mpaka atakapofikiwa

Hakuna China wala Russia atakaejaribu kukinga kifua zaidi ya maneno

China kawekewa Taiwan inamtazama vizuri tu.

Kiduku akijifanya hana akili nzuri kuna South Korea

Mrusi ambae alikua na afadhali, kasogezewa fupa lisiloisha Ukraine kila aking'ata wapi na wenzake China na North Korea wanajifunza kutokana na makosa ya Swahiba wao Russia.

Wakimalizana na Iran nadhani kituo kinachofuata atakua kiduku, kiduku akiguswa najua China na Russia wataingilia, na hapo watakua wamechelewa.

Umoja wa ulaya utaungana na Us

Kwa North Korea itakuwa ni ngumu mkuu kwa kuwa tayari ana nuclear bomu na anaweza kulitumia kama kinga ya vita. Pia North Korea sio tatizo sana kwa usalama wa Dunia na Marekani kwa kuwa anadeal na issue zake na raia wake.

Kinachomponza Iran azuiwe kumiliki nuclear nadhani ni tabia yake ya kufadhili vikungi vya kigaidi jambo ambalo Marekani anaona ni hatari kwa usalama wake na usalama wa dunia. Tupende tusipende Marekan ndio kiranja wa Dunia hivyo anapaswa kulinda usalama wa Dunia
 
USA kashapata kisingizio cha kuwanyoosha hawa. Wanamsubiri aendelee kurusha missiles zake middle wamshushie vifurushi. Attack ya kwanza ilikuwa kulenga viongozi sijui kama wamefanikiwa. Zitakazofuata za miundombinu waIran wataanza kukimbia nchi.
Wakipiga hizo miundombinu nchi itajaa maandamano makali zaidi.
 
Back
Top Bottom