Kuna mtu kanirushia link yao ananiambia unajiunga kwa Kiasi fulani cha pesa, mfano 540K halafu wao watakuwa wanakutumia video za matangazo ya biashara Kila siku video tano, unaview sekunde 5 Kila tangazo, halafu wao wanakulipa 18,000 Kila siku, nimekuja kwenu mnisaidie tafadhali kabla sijapigwa.
Mkuu kiufupi kabisa hawa ni matapeli,
Hata panya ili tuwanase huwa tuna wawekea mnofu wenye sumu au unatega mtego wenye mnofu... Sasa kuna panya wajanja huwa hawanasi kwenye mitego kama hii Sasa hembu tofautisha gap kati ya akili ya panya na akili ya wanadamu... Lakini bado kunapanya wanacheza na akili ya mwanadamu😂😂😂 nitoe Wito jamani binadamu wezangu tujitahidi panya wasituzidi akili/ujanja.
Matapeli wanatumia sifa kuu nne za mwanadamu kama ni mwepesi kwenye hizo sifa basi unahatihati ya kutapeliwa.
Sifa hizo ni hizi.
1. Tamaa (usiwe na tamaa na kitu kisichokua halali yako) pia hapa usiwe mroho mroho wa vyakula na vinywaji pia usimuamini kila mtu.
2. Uaminifu (usiwe mwepesi wa kuamini jambo)
3. Huruma (ukiwa na huruma sana basi hakikisha unakuwa na hekima ya kutosha/akili kwasababu kupitia huruma yako tapeli anaweza kukuaminisha (Kwahiyo tapeli anaweza kukuingia kirahisi akikujia na gia ya kuhuzunisha ukaingia mkenge) anaweza wakaja na stori ya kuhuzunisha ukamuonea huruma pengine ukamkaribisha nyumbani, game over))
4. Shida(umasikini mbaya sana, ukiwa na shida tuliza akili vizuri usiwe na pupa wala haraka amua maamuzi yako kwa Akili timamu na kufauta talatibu za kisheria, sio kwasababu una shida ndio uchukulie poa.
Yaani kwa mwanaume hakikisha watakoa fanikisha kukuibia ni wale wanaokuja ana kwa ana na silaha/majambazi au vibaka na umezidiwa, ila sio sio kwa kutapeliwa.
Mwisho kabisa linapokuja suala la mali aidha makabidhiano/kuuziana usichukukulie poa wala usilete kujuana sijui rafiki mpenzi ama ndugu, huyu jamaa yangu... Hakikisha taratibu zote zinaenda kiuweledi zaidi /kisheria/kiprofessional kwanini ni kwasababu hari ya mtu huwa inabadilika kulingana na mazingira na jambo analopitia wakati huo, mfano: mtu akiwa nashida huwa anashuka anakuwa mkarimu mpole na kwa muda huo anachokiongea ni kweli kinatoka moyoni na yuko serious kabisa, sasa wewe chakufanya hapa pasipo kujali wanakuaga muaminifu au sio muaminifu wewe cha kuzingatia Hakikisha mnaandikishiana kisheria na mbele ya mashahidi, usije kuthubutu mkakabidhiana kienyeji,
Kwanini kwasababu baadae shida ikiisha na ile hali ya usikivu unyenyekevu inaisha, ikiisha swala lako anakuwa halichukulii uzito kama walivyokua anakuomba. usumbufu unaanzia hapo na anaweza akakudhulumu kama akijua hakuna shahidi yoyote.