Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili yatolea ufafanuzi adhabu dhidi ya Lissu kumfungia kampeni. Yasema ameadhibiwa na Kamati ya Vyama 15 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 Kamati ya Maadili yatolea ufafanuzi adhabu dhidi ya Lissu kumfungia kampeni. Yasema ameadhibiwa na Kamati ya Vyama 15 vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu

Ni kweli, maneno huwa yanaua yakitumiwa negatively, ila mtu akipuuzwa na maneno yake mwishoni anakosa maana na kuwa irrelevant.
Tatizo lipo hapa mkuu, kwa sabau Lissu hazungumzi maneno ya kupuuzwa, ndio maana wahusika wanahangaika sana.
Watu wanamwelewa vizuri sana Lissu, kwa maana anasema mengi wanayoogopa kuyasema wengi wa hao watu.

Nakushukuru kwa ufafanuzi wako, kwani nimekuelewa vizuri. Sasa najua msimamo wako haujaathirika na lolote.
 
Ndio maana ya uchaguzi kuwa anayeshinda anatangazwa. Ila kwa assessment based na hali ilivyo, Lissu atashindwa na hatakubali kushindwa. Siku zote huwa kuna correlation kati ya ushindi wa viti vya ubunge na kura za urais. Huwa haiwezekani mtu adai kushinda urais halafu ukiangalia viti vya ubunge alivyoshinda haviakisi ushindi wa kura za urais. Kumbuka kura za ubunge ni rahisi hata kila chama kujihesabia na kujua kana kilishinda au la.

Watu wanadhaniwa kuwa ni wengi katika mIkutano ya Lussu ndio hao hao wanaojaa katika mikutano ya CCM. Angalia tu mtaji wa wanachama wa kila chama kwanza kabla ya kufikiria wapiga kura wengine.
Sio lazima aliyeshinda kwa kupata kura nyingi ndio anatangazwa. Inategemea uhuru wa mamlaka inayosimamia uchaguzi wa kutangaza mshindi kulingana na aliyepata kura nyingi. Lukas Lukashenko wa Belarus alitangazwa mshindi kwa kupata zaidi ya asilimia 80 za kura zilizopigwa lakini mpaka leo hawezi kutoka nje bila ulinzi unaoeleweka na aliapishwa kwa kujificha. Mtaji unaosema wa wanachama hautoi picha halisi hasa kwa upande wa CCM kwa sababu watu wengi walijiunga sio kwa mapenzi lakini kwa maslahi au mazoea. Watumishi wengi wa umma ni wanachama kwa sababu wanaamini ni njia ya kuhakikisha ustawi wao katika utumishi wa umma. Huwezi kuamini kuwa wote hawa watakipigia kura chama ambacho wana kadi yake. Hii ni tofauti na vyama vya upinzani ambako ukweli ni kuwa wengi wanaogopa kujiunga rasmi kwa kuogopa kuwa itaathiri ajira au biashara zao. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa kuwa vyama vya upinzani vina wafuasi wengi ambao watawapigia kura kuliko idadi ya wanachama. Aidha, hata idadi ya wanaohudhuria mikutano yao haitoi picha kamili ya wafuasi kwa sababu wengi wanaogopa kuonekana wakihudhuria kwa sababu ya ajira zao au kuogopa kuwa kuna uwezekano wa wahudhuriaji kushughulikiwa.

Amandla...
 
Nikajua makamanda wataandama kupinga maamuzi ya kamati ya maadili lakini naona wanaendelea kubwekea nyuma ya keyboard kama kawaida yao
 
Tume hii iliyojaa doublestand nani mwenye akili ataiamini?!

Ina maana kwenye hizo form za kugombea wahusika hawajazi ananuani zao?

Na kama hawajazi anuani tofauti na za vyama vyao bali wanajaza za chama,nani alipaswa kuwa addressed kwenye hiyo barua kupitia ananuani ya chama?

Je,si walipaswa kumu-address Lissu kama mgombea kupitia anuani ya chama chake?
Hakuna kamati hapo ni shina la CCM
 
Ndio maana ya uchaguzi kuwa anayeshinda anatangazwa. Ila kwa assessment based na hali ilivyo, Lissu atashindwa na hatakubali kushindwa. Siku zote huwa kuna correlation kati ya ushindi wa viti vya ubunge na kura za urais. Huwa haiwezekani mtu adai kushinda urais halafu ukiangalia viti vya ubunge alivyoshinda haviakisi ushindi wa kura za urais. Kumbuka kura za ubunge ni rahisi hata kila chama kujihesabia na kujua kana kilishinda au la.

Watu wanadhaniwa kuwa ni wengi katika mIkutano ya Lussu ndio hao hao wanaojaa katika mikutano ya CCM. Angalia tu mtaji wa wanachama wa kila chama kwanza kabla ya kufikiria wapiga kura wengine.
Usijiweke katika boksi unalojua halina hewa, na kulifunga kabisa ili ukose hewa.

Hiyo 'correletion' unayoiandika hapa siyo 'absolute'. Kuna mifano mingi sana duniani ambako rais alipatikana bila ya kuwa na wingi wa wabunge. Hili hutokea mara nyingi tu duniani, kwa nini lisiweze kutokea hapa. Watu wasipompenda mgombea urais wa chama, sio lazima wasimpende anayegombea ubunge.
Inaeleweka sana kwa CCM kuitumia dhana yako hiyo kuhalalisha ushindi wa urais hata kama ni kwa kuiba kura. CHADEMA wasikubali huu uinga.
 
Mbona malalamiko aliyoyaleta yeye hayajajibiwa?
 
Tatizo lipo hapa mkuu, kwa sabau Lissu hazungumzi maneno ya kupuuzwa, ndio maana wahusika wanahangaika sana.
Watu wanamwelewa vizuri sana Lissu, kwa maana anasema mengi wanayoogopa kuyasema wengi wa hao watu.

Nakushukuru kwa ufafanuzi wako, kwani nimekuelewa vizuri. Sasa najua msimamo wako haujaathirika na lolote.
Ukweli hauwezi kuhodhiwa na mtu yeyote yule, na utabaki kuwa ukweli.
.Lissu anaposema waliompiga risasi wafichuliwe, hilo litaendelea kugusa wengi.

Tatizo la Lissu liko kwenye kuanisha sera zake kinaga ubaga na mikakati endelevu ya maendeleo kwa nchi nzima.
 
Acha watetee ajira zao,wangejua kuwa mda wa sarakasi ulishaisha wangetulia wakafata kanuni. Mbona hiyo kipara hajajibu hoja ya Lisu kuhusu barua za malalamiko ya chadema kuhusu magufuri.

Jitu bila aibu et linatoka mbele ya kamera kuharisha likidhan wtz wote ni wanaccm. Eti kamat ya vyama vya siasa.shame on you NECCM.Ila huu mziki wa 2020 mpaka familia zenu zinawaona mlivo pumba.kwani mkitenda haki magufur atawafunga ama!.2020 ndo mwisho wa ujinga wenu. warahi mtakuja mfirisiwe hamtakuja kuamini nawaambia.
 
Ukweli hauwezi kuhodhiwa na mtu yeyote yule, na utabaki kuwa ukweli.
.Lissu anaposema waliompiga risasi wafichuliwe, hilo litaendelea kugusa wengi.

Tatizo la Lissu liko kwenye kuanisha sera zake kinaga ubaga na mikakati endelevu ya maendeleo kwa nchi nzima.
Ningependa sana kujadili nawe hii habari ya sera za CHADEMA na uelewa wa wananchi juu ya sera hizo. Nina hakika kuna sehemu kadhaa tutakazokubaliana kati ya wewe na mimi. Lakini najua wakati wa kufanya hivy umepita tayari.

Ninaloweza kukueleza hapa ni kwamba, endapo wananchi watampa ushindi Lissu sio kwa sababu ya sera nzuri, au jinsi alivyozielezea sera hizo. Maoni yangu ni kuwa uchaguzi huu ni zaidi ya sera.
Na hata ukiiangalia CCM na sera zake, sidhani kuwa ni sera hasa zitakazowabeba endapo watashinda uchaguzi huu. Sera hizi zimekuwepo siku nyingi sana na watu wanajua tofauti ya kuwa na sera na utekelezaji wa sera hizo.

Kwa maoni yangu, kama waTanzania tungekuwa tumefikia upeo fulani wa uelewa, sera kuu kabisa ambayo ingeamua uchaguzi huu ni UHURU, HAKI ZA WATU na UTAWALA BORA. Hakuna sera iliyo kuu zaidi ya hiyo hapo.
 
Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Taifa yabainisha uongo wa Tundu Lissu na kueleza yafuatayo:
1. Siyo NEC iliyompa adhabu kama anavyotangaza bali amepewa na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ambayo wajumbe wake ni vyama vyote 15 ikiwemo Chadema na 11 ya wajumbe hao wameona Tundu Lissu ana atia
2. Tundu Lissu alipokea barua na alijitetea mbele ya Kamati kupitia mawakili wake wawili na kuomba Kamati impunguzie adhabu. Hii maana yake ni kuwa walikiri ana makosa
3. Sheria inataka taarifa ipewe vyama siyo mgombea binafsi na utaratibu kama huo ulishawahi kutumika Tundu Lissu alipopewa madai na TADEA na alijibu madai hayo yaliyowasilishwa kupitia CHADEMA kama ilivyo utaratibu.
Mengine sikiziza mwenyewe. Hakika Tundu Lissu ni mwongo na anadhamira mbaya na nchi yetu ili kuwafurahisha mabeberu wake. Chukua hatua na akili kichwani. Achana na Tundu Lissu.
 
Hata wafungie kampeni Hadi tarhe 28 kura yangu kwa lissu
 
Huyu babu tapeli anaongea nini hapa zaidi ya porojo, sisi tupo na Lissu hahitaji hata kampeni. shame on them

Babati unaona alichofanya Tundu Lissu kudanganya umma ni sawa?. Yaani mgombea wa Urais anasema uongo wa wazi na kudanganya umma huku akijua anachosema ni uongo. Yaani huko amepeleka mawakili wake nguli kumtetea na kuomba apunguziwe adhabu, huku kwenye public anasema hajapokea barua na hajapewa nafasi ya kujitetea. Akili yako kichwani ndugu. Lissu ni sumu
 
Back
Top Bottom