Je, Kuna sheikh yoyote mwenye masters au phd kama ilivyo kwa maaskofu wengi?

Je, Kuna sheikh yoyote mwenye masters au phd kama ilivyo kwa maaskofu wengi?

Status
Not open for further replies.
hizo ni kejeli ambazo hazina msingi.
Hakuna kejeli hapo mkuu, ukweli usemwe ni muhimu mashekh wawe si tu wabobevu katika mambo ya Dini , bali hata mambo ya duniani hapa achana na phd na masters za ufugaji wa majini
 
Yeah wapo ila ni wachache sana , kibongo bongo hakuna ninayemfahamu ila huko duniani namjua mmojawapo Dr Bilal Phillips japo nae ni Phd za huko huko elimu akhera.
Na jamaa ni mtata kichizi inavyoonekana ni wale wa Jini kwa Jino 😂
Maana nchi karibu nane nadhani ikiwemo Kenya walishampa Ban asiingie.

Wenzetu walijikita zaidi kwenye neno na kueneza neno , ila upande wa pili show zote zinapigika neno linapigwa na elimu ya Dunia wamo tena sio shule ya mchezo mchezo mtu unakuta ni Padre huku ni mwanasheria au Daktari tena daktari bingwa 😂😂 vitabu vinachezewa kotekote yani !!
Daa umenikumbusha Padre Rimisho ni komandoo na ni doctor pia wa chuo vha ardhi DSM ni mtaalamu mzuri wa Majengo.
 
Daa umenikumbusha Padre Rimisho ni komandoo na ni doctor pia wa chuo vha ardhi DSM ni mtaalamu mzuri wa Majengo.
Alafu kuna muumin wa sheikh UBWABWA anataka kumfanisha naye, huu si uendawazimu?
 
Kumbuka Kuna profesa Juma kapuya, Kikwete, profesa Ibrahim Lipumba na Mimi hapa
 
Una fikra finyu sana kijana kuhusu elimu ya dini mkuu.
Kuna uwezekano wa kusoma elimu ya dini na ya secular kwa wakati mmoja.
Huyo Ahmad Rusaganya amesoma tarekh,usual,balagha na korokoro zote huku akisoma na secular.
Alienda hadi Jordan kusoma kama ilikua hujui.
Kijana kila jambo Lina watu wake, acha kubisha mambo usiyo kuwa na elimu nayo.

Unaweza kusoma na hakuna anaye bisha hilo ndio maana huko juu, nimeandika ni juu ni jambo linalo Faa, lakini kiuhalisia ni gumu sana, sababu mfumo wa elimu ya Dini, ni kila unachofanya lazima ukifanyie kazi, kimatendo na ukisomeshe pia.

Kwa wakati mmoja ni ngumu, wengi ni aidha walimaliza kwanza secular kisha wakasoma dini, au waliacha secular kisha wakasoma dini.

Ndio maana amekuwa hivyo alivyo. Mambo anayosomesha anakosea na ana makosa mengi mno. Kwanza usulubu wake sio mzuri katika ufikishaji wa dawa.

Lakini hata sisi tunasoma hiyo dini, lakini hatuwezi kufikia daraja la ushekhe, tunaishia kuwa ni wanafunzi tu. Sasa ili ufikie Daraja la juu, inabidi utumie muda mwingi kwenye dini.
 
Upo sahihi huwezi kua na kofia mbili either dini or elimu dunia.

Otherwise itakua ni ELIMU YA HAPA NA PALEE
Huwezi kua mbobevu kwenye dini bila kujitoa na kua dedicated na ELIMU ya DINI.
Watu wanaichukulia poa sana Elimu ya dini. Laiti wangesoma historia za Wanazuoni wetu, wasingeandika huu ujinga. Halafu anamtolea mfano Sheikh Rusaganya ? Anachekesha sana.

Huwa tunawaambia watu hivi "Ijue haki kwanza utawajua wenye haki ni kina nani.".

Na ndio elimu za hao Masheikh, yaani za kudandia dandia. Ni Masheikh wa Muhadhara na matukio.
 
Doh aisee mna fikra finyu sana.
Hii secular yenyewe ndio elimu ya kwanza aliyoanza kufundishwa baba yetu Adam kama elimu ya mazingira kama ilikua hujui.
Hivi unajua kwanza maana ya Secular ?
 
Elimu dunia hawaitaki? Au kama mmoja wa wachangiaji walivyosema ni uvivu
Waislamu ni tofauti sana na wasio kuwa Waislamu. Waislamu tunajua Kuna la muhimu na la muhimu zaidi. Elimu ya dini ni muhimu na ni lazima kwa kila mtu. Lakini elimu ya mazingira ni muhimu lakini si lazima kila mtu asome elimu hiyo, wakisoma wacheche watawatosheleza wengine.
 
Kijana kila jambo Lina watu wake, acha kubisha mambo usiyo kuwa na elimu nayo.

Unaweza kusoma na hakuna anaye bisha hilo ndio maana huko juu, nimeandika ni juu ni jambo linalo Faa, lakini kiuhalisia ni gumu sana, sababu mfumo wa elimu ya Dini, ni kila unachofanya lazima ukifanyie kazi, kimatendo na ukisomeshe pia.

Kwa wakati mmoja ni ngumu, wengi ni aidha walimaliza kwanza secular kisha wakasoma dini, au waliacha secular kisha wakasoma dini.

Ndio maana amekuwa hivyo alivyo. Mambo anayosomesha anakosea na ana makosa mengi mno. Kwanza usulubu wake sio mzuri katika ufikishaji wa dawa.

Lakini hata sisi tunasoma hiyo dini, lakini hatuwezi kufikia daraja la ushekhe, tunaishia kuwa ni wanafunzi tu. Sasa ili ufikie Daraja la juu, inabidi utumie muda mwingi kwenye dini.
Una ujuaji mwingi halafu mbele kiza.
Hakuna jambo gumu kama mtu ukalitilia mkazo na ukalifanyia kazi.
Nenda kajifunze maana ya sheikh kisheria na kiistwilagha ndio urudi hapa naona unaleta ujuaji mwingi tu.
 
Nenda kajifunze maana ya sheikh kisheria na kiistwilagha ndio urudi hapa naona unaleta ujuaji mwingi tu.
Hili tatizo lingine Sasa, ndio maana una muona Sheikh Rusaganya ni msomi, kiistilahi ndio kisheria.

Elimu ya dini ni jambo kubwa sana kijana. Wajue Wanachuoni kwanza ndio utajua uzito na ukubwa wa jambo la dini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom