Je, Mwanamke ana wajibu wa kuchangia kifedha ndani ya Ndoa?

Umemaliza mkuu.....
 
Vijana watajua wenyewe waingie kwenye ndoa ama wasiingie maamuzi ni ya kwao. Na wakikaa kizembe huko kwenye ndoa watapigwa tu.
 
Nyie ndio mlikuwa na haki sawa
Mna wajibu wa kuitumikia kwa vitendo katika nyanja zote na sio kwenye siasa peke yake
50/50 haitekelezeki hata kwa mwanaume. Wanaume wengi watakataa. Kama ni utafutaji wanawake wameanza kuweza kiasi flani..
Sasa wewe mume wangu nikuage natoka naenda bar na rafiki zangu nirudi nikute umenipikia unaweza?
50/50 inawezekana kwenye mambo kama ajira, elimu na umiliki wa mali. Linapokuja kwenye suala la ndoa mwanaume wa kiafrika hawezi hayo mambo.
 
Vijana watajua wenyewe waingie kwenye ndoa ama wasiingie maamuzi ni ya kwao. Na wakikaa kizembe huko kwenye ndoa watapigwa tu.
Unavyoongea hayo kumbuka circle ya vijana haiishi kwa watu baki tu. Hata wewe mwenyewe ni dada au mzazi/mzazi mtarajiwa wa kijana.
 
Unavyoongea hayo kumbuka circle ya vijana haiishi kwa watu baki tu. Hata wewe mwenyewe ni dada au mzazi/mzazi mtarajiwa wa kijana.
Bahati nzuri nina kaka mdogo wangu mmoja ameshaoa yupo na familia yake kitambo. Sina mtoto wa kiume. Na hata ningekua nae asingekuwa kataa ndoa maana angelelewa vizuri.
 
Hehehe!!!
Mwanamke ana haki ya kutumia hela yake bila kulazimishwa kuitumia kwa ajili ya familia.
Kama ataamua kusaidia kwa hiari basi hiyo ni sadaka na wema wake tu!
Wewe akili huna kabisa. Na sijui kwanini mtu ukiwa mtetezi wa serikali ya ccm mara nyingi akili nazo zinakimbia
 
Kaka aina hii ya reasoning ni level za akina Socrate!! Naamini atakuwa amekuelewa
 
Hehehe!!!
Mwanamke ana haki ya kutumia hela yake bila kulazimishwa kuitumia kwa ajili ya familia.
Kama ataamua kusaidia kwa hiari basi hiyo ni sadaka na wema wake tu!
Uko sahihi. Hata akihonga vijana wa mjini no complaints.
 
Mwisho wa siku ukitaka ndoa iingie matatizoni gusa pesa ya mwanamke
 
Akifanya 10% ataipresent kama 70% ya mambo hayaendi bila yeye ila kwa mfumo wa malalamiko si mamlaka. Bado utakuwa na sauti ya mwisho kama mwanaume na atakuheshimu.

Akifanya 40% ataingilia mamlaka yako kiasi ila bado atakuheshimu maana 60 si haba. Mtakuwa mnabishana bishana na atakuwa mjuaji.

Akifanya 50% kwake hapo ni kama anafanya yote na wewe upo hapo kulishwa, kaheshima katakuwepo ila usipokuwa ngangari Kiburi kitakuwa 100% na anaweza kukupa maagizo ni nini cha kufanya na maisha yako. Sentensi za ushauri za nyodo mfano" Maisha si mepesi kama unavyoyachukulia, Sipendi mwanaume awe mzembe mzembe n.k " utazoea kuyasikia.

Akifanya above 50% kwake wewe ni sawa na BEKI TATU saa yoyote anakuondoa.
 
Yeah Tena uchumi WA familia unatakiwa uwezeshwe na %75 ya kipato Cha mwanamke sa Jichanganye uoe Jobless
 
Kaka aina hii ya reasoning ni level za akina Socrate!! Naamini atakuwa amekuelewa
Wanawake na logic ni vitu viwili tofauti kabisa. Mtu anataka usawa lakini hataki wajibu unaikuja na huo usawa. Mimi ndio maana hata wadogo zangu naenda nao kwa logic, sio huu ujinga wa usawa wa kijinsia.

Kuna madogo wawili wanasoma chuo, mwaka mmoja na umri wao sawa, mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Ninapowatumia hela za matumizi yule wa kiume namtumia kiasi kikubwa zaidi, kwa sababu najua yule wa kike pesa ypte anaweza kuibana na kumbebesha mzigo boyfriend wake privilege ambayo yule wa kiume hana. Na yule wa kiume nae atabebeshwa bill na girlfriend wake cost ambayo yule kike hawezi kuingia. Kwa logic kama iyo hata siku moja siwezi kutumia kanuni ya usawa ninapowapa hela. Ni lazima dogo wa kiume nimpe kiasi kikubwa zaidi
 
Ndoa na mwanamke msomi au mwenye hela ni Mungu mwenyewe aingilie kati la sivyo inavunjika wakati wowote.
 
Comments ni nyingi sijasoma,. Ila nadhani wachangiaji wengi walikuwa wanaume wakisupport mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…