Hapa inaonekana unaleta tafsiri yako mwenyewe ya 50/50, hii package nzima nzima bibie kuanzia akili mpaka mitazamo, sababu katika hiyo 50/50 mwanamke kajazwa ujinga ya kuwa mwanaume ndio adui yako namba moja na ni mshindani wako pia, kitu ambacho si sahihi.
Asili ya mwanamke ni kubaki nyumbani hii ni tangu na tangu, mwanamke kutoka ni kumtafutia matatizo kama anayokumbana nao leo, shida yenu sio wakweli katika maneno wala vitendo.
Usidanganye watu bibie huwezi kufanya kazi na ukafanikiwa katika malezi, hili halipo bibie. Hizi kazi zenu za maofisini sio kweli.
Malezi ni mjumuiko wa vitu vingi, ni kutoa elimu, kuhudumia, kudumu muda mwingi na mwanao na kurekebisha, watoto wenu mnao waachia dada wa kazi useme unalea ? Au unafikiri kulea nikumchambisha tu mtoto, au kumlisha au ?