Kama Mungu hayupo, maisha yana maana gani? Na kama yupo, kwanini Dunia inateseka hivi?

We chagua Moja tu acha kupoteza muda wako hili swali mpaka INAKUFA hutopata jibu.
 
Kutokujua chanzo cha kitu si ushahidi kwamba hakikuumbwa. Kusema “ulimwengu upo tu” bila kueleza kwa nini au vipi ni sawa tu na kusema “Mungu yupo tu— zote ni statements zinazohitaji msingi wa hoja.

Big Bang si hadithi ya kufikirika – ni model ya kisayansi inayotegemea ushahidi wa observational, kama cosmic background radiation na redshift ya galaxies. Haijasema nini kilikuwa "kabla", lakini inaeleza vizuri jinsi ulimwengu ulivyo anza kupanuka.

Kusema kila kitu lazima kiwe na chanzo (cause) ni hoja yenye mantiki itayokuongoza hadi kwenye First Cause — ambacho hakikusababishwa na chochote kingine. Hii ndiyo hoja ya classic ya Cosmological Argument. Huwezi kusababisha msururu usio na mwisho wa sababu.

Kwa hiyo, ukisema:
"Hakuna aliyejua mwanzo wa ulimwengu" –ni
sawa, lakini pia usidai kwamba "ulimwengu haukuumbwa/hauna Muumbaji .
Hiyo nayo ni imani, sio maarifa.

Siyo kwamba tuna uhakika wa kila kitu, lakini kati ya kusema ulimwengu haukuumbwa bila ushahidi na kusema ulimwengu una chanzo fulani, labda Muumba, hoja ya pili ina uzito wa kifalsafa na kisayansi zaidi – hata kama si majibu yote yapo.

Not knowing is not a license to deny.
 
Mateso ni nini?
 
Nakushukuru kwa kushiriki katika mjadala huu wa kina. Kama waumini wa mantiki, tunathamini sana jitihada zako kueleza uwezekano wa Mungu kupitia dhamiri, maana, na mpangilio wa asili.

Hata hivyo, kama Agnostics-Ignostics, tunaamini kwamba mijadala kuhusu Mungu mara nyingi huzunguka dhana ambayo haijafafanuliwa vya kutosha hata kabla ya kuanza kuijadili— aidha kuikubali au kuikataa.

• Mara nyingi tunaombwa kumchukulia huyu Mungu kama wa kweli kabla hatujaelewa "Mungu" inamaanisha nini kwa njia ya wazi.

Sihitaji circular reasoning inayozunguka kwenye imani ili kumuelewa.

Nahitaji kuelezewa dhana ya “Mungu” kwa njia isiyotegemea maandiko, hisia, au mila fulani? Njia ambayo akili yoyote huru inaweza kuielewa na kuiweka mezani kwa uchambuzi wa wazi?

Niko tayari kusikiliza. Lakini kama hatuwezi kuelewa “Mungu” kama dhana, basi mjadala wa “kama yupo au hayupo” hauwezi kuendelea.

Kwasababu itakua si busara kwa watu wenye Maarifa kujadili kitu wasichokijua.
 
Mimi sijui ulimwengu ulianza vipi.

Wewe unadai Mungu ndiye muumbaji wa ulimwengu na huna uthibitisho wala uhakika.

Unaleta hoja uchwara zisizo na kichwa wala miguu.
 
Wewe una uhakika na ushahidi upi kwamba Mungu ndio kaumba ulimwengu?

Au unatetea imani zako za vitabuni ulizo aminishwa na kukaririshwa?
 
Kabla ya kuuliza kama Mungu yupo, tujiulize—tunaposema "Mungu", tunamaanisha nini?

Mungu (kwa muktadha wa mantiki huru) nitaeleza ifuatavyo

Chanzo kisicho na mwanzo, chenye akili au nguvu ya hali ya juu, kinachosababisha kuwepo kwa mpangilio, sheria, na uwepo wa ulimwengu huu.

Hii haimaanishi Mungu wa dini fulani. Inamaanisha:

Chanzo (source) – kitu au hali iliyosababisha kila kitu kilicho hai au kisicho hai.

Kisicho na mwanzo (uncaused) – kwa sababu kila kitu tulichonacho kina chanzo, tunahitaji kujiuliza ikiwa kuna kitu ambacho hakikuanzishwa na kingine.

Chenye akili au nguvu ya mpangilio – si lazima kiwe "kiumbe", lakini kinaonekana kupitia muundo wa akili, sheria thabiti, na utaratibu wa maumbile.

Kwa hiyo, unaweza kuweka dhana hii mezani na kujiuliza:
Je, kuna ushahidi wa "mpangilio" unaoashiria chanzo chenye akili au nia fulani?
Ikiwa ndiyo—unaweza kuchunguza dhana hii zaidi. Ikiwa hapana—basi bado hatuna msingi wa kuendelea mbele.

Dhana ya Mungu inayoweza kuchunguzwa na akili yoyote ni:
“A necessary, possibly intelligent cause of existence and natural order.”
 
Mimi sijui ulimwengu ulianza vipi.

Wewe unadai Mungu ndiye muumbaji wa ulimwengu na huna uthibitisho wala uhakika.

Unaleta hoja uchwara zisizo na kichwa wala miguu.
Ah, kumbe hujui ulimwengu ulianza vipi lakini unakuwa na confidence ya kupinga nguvu ambayo ndiyo chanzo cha huo ulimwengu.Funny how you dismiss God kwa kusema hakuna proof, lakini unaamini theory ya explosion iliyo-organize vitu perfectly bila director,,even explosion ya gas haipangi viti sebuleni!

So, kabla hujaita hoja za wengine “uchwara,” angalia hizo zako ambazo hazina kichwa, miguu, wala spine.
 
Nipo kwenye hii stage kila kitu naona kama ilikuwa ndoto

Kwa sasa uliyoyaandika ndiyo nayaishi kila siku

Asante sana. Kwa kukutana na mtu mwenye mawazo kama yangu
 
Wewe una uhakika na ushahidi upi kwamba Mungu ndio kaumba ulimwengu?

Au unatetea imani zako za vitabuni ulizo aminishwa na kukaririshwa?
Wewe una uhakika na ushahidi upi kwamba Mungu ndio kaumba ulimwengu?

Au unatetea imani zako za vitabuni ulizo aminishwa na kukaririshwa?
Kuna watu wanapenda scientific evidence, wengine wanachukua faith kama “shortcut.” So, unaweza kusema, “If God is just a myth, explain how the universe came from nothing—no energy, no matter, no logic? Hiyo ni kama kusema hakuna muumba, lakini kila kitu kina muundo, sheria, na purpose. So, either una imani au una logic, lakini mixing both without evidence ni kama trying to swim on dry land.”
 
Kama hoja ni kwamba Mandela hakuchagua azaliwe Afrika Kusini au hata kuzaliwa kwenyewe, ni wazi kwamba Mungu hakuamua sio tu Mandela azaliwe lakini pia azaliwe wapi.

Kama watu wote popote, hakuna mtu ambaye hakuzaliwa na ambaye anakuja duniani pasipo utashi au uhuru wa wazazi ama ni mchakato wa kimaabara au wa asili.

Mungu hawambii watu wazae. Watu wenyewe ndio huamua wazae au wasizae, wapi na kwanini.
 
Siku baada ya siku

Sio msomi sana lakini najitahidi kusoma kadri ninavyoweza lakini

Kadri nazidi kusoma napata ukakasi kwenye maswala ya Mungu na dini kwa ujumla

Mpaka sasa kuna muda nahisi hakuna Mungu kuna muda najipa imani yupo ila najiuliza

Mbona ukiishi kwa sheria za kibinadamu za kawaida unakuwa mtu bora kuliko mtu wa dini au anayeamini katika Mungu

Itoshe kusema HAKUNA MUNGU
 
Nadhani tunarudi kule kule kwenye tatizo la msingi 😇

Unatuambia kuhusu "chanzo kisicho na mwanzo chenye akili" kana kwamba hilo ni jambo linaloeleweka, linajulikana au kuthibitishika—lakini je umepataje uelewa huo?”

Je, ni utafiti wa kisayansi? Je, ni dhana inayotokana na uchambuzi wa kielimu? au ni muunganiko wa nadharia na Mila ulizorithi?

Umejifunza wapi? Mkuu Notorious_Marcc.
 
Wewe wala huelewi unacho andika unakurupuka tu.

Nilikwambia mimi siamini habari za Mungu wala Big-Bang.

Nakuuliza hivi, Una uhakika, uthibitisho na ushahidi upi kwamba Mungu ndiye kaumba ulimwengu?

Hivi unaelewa kiswahili?
So, kabla hujaita hoja za wengine “uchwara,” angalia hizo zako ambazo hazina kichwa, miguu, wala spine.
Nakuuliza hivi 👇

Una uhakika na uthibitisho upi kwamba Mungu ndiye kaumba ulimwengu?

Usitetee na kufosi arguments zako uchwara za vitabuni zisizo na kichwa wala miguu.
 
Una uhakika gani kwamba Mungu aliumba ulimwengu?

Au unatetea hoja za kihuni za kutungwa na kina Aquinas zisizo na uthibitisho wala ushahidi wowote ule.

Hao philosophers wako ulio wasoma wana uhakika na uthibitisho upi kwamba Mungu ndio aliumba ulimwengu?

Walimuona akiumba?

Au walifosi mawazo yao uchwara yasiyo na uhakika wala ushahidi?
 
Yeah sure.

Mungu hayupo.

Ni wajinga wachache tu wanahangaika kumuelezea na kumtetea huyo Mungu aonekane yupo kumbe Hayupo.

Wanajaribu kufosi imani zao za Mungu, kwa kumtetea sana huyo Mungu aonekane yupo.
 
Kwanza kabisa, hujathibitisha Mungu yupo.

Na kama hujathibifisha hilo, utajuaje Mungu yupo kweli na hizo habari za Mungu si hadithi za watu tu?
 
Unataka uthibitisho wa kisayansi kwamba Mungu ndiye aliumba dunia?
Ni kipimo gani cha kisayansi kinaweza kumpima Muumbaji wa kipimo?
That's like trying to use a thermometer to measure ambition. It doesn't work.

Science inafanya kazi ndani ya mfumo wa universe ,not beyond it. Kutaka "proof" ya Mungu kisayansi ni kama kuuliza kamera ya CCTV ikuonyeshe nani aliiunda CCTV.

Kama si Mungu, ni nani basi aliumba ulimwengu?

Matter ilijiumba yenyewe?

Energy iliamka asubuhi moja na kusema, "Leo nataka kuwa Galaxy"?

That’s like believing kamusi ilijandika yenyewe baada ya kurushwa hewani na upepo. Hii ni comedy ya quantum level.

Unasema tusitumie vitabu kama Biblia, Quran au Torati kwa sababu ni "uchwara".
Swali dogo:
Kama mtu asiyemuamini Mungu haamini vitabu vya dini, halafu anauliza kuhusu Mungu, si kama kufunga macho na kuuliza kama taa inawaka?

Hauwezi kuthibitisha kuwepo kwa Mungu kama unavyothibitisha uzito wa mawe.

Usipokubali uwepo wake, basi lazima ukubali kwamba dunia hii iliumbwa kwa bahati mbaya iliyo na mpangilio mkali kama msafara wa kijeshi.

That sounds more insane than believing there's a God.

“The absence of proof is not the proof of absence.”
Na kuamini kuwa hakuna Muumba kwa sababu huoni, ni kama kusema "nimefunga macho, hivyo jua halipo.

So before you throw away the idea of God, jiulize: ni busara gani kuamini kuwa “nothing” ilizaa “something” bila sababu, bila mwelekeo, bila nia — halafu ikatufikisha hapa ambapo wewe unataka “uthibitisho”?

Mambo mengine hayataki ushahidi wa maabara ,, yanahitaji unyenyekevu wa akili, sio ujeuri wa lugha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…