Katikati ya harakati za 50/50 kinyume chake wanawake wengi siku hizi hawana furaha

Katikati ya harakati za 50/50 kinyume chake wanawake wengi siku hizi hawana furaha

Nikiwa darasa fulani la sheria mwaka 2018 niliwahi kuuliza hivi "je, kwa harakati hizi za 50/50, mizani ikizidi yaani wanawake wawe juu zaidi, zitaanza harakati za kuwashusha wanawake na kuwainua wanaume?"
 
Je bibi hakuwa anafanya kazi? Ndio mnawadanganya wanawake ili muwape mikopo uchwara ya biashara n.k inayowapelekesha resi kama wanevuta bangi

Sijakuelewa Mkuu.

Bibi yangu alikuwa Mwalimu kipindi cha Nyerere, Mwinyi na Mkapa.
Kwetu Mwanamke lazima afanye kazi iwe ya kuajiriwa au kujiajiri.

Kuchukua mkopo ni ishu nyingine Mkuu.
Kwani wanaume hatuchukui Mîkopo?
Taifa lako unajua linadaiwa kiasi gani?
Marekani ambaye ndiye kiranja wa dunia unajua anadeni kiasi gani?

Kama mwanaume ni vizuri kujadili mambo kwa mantiki ili kulinda heshima ya uanaume ambayo Mungu alitupa.

50*50 hata mîmi sikubaliàni nayo katika baadhi ya muktadha lakini hiyo haimaanishi kuwa muktadha mwingine isitumike.

50*50 katika kupata haki za kupata huduma za kijamii kama elimu, afya, fursa, n.k. ni sahihi.

50*50 katika wajibu na majukumu ya kifamilia hapo lazima umakini uwepo. Huu itatokana na kuwa familia ni taasisi aû ufalme mdogo unaojitegemea
 
Huyu mtoa mada hanaga linguine zaidi ya kuongelea 50/50 kama li mke lako ni Limama la nyumbani then tulia, hii vita ya kusafisha 50/50 won't get you anywhere...pumbafu.
Af wenzie wanamtetea eti hajaongelea kwa ubaya🤣 tushawahi kupopoana kwenye mada na huyu jamaa mwaka 2022 alikua anatukana wanawake kinoma. Nahisi kaoa jitu gani sijui au bosi wake ni mwanamke basi anamsumbuaa
 
Dunia haimsubiri mtu, kaeni hapo kusubiri wanawake wabadilike muone kama dunia inarudi nyuma. Stress ni part ya maisha ya mwanadamu, kivipi stress itumike kama tusi?

By far kunafaida lukuki za maisha katika mfumo wa sasa, kuliko mfumo wa uzamani, ndio maana baba na mama zenu waliona ni vyema kumuwezesha mwanamke ili ajitafute kiuchumi kuliko walivyopata kuishi wao.

Zamani wanawake hawakuwa na stress au hakukuwa na social interaction ya kudisplay hizo stress zao? Msipende kuwaongelea wanawake wa zamani kabla hamjavaa viatu vyao kuona how did they feel about the world... wanawake wazamani kupigania uwezeshwaji wa mtoto wa kike, ni ushahidi tosha kuwa walikuwa na stress zao, zilizopelekea wao kuona mwanamke akiwezeshwa kuna aina ya stress itaondoka, unfortunate imeondoka hiyo imekuja stress mpya, which
is okay, mnategemeaje maisha bila stress? Again we are tired with ya'll weak minds mnaotamani dunia ambayo ni stress free... mko delulu.

Mnajadili mada makini kibinafsi na kiufunyu wa fikra sana, na haisaidii wala haijengi.
 
Tulikosea kuipokea hii sera ya usawa. Ni either tungeachana nayo kabisa au tungeifanyia marekebisho iendane na maisha yetu kimaadili na kiuchumi. Wanawake waweke ego pembeni waifanyie tathmini hii sera ya usawa kuona kama imejenga au kubomoa taswira na mustakabali wao kwenye jamii
Kabisa, hawa wanaojiita wanaharakati wanawaharibia wenzao tu wengi wenyewe wameshapigwa matukio. Shida ni pale tunapotaka mwanamke afanye majukumu ya mwanamme na mwanamme afanye ya mwanamke. Hii ni shida sana tusipokuwa makini kulinda utamaduni wetu tutaishia kama watu wa west, kuwa na maisha mazuri bila furaha kwani wanawake wamechukua power sana kiasi family zinayumba kila leo.
 
Sasa swali langu linakuja. Wewe income yako ni kama GSM? Mimi nimetoka kwetu napata kila kitu, nikaanza kazi nijihudumie,
Umekuja kunioa ukasema niache kazi nilee watoto , nyumbani unaniachia elfu moja ya dagaa wanangu wale, wewe unaenda kukesha bar, kwakuwa mama yako hakusoma, baba yako alikupeleka shule ya kata unataka na wanangu wasome kata kwakuwa wewe huna uwezo, nakaa nyumbani nafubaa kama mzee wa miaka 60 kisa mume wangu hataki nifanye kazi nibaki nilee watoto,

Ukirudi nyumbani unanikuta nimefubaa huvutiwi tena na mimi ulienioa miaka 7 nyuma nilipokua najinunulia lotion ya 35,000. Saizi unanipakisha minara coconut oil. Unaenda kazini kwako unakutana na secretary anapaka lotion ya 20,000 anapendeza anawaka unamtamani unakaa ukimwambia mke wangu hana mvuto tena. Wanaume mna utindio si eti?

Nani aliwadanganya kuwa kupinga 50/50 ni lazima mwanamke abaki nyumbani? Personally huo ujinga wa 50/50 siutaki kwangu hata sukari ikiisha sinunui bila mahesabu. Nilishamtengenezea Mr kwamba mimi ni support yako. Pale unapotoa mimi ndo ntaongeza kama kuna ulazima. Gharama zangu za maisha ni kubwa, hujanioa ili u shrink my standards otherwise ungeenda kuoa kijijini kwenu sitimbi huko. Na kazi nafanya na wanangu nalea. Hivi mfano kazini umefukuzwa ghafla na akiba huna tunaishije nyumbani? Mwanaume huna uwezo wa kunitunza huna unakomalia nikae nyumbani nivae madera. Are you serious? Kazi nafanya kama kawa na familia yako utaihudumia maana wewe ndo baba.

Wanaume wengi mnataka mwanamke ambae anakaa nyumbani ili umnyanyase. Au sio.
Muwe na uwezo wa kuwahudumia basi sio mke anamiaka 30 anafanana na kabibi ka miaka 65.

50/50 ni kwenye fursa kwa sababu hawa waliosoma waende wapi? Kama wanaume mngekua that smart si mngekua mnaongoza peke yenu madarasani. Ndo maana kuna vilaza na kuna wanawake wanaongoza. Acheni ubinafsi.

Most of us submissive women tuko makazini na ndoa zetu wanaume tunawaheshimu vizuri tu.

Tena wanawake acheni leo niwape siri, ukitaka kumcontrol mwanaume kuwa submissive. Yani shingo ndo inazungusha kichwa. Sitawafundisha kila kitu. Mwanaume akirudi nyumbani muoneshe heshima zote, mkiwa public mtreat kama mfalme uone kama hato fall for your desires.

Hawa wa jamii forum wengi wanachuki za bure na wanawake na kuna mahali wanashindwa kuelezea wanachotaka. Chanzo cha wanawake kutokua na heshima sio kazi walizo nazo bali ni jinsi wanaume mlivyoshindwa ku play part zenu,yani mwanaume anashinda bar, ana shinda anabet, kila akirudi hana hela, watoto wanarudishwa ada. Na mke alisoma ana kadregree akae nyumbani kisa mume atajiskia vibaya? Stupid
Umeongea kwa hisia lakini umeongelea aina moja ya mume sasa swali kwako, je kama una mume anayewajibika kama mume. ana provide mahitaji yote muhimu, akitoka job yuko nyumbani tu na wewe na akitoka na family yake, kujumla anatimiza kwa uwezo wake mahitaji yako kifedha, mapenzi na uaminifu. Kama mke nini zaidi utataka kwa mume? Point moja muhimu umeongea mume mnyime chochote lakini red line ya mume ukimvunjia heshima kama humuheshimu basi ndoa inaenda kufa.
 
Zama za mwanaume kuwa mtawala badala ya kiongozi zimepitwa na wakati....

Any man even zero brains wanaweza kuwa watawala kwenye familia zao ila VERY FEW MEN wana karama ya kuwa viongozi wa familia zao

Viongozi 50/50 sio shida zao, wamechagua wanapopamudu na familia zimeendelea kuevolve bila shida
Hakuna nyumba ikasimama imara ikiwa mke anamtawala mume hata kama mke ana kipato kikubwa kuliko mume lakini kama humpi nafasi ya mume kuwa kiongozi wa family basi haitadumu. Ila kuongezea hapo hata mume kuwa kiongozi sio kwamba ndio awaburuze tu hapana, mume mwenye busara kama kiongozi ni kumshirikisha mke katika mambo ya maamuzi hata kama yeye ndio mwenye sauti ilajenga mapenzi.

Umeongelea mume zero brain, sasa wakati unamkubali hukujuwa kama ni zero brain? Mfano mmoja tu, ofisi unayofanya kazi labda una Manager lakini haina maana kuwa hakuna watu wa chini labda wana uwezo kuliko huyo Manager lakini ni lazima utampa heshima kama kiongozi basi na family is the same.
 
Peace,

Itakushangaza lakini ndio ukweli, tupo katika zama za upendeleo na "kuinuliwa" kwa wanawake na fursa kede kede pasina shaka mimi na wewe tulitegemea ustawi wa wanamakae kiuchumi, kiroho, kijamii, kiakili na kua na furaha zaidi ila sasa hali ni tofauti kabisa.

Mazingira ya ajira na kazini yanamfanya mwanamke kua compititive na aggresive akipoteza kabisa ile setup na tone ya mwanamke.

Wanawake wengi japo utawaona katika vyeo tofauti na huko maofisini wakipewa promotions kede kede ila ukiwatizama usoni hakuna nuru wala furaha yoyote yani wamekua mangangari, madumejike fulani kisirani ile hali ya uanamke imewatoka wako na mastress full tank.

Kupishana na wanawake njiani wanaongea wenyewe imekua kawaida sana. Wamekua watu wa kupenda mabishano kila mara, visirani, jeuri na watu wa shari. Unaweza kumsalimia mwanamke kama hakukusikia vizuri akakujibu "kwa kufoka akijua ulimsema kw ubaya inshort wako aggresive mda wote ego iko juu zaidi za mawingu.


Kuna member mmoja humu jf wiki chache alipost uzi kua "wanaume siku hizi wamepunguza na hawatongozi tena kama zamani" nakubaliana nae kwa 100% hata mimi kutongoza kumepungua sana maana ule utamu wa mwanamke uliotupelekea kutongoza (sio wote) haupo tena njiani unapishana na madume jike tu yamefura visirani sasa nitongoze ligalagala la nini ?!


Hawana furaha tena wala utilivu wa akili na hata kiuchumi wanawake ndio wamekua wadangaji kuliko kipindi chochote katika historia ya mwanadamu yani mambo yamekua vice versa haki sawa imekua ni jabali linalowatesa wanawake wenyewe.

Ukikutana na hawa wanamake wa haki sawa hata mkizungumza wanapenda mbishane tu hawataki utulivu ghasia, mivutano na majibizano ni sifa yao kuu. Wamejaa negativities deep down their bones.

Zamani ulikua ukimuona mwanamke mwili unasisimka, sasa haya magalagala madumejike ya siku hizi unalitazama unaona kabisa uanamke haupo lidude limekaa hapo limekutolea macho pima kama fundi saa.

Nyie ni mashahidi hata masingle mother wanaongezeka kwa kasi ya 4G kwasababu hiki kizazi cha haki sawa hakina ile haiba ya mwanamke ni mangangari ngangari full jeuri.
Unahoja ila umesimanga sana mkuu 😀. Hata talaka zimekuwa nyingi, achilia mbali uoaji wenyewe pia ni kama unatoweka.
 
Umeongea kwa hisia lakini umeongelea aina moja ya mume sasa swali kwako, je kama una mume anayewajibika kama mume. ana provide mahitaji yote muhimu, akitoka job yuko nyumbani tu na wewe na akitoka na family yake, kujumla anatimiza kwa uwezo wake mahitaji yako kifedha, mapenzi na uaminifu. Kama mke nini zaidi utataka kwa mume? Point moja muhimu umeongea mume mnyime chochote lakini red line ya mume ukimvunjia heshima kama humuheshimu basi ndoa inaenda kufa.
There is an exception to the general rule.

Sasa mimi kinacho nishangaza ni vile wanaume wa jf wanavyo generalize kwamba wanawake wote wanaofanya kazi ni madume
Jike as if hao wote waume zao ni sweet loving husbands. Wanahesabika mkuu. Sijui niwaambiaje
 
Turudi miaka 50 nyuma, wanawake hawakuwepo kwenye nafasi mnazosema walikua wanashinda majumbani kulea watoto, je, wote waliolewa? Wote walidumu
Kwenye ndoa zao miaka yote? Hapakua na single moms? Wanaume ndo walikua wanazaa kama kuku mnakuja kujua siku za misiba.

Wanawake walikua wananyanyaswa kwasababu hawakua na kipato. Ndo chanzo cha harakati. Na harakati zilipoanza hawakumaanisha 50/50 kwenye familia bali kwenye fursa ili wanawake wajitafute wasiwe wananyanyasika majumbani.

Sasa mnataka turudi kwenye zile zama ili tuwe tunapigwa au shida ni nini?

Hao wanawake wanaofanya kazi waache waende kudanga ndo mfurahi?? Au mnataka wote wawe wauza baa.

Baadhi ya wanaume kuna kitu kina nipa alert mna shida mahali. You are intimidated by women’s success kwasababu hata wanawake ambao hawana kazi bado mnawa cheat, bado mnawazalia watoto mnawaleta kwasababu mnajua hawana pa kwenda. Hicho ndo mnachotaka.

Men step up your game. Vaeni mamlaka sio kulalamika kwenye forums. Kazaneni kufanya kazi mtuzidi vipato.
 
Telenovela unayosimulia haina director mzuri nenda katunge tena. Hiyo kitu haipo!

Tukirudi kwenye uhalisia, mwanaume hana kazi na anataka mwanamke amwabudu aache kazi walie wote njaa. Niite mbishi ila kazi huniachishi.

Kama story unayoisimulia ingekua kweli ningekuuliza hivi Ina maana wakati hamjaoana alikua anarudi saa tisa na nusu jioni ila ulipomuoa akawa anaongeza muda wa kuchelewa kurudi? Inferior men are scary. Mngekua mnawajali wanawake wenu mkiwaachisha kazi hamuendi kuchepuka na kuzalisha michepuko mbona fresh tu. Ila mwanamke anapambania future ya wanae anawatengenezea akiba kwasababu tunajua wanaume wengi nguvu za kiume hamna ila mko busy kutembeza hizo rungu kuonesha vilema
Vyenu mnasahau family kwa ulimbukeni
Nikisoma maandishi yako, sio bure una stress na Kuna vitu ume/unapitia...pole, ila tafuta professional counseling.
 
There is an exception to the general rule.

Sasa mimi kinacho nishangaza ni vile wanaume wa jf wanavyo generalize kwamba wanawake wote wanaofanya kazi ni madume
Jike as if hao wote waume zao ni sweet loving husbands. Wanahesabika mkuu. Sijui niwaambiaje
Hili sio sawa kila familia ina changamoto zake wengine ni lazima kila mmoja afanye kazi ili maisha yaende ila kubwa la msingi haijalishi unafanya kazi au mke wa nyumbani basic ni zile zile kuheshimiana. Labda wale wanawake wakianza kufanya kazi basi wanajiona wako sawa na mume. Tujikumbushe hotuba ya Rais wetu, alisema pamoja kuwa yeye ni Rais wa nchi lakini kwa mume wake anampigia goti, powerful message.
 
Hili sio sawa kila familia ina changamoto zake wengine ni lazima kila mmoja afanye kazi ili maisha yaende ila kubwa la msingi haijalishi unafanya kazi au mke wa nyumbani basic ni zile zile kuheshimiana. Labda wale wanawake wakianza kufanya kazi basi wanajiona wako sawa na mume. Tujikumbushe hotuba ya Rais wetu, alisema pamoja kuwa yeye ni Rais wa nchi lakini kwa mume wake anampigia goti, powerful message.
Hiki sicho ambacho wana ki advocate wanaume wenzio humu. HAWATAKI MWANAMKE AFANYE KAZI! Sijui tunaelewana. Yani hilo suala la heshima ni la kwako wewe. Kwasababu sio kweli kwamba wanawae wanaofanya kazi wote hawaheshimu ndoa zao na sio kwamba wasiofanya kazi wanaheshimu waume zao.

Kuna mentality hapa ipo na ndo nnayoikataa. Wenzako hawataki wanawake wafanye kazi because wanaamini automatically mwanamke atakua na dharau. Sijui kwanini wako negative kiasi hiko.
 
Hiki sicho ambacho wana ki advocate wanaume wenzio humu. HAWATAKI MWANAMKE AFANYE KAZI! Sijui tunaelewana. Yani hilo suala la heshima ni la kwako wewe. Kwasababu sio kweli kwamba wanawae wanaofanya kazi wote hawaheshimu ndoa zao na sio kwamba wasiofanya kazi wanaheshimu waume zao.

Kuna mentality hapa ipo na ndo nnayoikataa. Wenzako hawataki wanawake wafanye kazi because wanaamini automatically mwanamke atakua na dharau. Sijui kwanini wako negative kiasi hiko.
Labda ndio tujiulize kwanini? Mimi nadhani wanakuwa wanaona wanachowafanyia wake za watu huko makazini au wanaona sasa inawatia hofu japo hata mke wa nyumbani tu anaweza kufanya. Ila lazima tukubali kuna mambo yapo yanatokea ndio chanzo cha hii hofu. Yes sio wote ila chance ya kushawishika huko ni kubwa lakini nasema tena sio wote.

Sasa mimi kama mimi, sipendelei mke wangu afanye kazi ya kuajiriwa ila ni wajibu wangu kutimiza part yangu, na sababu ziko nyingi. Mkiwa mna familia changa Mme katoka asubuhi mke katoka asubuhi mnarudi jioni watoto wako na dada hii inanipa shida sana, gharama zake huko mbeleni zitakuwa kubwa sana. Ndio maana nimesema tugawane majukumu mimi nitafute wewe angalia familia. Tukianza kuingiliana majukumu ndio shida inakuja hapo.

Mke akiwa home tu hakuna mtu atauliza kwanini, sababu yuko kwenye jukumu lake lakini mwanamme akikaa home tu inakuwa issue, mke mwenyewe atamwambia mume wangu toka uhangaike sababu sio sehemu ya jukumu lake kukaa home tu.
 
Labda ndio tujiulize kwanini? Mimi nadhani wanakuwa wanaona wanachowafanyia wake za watu huko makazini au wanaona sasa inawatia hofu japo hata mke wa nyumbani tu anaweza kufanya. Ila lazima tukubali kuna mambo yapo yanatokea ndio chanzo cha hii hofu. Yes sio wote ila chance ya kushawishika huko ni kubwa lakini nasema tena sio wote.

Sasa mimi kama mimi, sipendelei mke wangu afanye kazi ya kuajiriwa ila ni wajibu wangu kutimiza part yangu, na sababu ziko nyingi. Mkiwa mna familia changa Mme katoka asubuhi mke katoka asubuhi mnarudi jioni watoto wako na dada hii inanipa shida sana, gharama zake huko mbeleni zitakuwa kubwa sana. Ndio maana nimesema tugawane majukumu mimi nitafute wewe angalia familia. Tukianza kuingiliana majukumu ndio shida inakuja hapo.

Mke akiwa home tu hakuna mtu atauliza kwanini, sababu yuko kwenye jukumu lake lakini mwanamme akikaa home tu inakuwa issue, mke mwenyewe atamwambia mume wangu toka uhangaike sababu sio sehemu ya jukumu lake kukaa home tu.
Hongera kwa kutumia neno baadhi. Sasa ndo unaelewa nnaposema wenzio wana generalize. Yani mimi niko kazini na sijawahi kuwa na mahusiano na mtu yoyote. Na kwa maisha ya sasa hivi mwanamke tegemezi ana kipengele cha maisha ya manyanyaso asipokua makini.
Rai yangu: wanaume wabaki na matamanio yao ya kuoa wanawake wa kuwaweka ndani ila wakawatoe kijijini, sio hawa ambao wazazi wao wamewasomesha hadi nchi za nje af uje umuachishe kazi.

Hawa mnaowaona mjini kama wanaliwa kwani ni wa kwenu? Kila mtu apambane na ndoa yake.

Kinachonishangaza zaidi kila siku ni mada kuhusu wanawake lakini hakuna anaeongelea kuhusu hawa wanaume marioo, yani huyu anataka atumie ela za mwanamke kwenda kufanyia uanaume
Wake wa kuzaa nje, kuna vitu vinachekesha sana
 
Kuna mdada jana nilikaa zangu sehemu kuna kama kagiza hivi akaawa amekuja na mwenzake mimi simfahamu ila namfahamu huyo mwenzake na huwa tuna utani wa kuitana mama na mtoto wake.

Sasa jana, akaja na huyo dada dukani mimi nimeketi kwa pembeni kuna kama kagiza hivi nimevaa sweater la hood nimejifunika ngumu mtu kunijua.

Sasa walipofika, yule dada ninayemjua akaniamkia kwa adabu na yule mwenzake akaunga tela kuniamkia, nikawaitikia kwa sauti ya uzito hawakunijua, wakaenda dukani na kutoka sasa wakati wakirejea kutoka dukani ndipo nikawaita kwa kumwita yule ninae mfahamu, aliponijua akacheka sana akawa ameanza utani kwa kunambia nimepokea shikamoo wakati mtoto wa juzi tu hapa najifanya mzee. Me kwa masihara nikamjibu sasa shikamoo kupewa na mwanamke si ni halali kwanza mwanaume mkilingana umri au akikuzidi hata mwaka m'moja unatakiwa kumuamkia. Akacheka sana halafu akawa anamwambia mwenzake kuwa tumemwamkia bwana mdogo huyu atupe shikamoo zetu.

Sasa yule demu akawasha tochi ya simu akanimulika usoni, mimi nikamwambia yule ambaye ninamfahamu kwamba yeye anamind shikamoo yake wakati mwenzake ameridhika kabisa kunipa shikamoo tena kwa adabu. Weeeeee yule demu ghafla sura ikabadilika. Anaonekana ni msimbe wa kama miaka 34 kama sio 35.

Aiseee sura ikawa utadhani mtu aliyemuona X wake aliyemtelekeza na watoto. Akasema yaani me najua ni mtu mziiiima kumbe katoto tena ka elfu mbili, me nikamwambia kwan kama nimezaliwa 2000 kuna ubaya gani ukinipa shikamoo yangu kama kidume, akajibu kidume utakuwa wewe me nikupe shikamoo kwa kipi unachostahili? Imagine huyu mtu hatujuani ndio kwanza nimemuona hapo kwa mara ya kwanza ila ndio ameanza kuwa na maneno ya kashfa kwa kitu ambacho kingeweza kuwa utani tu na tukamalizana bila alterations zozote.

Akawa sasa kama mtu amepigwa na shoti midomo,sura na mwili unamuona kabisa inatetemeka anaonekana kama alipatwa na jazba kali akawa kama anataka kuanzisha tifu ili tuanze rushiana maneno. Mwenzake akashtukia akaanza muondoa ile ya utani huku ananiambia hiyo shikamoo utarudisha hata kwa makonzi. Me nikawa namzingua yule mwenzake nikamwambia sirudishi tena ya mwenzako nimeipenda nataka tukikutana tena ndio iwe utaratibu, demu akajibu nenda nyumbani ukabadilishwe Pampers na mama haraka unachelewa. Hapo uso alioweka ni ule wa hasira.

Sasa unachosema mleta uzi si jambo la uongo kabisa ni ukweli kabisa hii kitu na si kawaida. Sijui ni chakula, hormones, hali ya hewa ama kitu gani, wanawake wa sasa hata mama zetu wanakiri kuwa kuna shida eneo la tabia. Tukiwasema wanasema tunawaandama.
 
Muachishe huyo zombie wako kazi. Kwani walioko makazini nao ni wake zenu? Mbona mna uchungu nao sana!

Au mnatamani muwe mnavaa pedi pia maana sielewi hasira ni za nini!
Duh unaonekana una hasira wewe...
 
Back
Top Bottom