Israeli - Imekuwa Taifa lenye nguvu kubwa sawasawa na jinsi Mungu alivyoahidi

Israeli - Imekuwa Taifa lenye nguvu kubwa sawasawa na jinsi Mungu alivyoahidi

Mimi natabiri anguko la Taifa linalojiita Israel , sababu pale walipo ni sehemu takatifu wanapanajisi kwa kuruhusu ushoga , uasherati , pamoja na kufanya dhuluma nyingi.

Siku zote Mwenyezi Mungu hayuko pamoja na watu waovu wafanya dhuluma na wanapozidi kwenye hayo basi maangamio yapo karibu hata ikiwa baada ya miaka 100 au 300 siku zote waovu hawana mwisho mwema .

Na tambua watu kuwa na mafanikio ya kidunia na kustawi vizuri sio ishara ya uchamungu na kupendwa na Mwenyezi Mungu kwani hata Firauni alineemeshwa kisawasawa kwa miaka mingi mpaka akafikia kufanya kiburi kujiona yeye ndio kila kitu , sasa angalia mwisho mbaya ulioje kwa watu waovu baada ya kujisahau sana akaangamizwa vibaya sana na hivyo hivyo ndivyo utakuwa mwisho wa Taifa linalojiita Israel usighurike na hizo so called achievements are nothing but destructions.
Katabiri kule Maka kwa mudi ,Mwanamfalme wa Saudia anapeleka starehe na ushoga

Kuhusu Israel kila kitu kipo wazi, na watamrejea Yesu na baadhi wameshamrejea

Warumi 3
1 Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini?

2 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.

3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?

4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.
 
Kwahiyo Allah ni Mungu wa waislam?
Naona hujanielewa. Hata huko Israeli kuna Wakristo wanaotumia jina hilo Allah wakimaanisha Mungu. Lakini maana ya Mungu inatofautiana katika Biblia na kwenye Quran. Kwenye Biblia Mungu ana nafsi tatu. Kwenye Quran, Allah ni mmoja tu.
 
Pilau ndiyo lipi na ugali ndiyo upi...
Afadhali umekula ugali leo. Nilikuwa namaanisha comment yako ni ile ile kila wakati("za kuambiwa changanya na zako cc...") hiyo ndio pilau 🙂
 
Afadhali umekula ugali leo. Nilikuwa namaanisha comment yako ni ile ile kila wakati("za kuambiwa changanya na zako cc...") hiyo ndio pilau 🙂
Ahsante kwa taarifa nilidhani wewe ndiyo ugali...
 
Watu wameduwaa! Watu wamebaki midomo wazi kwa jinsi wanavyoona Taifa la Israeli likiinuliwa na kuwa na nguvu kubwa. Nawaonea huruma wanaoamini uongo wa Ibilisi eti Biblia ni maneno ya watu. Biblia ingekuwa ni maneno tu ya watu, basi ahadi alizozitoa Mungu kwa Israeli zisingetimia kwa usahihi wa ajabu kama tunavyoshuhudia leo. Mungu aliahidi mambo makubwa kwa taifa la Israeli, na licha ya vikwazo na mapingamizi mengi, historia imethibitisha wazi jinsi ahadi hizo zilivyotimia.

Baadhi ya ahadi za Mungu kwa Israeli zilizotimia:
  1. "Nitawatawanya katika mataifa na baadaye nitawarudisha" (Ezekieli 36:24)
    Israeli walitawanywa duniani kote baada ya uharibifu wa Yerusalemu mnamo mwaka 70 BK. Lakini Mungu aliahidi kuwakusanya tena, na mnamo mwaka 1948, taifa la Israeli lilirejeshwa rasmi. Jambo hili sio la kawaida kwa taifa lililotawanyika kwa maelfu ya miaka.

  2. "Nitakufanya taifa kubwa" (Mwanzo 12:2)
    Mungu alimwahidi Ibrahimu kwamba atambariki na kumfanya kuwa taifa kubwa. Leo Israeli ni taifa lenye nguvu, na lenye ushawishi mkubwa ulimwenguni.

  3. "Nchi ya Israeli itastawi" (Ezekieli 36:34-35)
    Mungu kwa kumtumia Nabii wa kweli Ezekieli, alitabiri kwamba nchi hiyo iliyokuwa kame na jangwa itastawi na kuwa na rutuba. Leo, Israeli inaongoza kwa uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo na umwagiliaji, na imegeuza jangwa kuwa bustani yenye mazao tele.
Naku-challenge wewe unayedai Biblia ni maneno ya watu, tunga na wewe ahadi fulani. Chagua nchi moja Afrika uitamkie ahadi hiyo. Tamka jambo ambalo halipo kabisa katika nchi hiyo, useme kwamba litakuwepo baada ya miaka 10 ijayo. Andika tamko lako hilo kwenye kitabu halafu uone jinsi utakavyoaibika baada ya miaka hiyo 10 kupita, kwakuwa hayatatimia utakayotamka!
Wewe ni mlokole ?
 
Wewe ni mlokole ?
Soma uzi huu utapata jibu
 
"Ahadi walizoahidiwa waisrael zimetimia"

Kabla ya kujua hizo ahadi kama kweli zimetimia au laa lazima tujue Israel ni nini kwa mujibu wa Biblia??

Ngoja nikurahisishie.

•jee ni watu maalumu.?
• jee ni Taifa furani??
•jee ni muunganiko wa kabila furani??
•jee Ni eneo la mipaka ya nchi????

Neno Israel kwa mujibu wa Biblia ni nini??
Setfree
 
Ungemuuliza kwanza Doctor yeyote usingeandika comment hiyo.
Magonjwa ya akili majina yake haya hapa. Niambie kama unaona jina "Dini" kwenye list hii:
  • Depression
  • Anxiety Disorders
  • Schizophrenia
  • Bipolar Disorder
  • Panic Disorder
  • Obsessive-Compulsive Disorder (OCD)
  • Post-Traumatic Stress Disorder (PTSD)
  • Anorexia, Bulimia, Binge Eating
  • Personality Disorders
  • Psychosis
  • Dementia (eg Alzheimer’s)
  • Attention-Deficit/Hyperactivity Disorder (ADHD)
"Religious disorder" can refer to various mental health conditions, including religious OCD (scrupulosity), religious delusions, or hyperreligiosity, which involve intense religious beliefs or obsessions that interfere with daily functioning.

Una Hyperreligiosity inakusumbua.
 
Back
Top Bottom