Tunarudi kule kule, wanaume wanyanyasaji wapo au hawapo?! Yani kwanini mnageneralise wanawake wote? Mngeanzia kwenye chimbuko la kwanini mwanamke amefika hatua ya kujipambania. Ni kwamba wanaume mlimmis use power zenu!! Full stop. Hatukatai wanawake wanaojisahau wapo lakini hiyo sio sababu ya kusema wanawake kuwa makazini ni tatizo. Sema kila mtu a deal na mke wake nyumbani! Na ndo unakuta mwanaume
Akioa tu, anamuachisha kazi mkewe bila
Hata kumpima kama anahekima yakusimamia nafasi au la.
Kwa dhana hiyo ya kugeneralise basi tutengeneze sheria kwamba mwanaume yyote anaenyanyasa mwanamke auwawe kama mnavyotaka wanawake washinde majumbani kulea watoto.
Sijui hata kama tunaelewana au mnakaza mafuvu tu
Aisee wewe ni much know halafu mbele kiza.
Mwanamke sababu ya kujipambania sio kwasababu mwanaume alimnyanyasa,kuna sababu nyingi za mwanamke kupambana na pia nj vizuri mwanamke kupambana,sababu hizo ni kama ifuatavyo;
1)Hali ya maisha ya kwao alikoanza kuishi,wengine toka wadogo wameanza kupambania maisha yao,mfano mamaangu mzazi,alianza kazi akiwa mdogo huku anasoma,maaba hakukuwa na mtu wa kumuunga mkono na babu alifariki ye akiwa mdogo sana.
2)Kujitegemea kwaajili ya matumizi binafsi na maendeleo binafsi,hili pia mwanamke linaweza mfanya apambane,na wala sio jambo baya maana wanawake mna mahitaji mengi mengine madogo madogo huwa mnaona ni sahihi mjitimizie wenyewe.
Kiufupi jambo la mwanamke kupambana sio baya,ila je anapambana kwa namna gani na kwa mazingira gani??
Je unataka kusema wanawake wenye pesa hawanyanyaswi!!??
Wapo wanawake wenye pesa na wananyanyaswa vile vile.
Haki sawa kwa wote ilikuja kwaajili ya kumpa mwanamke nguvu ya kuweza kujitetea,na kujitetea huko sio kwa pesa,bali kwa kupewa usawa sawia na wa mwanaume kimaamuzi,kiajira n.k n.k ikienda sambamba na sheria za kumuwajibisha mwanaume ataemnyanyasa mwanamke.
TAMWA na TAWLA ndio moja wapo ya vyombo vinavyotekeleza hilo.
Akili yako inajijengea kuwa mwanamke anapambana kwasababu alipitia manyanyaso hapa unakosea.
Tatizo lililokuwepo hapa hili suala la haki sawa kwa wote limewafanya mjisahau ninyi ni kina nani.
Asilimia 90 ya wanawake wa siku hizi mnajifanya wajuaji,hamtaki kuelekezwa na wala hamtaki kuongozwa.
Mwishowe mnaishia huko mnakoishia.
Point kuu narudia pale pale msijisahau ninyi ni kina nani katika jamii.
Licha ya kipato jitambueni na mplay role yenu kama wanawake katika jamii.